Swala la nyuklia lawa kitendawili.

Kutokana na habari zilizo patikana kutoka ndani ya Ikulu ya Amerika, zinasema , rais, Obama ,alikubaliana na waziri mkuu wa Izrael, Binyamin Netanyahu,wakati walipo kutana hivi karibuni, rais Obama, alihaidi kuendeleza ule mswada wa uanaosema "Usiulize na usiseme au kuongea"
Hata hivyo wasemaji wa serikali zote mbili walikataa kuelezea kuhusu swala hilo.
Picha hpo juu, wanaonekana, rais wa Amerika, Baraka Obama, akiwa ameinama huku akimsikiliza, waziri mkuu wa Izrael, Binyamin Netanyahu, wakati walipo kutana hivi karibuni jiji Washington.
Picha ya pili ni ya moja ya kombora la Izrael, lenye uwezo wa kubeba siraha ya kinyuklia likijaribiwa kwenda angani.
Lazima tujifunze kuishi na hali hii, "Asema waziri wa mambo ya nje wa Izrael".

Katika kikao hicho,waziri wa mambo ya nje wa Izrael, Lieberman, alisema swala la amani kati ya Wapalestina na Waizrael kwa sasa haliwezekani na lazima jamii ijifunze kushi na hali hii.
Akitoa mfano wa wa kiwiwa cha, Syprus,Nagorno - Karabakh na Visiwa vya Falkland, dunia imekubali kuhishi na hali hii, hivyo basi wakati umefika kukubali kuishi kwa kuzoea hali hii.
Picha hapo juu, wanaonekana,waziri wa mambo ya nchi za nje wa Izrael,Vigdor Lieberman akimkaribisha mjumbe wa serikali ya Amerika George Mitchell anaye shugulikia swala la kuteta amani kati ya Wapalestina na Waizrael.
Mwanasayansi wa Iran apotea kimiujiza.

Tehran, Iran - 08/10/09.Kuna habari za kutatanisha yakuwa aliyekuwa mchunguzi na mwana sayansi maswala ya nyuklia ya Iran, Shahram Amir, amekimbia kutoka Iran na aliko elekea hakujulikani.
Hata hivyo kwa mujibu wa serikali ya Iran, inadai yakuwa kupotea kwa mwanasayansi huyo miezi mitatu iliyo pita akitokea kuhij Makka, kulifanywa na serikali ya Saudi Arabia na Amerika.
Hata hivyo serikali ya Amerika imekanusha habari hizo, na kusema haina habari za Shahram Amir mahari alipo.
Picha hapo juu,ni ya bendera ya Iran, nchi ambayo imekuwa na msimamo mkali hasa katika swala la haki yake ya kuwa na utaalamu wa kinyuklia.
Taliban, bado tishio, ijapokuwa kuna ulinzi mkali.

Kwa mujibu wa mashahidi walioshuhudia tukio hilo, walisema mlipuko huo ulitokea muda wa mbili na nusu hasubuhi kwa muda wa aneo hilo.
Kufuatia mlipuko huo watu wapatao 17 wamepoteza maisha yao na zaidi ya watu 63 kujeruhiwa vibaya.
Kufuatia mlipuko huo, kundi la Taliban, limedai yakuwa ndilo lililohusika na mlipuko huo.
Picha hapo juu, wanaonekana askari wa Aghanistan, wakiangalia kwa makini, ni jinsi gani bomu lilivyo haribu majengo ya ubalozi huo.
No comments:
Post a Comment