Sunday, November 9, 2008

Mgogoro wa mashariki ya kati( Palestina na Izrael) bado kitendawili"Niwakati mgumu asema bi,Condeleeza Rice"

Bara la Afrika lajianda na mapokezi ya Papa Benedict XVI mwaka 2009.

Vatican City, Vatican,09/11/08. Papa Benedict XVI, anatarajiwa kufanya ziara katika bara la Afrika mapema mwakani. Kwa mujibu wa msemaji wa Vatican, Papa Benedict XVI,atafanya ziara hii ikiwa moja ya maandalizi ya mkutano na maaskofu kutoka bara la Afrika, utakao fanyika mwezi wa Oktoba 2009. Kwa mijibu wa msemaji huyo, alisema yakuwa Papa, atafanya ziara katika nchi za Angola na Kamerooni. Kamerooni itaandaa mkutano utakao wajumuisha viongozi Afrika wa kanisa Katoliki. Picha hapo juu ni ya Papa Benedict XVI,ambaye anatarajiwa kufanya ziara katika bara la Afrika mapema mwaka wa 2009.

Mgogo wa mashatiki ya kati(Palestina na Izrael) bado kitendawili"Niwakati mgumu asema Condelleza Rice". Sharm el Sheikh, Misri- 09/11/08. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amesisitiza na kuziagiza jumuia ya Ulaya, Urusi na Amerika na kwa kushirikiana na Umoja wa mataifa,zijitahidi kutatua mgogoro wa mashariki ya kati, ambao ni kati ya Palestina na Izrael. Akisisitiza hayo, waziri wa mambo ya nje wa Amerika, bi ,Condeleezza Rice, amesema ya kuwa makubaliano ya kutimiza mkataba wa kuwa na Palestina huru yamekuwa magumu kwa kuzingatia kwa sasa nchini Israel kunatarajiwa kufanyika uchaguzi mwezi wa februari, na kufanya makubaliliano hayo kuwa finyu kwa sasa. Bi Rice, aliongezea kwa kusema yakuwa, serikali mpya inayo kuja ya rais baraka Obama, itakabidhiwa kazi hii. Picha hapo juu anaonekana waziri wa mambo ya nje wa Amerika Condeleeza Rice kushoto akiwa na badhi ya viongozi waliokuja kuuzuria mkutano wa kutafuta kutatua mgogoro wa mashariki ya kati mjini Shrm el Sheikh. Rais wa zamani wa Sudan afariki dunia. Khartoum, Sudan-5/11/08. Aliyekuwa rais wa Sudana Ahmed al Mighani amefariki dunia, akiwa nchini Misri. Rais Ahmed al Mighani,alichaguliwa kuwa rais wa Sudani mwaka 1986 hadi alipo tolewa madaraka na na jeshi lili ongozwa na rais wa sasa, Omar El Bashir mwaka 1989. Akiongeaha yaha kuthibitisha kifao chake, msemaji wa serikali ya Sudani, alisema yakuwa,mija ya watu wakwanza kutoa rambi rambi ni rais wa sasa wa Sudan Omar el Bashir. Picha hapo juu ni bendera ya Sudani, nchi ambayo rais Ahmed al Mighani, aliiongoza kwa muda wa miaka minne kabla ya kutolewa madarakani kwa nguvu za kijeshi.
Muammar Qaddafi ailaumu Amerika" Ziarani Belarus".
Minsk,Belarus-5/11/08.Kiongozi wa Libya ,Muammar el Qaddafi, ame ilaumu Amerika kwa kutumia uwezo wake visivyo wakati alipo kutana na viongozi wa Belarus.
Qaddafi, alisema ya kuwa, Libya zimakuwa zikipewa mzigo wa lawama zisizo na msingi, na hii yote inatokana na kutokuwa na usawa.
Alizidi kwa kusema yakuwa Amerika na washiriki wake wamekuwa wanakiuka haki za binadamu.
Kusisitiza hayo mwenyeji wake, rais wa Belarus,Aleksandr Kukashenko, alisema inatokana na baadhi ya sheria za Umoja wa matifa zinakiukwa na nchi wana chama hasa nchi zenye nguvu.
Mtoto wa Osama bin Laden, aomba hifazi za kikimbizi Uispania.
Madrid, Uispania - 7/11/08. Mwana wakiume wa kiongozi wa kundi kubwa linalo husishwa na ugaidi duniani Al Qaeda Osama bi Laden ameomba hifazi ya kikimbizi nchi Uispania.
Mwana huyo, anaye julikana kwa jina la Omar Osama bin Laden mwenye miaka 27, aliomba hifazi hiyo hivi karinbuni kwa mujibu wa serikali ya Uispania.
MWana huyo ambaye ameoa mwanamke wa kiingereeza, aliwekwa kwenye nyumba za kufikia wakimbizi zilizopo kwenye kiwanja cha ndege cha Barajan International Airport.
Hata hivyo kwa mujibu wa mmoja wa msemaji wa serikali, alisema ya kuwa mtoto huyu wa Osama bin Laden, amesha kataliwa ukimbizi ,a muda wowote ata rudishwa alikotokea.
Picha hapo juu ni ya mtoto wa Osama bin Laden, kwa jina Omar Osama bin Laden kulia akiwa na mkewe Jane Felix Browneau Zaina Muhammad Al Sabah, mapema walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari.

No comments: