Thursday, November 6, 2008

Demokrasi yaleta historia.

Demokrasi yaleta historia nchini Amerika, Baraka Obama, mwafrika wa kwanza kuwa rais wa Amerika.

Illinois,Amerika-5/11/08. Mgombea urais kupitia chama cha Demokrat nchini Amerika , Baraka Obama amechaguliwa kwa kura nyingi kuwa rais wa nchi hiyo, kwa kumshinda mpinzani wake John McCain wa chama cha Republikan
Kuchaguliwa kwa Baraka Obama kuwa rais wa Amerika, kume weka historia ya nchi hiyo, kwa kuwa rais wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika kuwa rais.
Baraka Obama mwenye miaka 47, atakuwa rais wa 44 wa Amerika.
Ushindi wa Baraka Obama, kumeleta hisia tofauti duniani, na amepongezwa na viongozi karibu wote wa dunia.
Picha hapo juu, wanaonekana rais, Baraka Obama akiwa na makamu wake Joe Bidenn wakiwa wanawapungia mikono kuonyesha ishara ya shukurani na kwa wananchi kuwaamini na kuwachagua kuongoza nchini.
Picha ya pili, ni picha ya rais Baraka Obama.
Picha ya tatu, wanaonekana rais, Baraka Obama na mkewe Michelle Obama, wakipiga kura siku ya tarehe 4/11/08,, siku ambayo historia iliwekwa kwa, Baraka Obama, kuchaguliwa kuwa rais.
Picha ya nne,anaonekana rais mpya wa Amerika, Baraka Obama enzi ya utoto wake , akiwa anaendesha baiskeli wakati wa utoto wake, na sasa ameshika uskani wa kuendesha uongozi wa Amerika.
Picha ya tano rais Baraka Obama,akimsikiliza makamu wa rais Joe Biden,hii inaonyesha ya kuwa katika uongozi kusikilizana ndiyo chanzo cha uongozi bora.
Picha ya sita anaonekana rais, Baraka Omaba, akiwa na bibi (nyanya) wakati alipo kwenda kumsalimia kijijini Kogelo alipo zaliwa baba yake nchi Kenya.
Picha ya mwisho, anaonekana rais mpya wa Amerika, Baraka Obama, akiwa na familia yake,toka kulia ni mke wake, Michelle Obama, Malia Ann Obama, na Natasha ( Sacha) Obama, wakiwaamkia wananchi waliokuja kushangilia kwa pamoja kuchaguliwa kwa bwana baraka Obama kuwa rais wa Amerika.

No comments: