Saturday, October 3, 2009

Rio de Jainero, wenyeji wa michezo ya Olyimpik 2016"Kwa mara ya kwanza katika udongo wa Amerika ya Kusini.

Rio de Janeiro, wenyeji wa michezo ya Olyimpik 2016."Kwa mara ya kwanza katika udongo wa Amerika ya Kusini".

Copenhagen, Denmark - 03/10/09.Jiji la Rio de Janeiro, limekabidhiwa rasmi kuwa mwenyeji na mwandaaji wa mashindano ya michezo ya Olyimpiki ya mwaka 2016.
Jiji la Rio de Jainero, litakuwa la kwanza katika historia ya michezo ya Olyimpik, kufanyika katika bara la Amerika ya Kusini.
Jiji la Rio de Janeiro, liliibuka kuwa la kwa mbele ya majiji ya Chikago Amerika, Madrid, Uispania na Tokyo Japan.
Akitangaza mbele ya wajumbe walioudhulia,rais wa IOC International Olyimpic Committee,Jacques Rogger,alisema waaandazi wa michezo ya Olyimpik mwaka 2016, ni Rio de Jainero,ni nderemo na shwange zilitawala kwa wajumbe wa Brazili na nchi Brazili, huku rais wa Brazil, Lula da Silva, akiwa anatokwa na machozi ya furaha, kwani alikuwa akiongoza kampeni ya jiji la Rio de Jainero kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya Olyimpik mwaka 2016.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Brazili, Lula da Silva, akiwa amekumbatia bendera ya Brazili kwa furaha sana mara baada ya Brazil kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olyimpiki ya mwaka 2016.
Picha ya pili wanaonekana, wakazi wa jiji la Rio de Jainero, wakishangilia kwa furaha,baada ya matokeo kutangazwa ya kuwa jiji lao, ndilo mwenyeji wa michezo ya Olyimpiki ya mwaka 2016.
Iran na jumuia ya kimataifa wafikia muafaka kwa muda.
Geneva,Uswisi - Serikali ya Iran, imekubali kuruhusu shirika linalo shughulikia ukaguzi wa nyuklia duniani, IAEA, kwenda nchini Iran kuchunguza, kiwanda cha pili kilichopo miji wa Qom.
Makubaliano hayo yamekuja baada ya mazungumzo marefu yaliyo fanyika nchini, Uswisi Geneva, kati ya wajumbe wa serikali za Amerika,Uingereza,China, Urussi,Ujerumani na Iran.
Akiongea mbele ya waandishi wa habari, waziri wa mambo ya nchi za nje wa muungano wa Ulaya ,Javier Solana, alisema huu ni mwanzo wa kutatua mgogoro huu.
Hata hivyo kwa upande wa Iran, mjumbe wake Saeed Jalili, alisema, Iran haitakubali kusimamishwa kwa mpango wake wa kuendelea na mitambo ya nyuklia kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mitambo haitakuwa yakutengeneza siraha za nyuklia.
Picha hapo juu, anaonekana,mjumbe wa Iran Saeed Jalili, akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya mazungumzo yaliyo fanyika jijini Ganeva.
Picha ya pilini ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa muungano wa Ulaya ,Javier Solana, akiongea na vyombo vya habari baada ya mkutano na serikali ya Iran, kuhusu swala nyuklia.
Viongozi wa Izrael na Palestina, wakubalianopo kuna unafuu kwa jamii zao.
Jerusalem, Izrael - 03/10/09.Serikali ya Izrael imewaachia huru wanawake 19, ambao ilikuwa imeshikilia kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa habari toka kwa wachunguzi wa hali ya kisiasa na usalama wa Izrael na Palestina,wamesema yakuwa kuachiwa kwa wanawake hao, kumekuja baada ya makubaliano ya kuwa video ya askari wa Izrael, Girad Shilit itaonyeshwa kwenye mitandao , runinga na kutangazwa kwenye vyombo vya habari, ili kuonyesha ya kuwa askari huyo ni mzima wa afya.
Kwa kuthibitisha makubaliano hayo, kundi linalo mshikilia, Girad Shilit, lilitoa video ya askali huyo na kuikabidhi kwa wajumbe wa nao husika na kupelekwa kwa wazazi wa, Gerad Shilit, na ndipo picha za video kusambazwa kwenye vyombo vya habari.
Picha hapo juu, ni picha ya Girad Shilit,akisoma gazeti,wakati alipo kuwa akipigwa picha tayari kutumwa kwa familia yake kuonyesha yakuwa yupo mzima wa afya.
Picha ya pili,anaonekana mmoja ya wanawake,ambao walikuwa wameshikiliwa na serikali ya Izrael, akiwa amebeba mtoto huku akimpangusa machozi, mara baada ya kukutana wa ndugu na jamaa.
Ufaransa yapata faida kubwa kwa mauzo ya siraha duniani
Paris, Ufaransa - 03/10/09. Serikali ya Ufaransa imeongeza maouzo yake ya silaha kwa kufikia asilimia 13% tangu mwaka 2000..
Mauzo hayo yametokana kufanya biashara na nchi kama, Brazil,Saud Arabia na Morokko.
Kuongezeka huko kwa mauzo ya silaha kwa asilimia 13%,yamekuja baada ya rais wa Ufaransa, Nikolas Sarkozy, kuipa kipaombele ukuzaji wa viwanda vinavyo tengeneza zana za kijeshi na ulinzi nchini Ufaransa na kuweza kuajili zaidi ya wafanyakazi 50,000.
Kwa mujibu wa machunguzi wa maswala ya kijeshi wanasema , makampuni ya Ufaransa yameweza kupata thamani ya Amerikani dolla $9.7billion, na kuwa juu kwa asilimia 7% katika soko la dunia.
Picha hapo juu, wanaonekana , baadhi ya wataalamu wa nchi za Kiarabu wakiangalia kwa na kuonyeshana ni jinsi gani ndege zilizo mbele yao zinaweza kufanya kazi.

No comments: