Monday, October 19, 2009

Mwaka 2009 hakuna kiongozi bora wa Afrika.

Mwaka 2009 hakuna kiongozi bora wa Afrika. London,Uingereza - 19/10/09.Shirika linalo simamiwa na mfanyabiashara mwafrika, Ibrahim Mo, limetangaza mwaka 2009 halitatoa zawadi kwa kiongozi yoyote wa Afrika. Akiongea leo jijini London, Ibrahim Mo, alisema kamati inayo simamia uchaguzi wa viongozi bora wa Afrika, imekosa kiongozi wa Kiafrika ambaye amekamilisha matakwa ya kiongozi kupewa zawadi na shirika hilo. Zawadi hiyo hutolewa kwa viongozi wa Afrika ni kiasi cha dola za Kiamerika Milllion tano na dola laki lakimbili killa mwaka hutolewa kimaisha mpaka hapo mteuliwa watakapo aga dunia. Picha hapo juu anaonekana, Ibrahim Mo, akiongea leo mbele ya wajumbe wa kamati waliokuja kushuhudia ni nani amechaguliwa kuwa kiongozi bora wa Afrika wa mwaka 2009, alitangaza yakuwa mwaka 2009 hakupatikana kiongozi aliye fikisha matakwa ya kuwa kiongozi bora wa Afrika. Mauji nchini Iran yaleta kushutumiana na nchi majirani.

Tehran, Iran - 19/10/09.Rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad, ameilamu Pakinstan kwa kuhusika na mauaji ya kujitolea muhanga ambayo yamesababisha vifo ya wakuu wa kijeshi wanchi hiyo pamoja na baadhi ya wananchi.
Hata hivyo serikali ya Pakistan, imekanusha madai hayo.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Iran, ambaye ameilaumu Pakistan kwa kuhusika na mauaji nchini Iran.
Hamid Karzai na wagombea wenzake kukwaana tena katika kiti cha urais.
Kabul,Afghanistan - 19/10/09. Kamati inayosimamia uchaguzi nchini Afghanistan ambayo ipo chini ya Umoja wa Mataifa, imetangaza yakuwa uchaguzi uliofanyika nchini humo ulikuwa na ukiukwaji washeria.
Kufuatia ukiukwaji wa sheria za uchaguzi, upo uwezekano mkubwa wa wananchi wa Afghanistan
kurudia kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa katiba ya Afghanistan, mgombea kiti cha urais lazima apatekura nyingi zaidi ya asilimia 50%.
Picha hapo juu, anaonekana Amid Karzai, akihutubia mbele ya mkutano wa umoja wa mataifa wakati akiwa rais wa Afghanistan mwaka jana.

No comments: