Wednesday, November 26, 2008

Maendeleo ya China yawa kitendawili kwa dunia"Usili ndiyo kikwazo"

Wairak wavutana kuongezewa muda kwa jeshi la Amerika.

Baghdad,Irak- 25/11/08. Mjadara mkali ambao unaendelea kukubaliana kwa wanchi wa Irak, kukubali kubakia kwa jeshi la Amerika na washirika wake kwa kipindi cha miaka mitatu, umefikia njia panda, baada ya mvutano mkubwa ulio tokea katika bunge la Irak, ili kukubaliana mswada huo.
Amerika yenye wanajeshi wapatao, 150,000, wapo nchini Irak.
Kufuatia mvutano huo, bunge limekubali kwa pamoja ya kuwa kura ya maoni huenda ikatumika ikiwa bunge litashindwa kukubaliana kupitisha muswada huo.
Bunge hilo, linalo jumuisha makundi makubwa ya yaliyo gawanyika kidini ,Suni,Shia na Kurdi.
Picha hapo juu anaonekana, waziri mkuu wa Irak, Nuri Kamal al Maliki, akiongea hivi karibuni kusisitiza lazima kuwepo na uhusiani kati ya Wairak.
Picha ya pili anaonekana,mwanajeshi mmoja wa jeshi Ameria akiwa amesimama nyuma ya muhimiri, huku akitizama usalama wa jamii japo wamekuwa na wakati mgumu wa kuleta usalama wa raia nchini Irak.
Picha ya tatu wanaonekana wananchi wa Irak, wakiandamana hivi karibuni siku ya tarehe 21/11/08, karibuni kupinga kuendelea kuwepo kwa jeshi la Amerika nchini Irak.
Maendeleo ya China yawa kitendawili kwa dunia"Usili ndiyo kikwazo"
Washington,Amerika - 23/11/08.Chifu Marshal wa maswala ya ulinzi nchini Amerika, Angus Houston, amesema kuwa maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia yanayo fanyika kisili nchini China yanaleta hali ya kutokuwa na usawa.
Chifu Marshal, Houston, alisema mpaka sasa China ajaeleza ni kwanini iliamua kuvunja kwa kuaribu mtamdao wa seteliti uliopo kwenye anga la dunia.
Akiongezea katika mazungumzo haya,alisema matumizi ya, China yamepanda kutoka pesa ya Kiamerika $ 59billion hadi $ 93.5billion na hii ni ongezeko la asilimia, 17.1% na huenda ikafikia 139billion.
Picha ya hapo juu ni bendera ya China, nchi ambayo ina leta vichwa kuuma kwa jumuia ya kimayaifa kutokana na usili wake.
Picha ya pili, ni ya bendera ya jumuia ya Ulaya, jumuia ambayo kwanjia moja kukua kwa teknolojia nchini China, kutathili kwa kiasi fulani jumuia hiyo kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo.
Picha ya tatu, ni ya bendera ya Amerika nchi ambayo ina zidi kuwa na wasiwasi na usili wa China.
Serikali ya Zimbabwe bado yatoa joto ya jiwe kwa jumuia ya kimataifa.
Harare, Zimbabwe - 24/11/08.Serikali ya Zimbabwe imewazui kuingia nchini Zimbabwe kwa kuwanyima visa, viongozi wa zamani wa kimatifa ambao walitaka kwenda kuangali na kutathmini hali halisi ya kijamii nchini humo.
Viongozi hao ambao walizuiliwa kuingia Zimbabwe ni, Kiffi Anan aliyakuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jimmy Carter ambaye alikuwa rais wa Amerika wa 39, na Bi Gracia Machelle.
Picha hapo juu anaonekana, rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akisikiliza kwa makini katika moja ya mikutano ya kuleta suruhisho la kisiasa nchini Zimbabwe.
Picha ya pili wanaonekana, viongozi ambao wamezuiliwa kuingia nchini Zimbabwe kwa kunyimwa viza, kutoka kulia ni Jimmy Carter, Koffi Anan na bi, Gracia Machelle.
Chama kipya cha kisiasa nchini Afrika Kusini chaleta mtikiso wa kisiasa.
Johannesburg,Afrika ya Kusini - 22/11/08.Mwenyekiti wa chama kipya cha siasa nchni Afrika ya Kusini " Congress of the People" Mosiuoa Lekote, amesema kwamba chama hiki kipya kinamwelekeo unao faa kuindeleza nchi, kuwa kipo tayari kuilinda katiba kwa kushirikiana na vyama vingine.
Mwenyeki, Mosiuoa Leketo ni mmoja ya viongozi wa zamani wa chama tawala ANC - African National Congress,ambaye pia ni mmoja ya viongozi waliopigania kupinga utawala wa watu wachache wa makaburu , ambao walileta siasa za kibaguzi za kuwabagua watu waliowengi kwa rangi za miili yao.
Picha hapo juu ni ya mwasisi wa chama kipya cha Congress of the People, bwana Mosiuoa Leketo, akiwa amezungukwa na wananchi wanao kubaliana naye kimsingi.
Picha ya pili, wanaonekana, baadhi ya wanachama wa chama cha ANC - African National Congress, wakiandamana, na mmoja wao akichana kadi kuonyesha ya kuwa hayumo tena katika chama hicho.

No comments: