Wednesday, October 14, 2009

China na Urussi kutiliana mkataba wa kibiashara.

Wanajeshi kuongezwa nchini Afghanistan"Waziri mkuu wa Uingereza atangaza".

London, Uingereza - 14/10/09. Waziri mkuu wa Uingereza,Gordon Brown,ametangaza yakuwa serikali ya Uingereza itapeleka wanajeshi wapatao 500, nchini Afghanistan.
Kutangazwa kwa idadi hiyo ya wanajeshi watakao kwenda nchini Afghanistan, kunakuja baada ya habari za kuaminika yakuwa Taliban na washiriki wake kuendelea kukua na kuongeza mapambano na majeshi ya NATO na washiriki wake, hali ambayo ikiachiwa hivi huenda ikawa mbaya zaidi hapo baadaye.
Hata hivyo uamuzi wa serikali ya Uingereza, kupeleka wanajeshi wake nchini Afghanistan,kunakuja wakati wananchi wa Uingereza wanakuwa na wasiwasi kuhusu hali halisi ya vita hivyo, ambavyo toka vimeanza vimekuwa vina toa matokeo tofauti kwa jamii nzima ya Waingereza.
Picha hapo juu, anaonekana, waziri mkuu wa Uingereza , Gordon Brown, akiwa anashikilia kichwa, kwani uamuzi wake unamweka katika njia ya panda.
Picha ya pili, anaonekana, waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, akiongea na wanajeshi, mapema alipo kwenda kuwatembelea, ili kuangalia hali halisi.
China na Urussi kutiliana mkataba wa kibiashara.
Beijing, China -14/10/09. Waziri mkuu wa Urussi, Vladamir Putin, na waziri mkuu wa China Wen Jiabao,wametiliana mkataba wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili zenye thamani ya 3.5billion.
Mikataba hiyo,kati ya Urussi na China, ulisainiwa mapema wiki hii, kabla ya kuanza kwa mkutano wa nchi za zenye mali ya asili zilizopo katika aneo la Asia.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa maendeleo ya jamii, wanasema kushirikiana kwa kwaribu, kati ya nchi hizi mbili, kunazipa muda mgumu sana nchi za Ulaya magharibi na Amerika, kwa kutaleta ushindani mkubwa wa kimazingira.
Picha hapo juu, wanaonekana, kushoto, waziri mkuu wa Urussi, Vladmir Putin, akipongezana na waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, kulia, mara baadaya kumaliza kutiliana mikataba ya kibishara na maendeleo ya nchi hizi mbili.
Umoja wa Ulaya, wataka kiongozi wa Guinea ashitakiwe.
Brussel, Ubeligiji - 14/10/09.Muungano wa Umoja wa Ulaya, umetoa wito yakuwa kiongozi wa kijeshi aliopo madarakani chini Guinea, Kaptain, Mussa Kamara, kufikishwa mbele ya sheria ili kukabiliana na mashitaka ya kukiuka haki za kibinadamu, wakati wa kuzuia maandamano,ambayo yaliandaliwa vyama vya upinzani.
Kwa mujibu wa mjumbe wa maendeleo ya umoja wa ulaya,Karel de Gucht, alisema yakuwa mkuu huyo wa jeshi,Kaptain, Mussa Kamara,anahusika na mauaji ya watu wasipungua 150, wakati walipo uwawa, tarehe 28, Semptemba,mwaka huu.
Hata hivyo , kiongozi huyo, wakijeshi alisema yakuwa hahusiki na mauaji ya watu hao.
Picha hapo juu, anaonekana, kiongozi wa Guinea, Kamptain,Mussa Kamara, ambaye ndiye kiongozi wa sasa wa Guinea.
Picha ya pili,wanaonekana wanajeshi wakiwa kazini kupambana na waandamaji katika jiji la Konakri.
Vifo vya watu ni namba isiyo julikana nchini Iraq.
Baghdad, Irak 14/10/09.Wizara inayo shughulikia haki za binadamu, imesema watu wapatao 85,000, wamepoteza maisha yao kati ya mwaka 2004- 2008, kutokana na vita vilivyo pelekea kung'olewa madarakani, aliyekuwa rais wa Irak, hayati , Saddam Hussein.
Kwa mujibu wa habari hizo , ni kwamba idadi ya namba hiyo ya watu waliopoteza maisha, imepatikana, kutokana na kuwepo kwa vyeti vya kuzaliwa na kutolewa vyeti vya vifo.
Akiongezea , wizara hiyo ilisema zaidi ya watu wapatao, 147,195, wamajeruhiwa.
Hata hivyo, wizara iliongezea yakuwa kunaidadi ya vifo vingi na majeruhi ambao hazijulikani, na huenda idadi ikawa kubwa zaidi.
Picha hapo, anaonekana mmoja wa mwanajeshi akimsaidia mwenzake ambaye ameumua vibaya,mara ya baada ya kushambuliwa vibaya katika mapambano.
Picha ya pili, wanaonekana wakina mama wawili, wakiwa wanauguza watoto wao, ambao wameumia kutokana na mapigano yaliyopo nchini Irak.
Picha ya pili, wanaonekana, baadhi ya watu wakiwa wanaelekea msibani, baada ya mmoja wa familia alipo poteza maisha baada ya kushambuliwa na bomu.

No comments: