Friday, October 23, 2009

Uchumi wa China wapata nafuu.

Uchumi wa China wapata nafuu. Beijing, China 23/10/09. Serikali ya China imetangaza ya kuwa hali ya uchumi wa nchi hiyo umepanda kwa kiasi cha asilimia 8%, kwa muda mfupi tangu dunia kukumbwa na tetemeko la kiuchumi. Kwa mujibu wa serilikali, kupanda kwa hali ya kiuchumi, kumekuja baada ya matumizi ya nje na ndani kuelekea kufanya vizuri kibiashara. Picha hapo juu ni ya bendera ya China, nchi ambayouchumi wake na maendeleo yake ya kiuchumi duniani yamekuwa yakienda vizuri. Wanchi wa Kenya waishitaki Uingereza kwa makosa ya miaaka ya 1950-60s.

London, Uingereza - 23/10/09. Raia wa Kenya watano wameishitaki serikali ya Uingereza kwa kosa la kuwatesa na kuwanyanayasa wakati wa miaka 1950 - 60, wakati wa harakati za kugombea uhuru wa Kenya.
Kufuatia ushahidi uliopo, unaonyesha yakuwa serikali ya Uingereza iliwafunga maelfu ya watu katika kambi na kuwatesa.
Hata hivyo,ofisi ya mambo ya ndani ya Uingereza, haikutaka kuoelezea lolote kutokana na habari hizi.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Kenya, nchi ambayo wananchi wake waliteswa vibaya wakati walipo kuwa wakigombea uhuru.
Picha ya pili ni ya bendera ya Uingereza,nchi ambayo ilikuwa ikitawala Kenya, kabla ya vita vya Mau Mau kuanza.

No comments: