Sunday, October 25, 2009

Kansellar Angel Markel ateua serikali mpya.

Wapalestina na Waizrael bado kukubaliana kimsingi haki zao Jerusalem Mashariki, Izrael - 25/10/09. Polisi wa Izrael wamevamia msikiti wa Al Aqsa na kupambana na waumini wa Kiislaam wengi wao wa kiwa Wapalestina. Kufuatia kuvamia eneo la msikiti huo wa Al Aqsa, waumini wa dini ya Kiislaam wengi ambao ni Wapelestina walianza kutupa mawe na huku polisi wa Izrael wakitumia mabomu ya kutoa machozi. Kwa mujibu wa shirika la kuktetea haki za binanadamu, limesema ya kuwa kuna baadhi ya watu walikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi. Picha hapo juu anaonekana mmoja wa kijana wa kipalestina akirusha jiwe kuelekea walipo polisi na huku wapiga picha wakiwa kazini kupata picha kamili ya matukio. Jeshi la serikali la kamata miji iliyokuwa chani ya Taliban. Islamabad, Pakistan -25/10/09.Serikali ya Pakistan, imetangaza yakuwa imekamata mji wa Kusini mwa Waziristan ambao umezungukwa na milima. Kwa mujibu wa masemaji wa jeshi, alisema yakuwa waliweza kupambana na kundi la Taliban na mshiriki wake Al-qaed kwa muda wa wiki moja na kufanikiwa kukaribia mji amabo kiongozi wa Taliban, Hakimullah Mehsud. Kufuatia mapambano hayom, maelfu ya watu wamekimbia maeneo yao kwa ili kuokoa maisha yao. Picha hapo juu wanaonekana wanachi wakiwa wanakimbia kuepuka kipigo kutoka kwa mmoja wa wanajeshi ambaye ana jaribu kuwatuliza wakimbizi waliokimbia vita vinavyo endelea nchini Pakistan kupambana na ugaidi nchini humo. Kansellar Angel Markel ateua serikali mpya. Berlin, Ujeruman - 25/10/09. Kansellar Angel Markel, ametangaza serikali mpya itakaoyo iongoza Ujerumani hasa katika kipindi hiki cha kupapamba na kuinua uchumi wa nchini hiyo. Serikali mpya chini ya uongozi wa Bi, Angel Markel imeteua Wolfgang Schauble kuwa waziri wa fedha amabye atakuwa na kibarua kigumu cha kujaribu kuangali maswala ya pesa na kupunguza kodi za mapato kuanzia mwezi januari mwakani. Picha hapo juu, anaonekana Bi, Angel Markel akiongea mbele ya wanachama wa chama chake mapema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mapema mwaka huu. Baghdad yashutushwa na hali ya milipuko ya mabomu. Baghdad,Irak - 25/10/09. Mabomu yamelipuka karibu na ofisi za serikali ya Irak na kupoteza maisha ya watu 108 na kujeruhi watu wasiopungua 512. Kwa mujibu wa habari , huenda idadi ya watu watakao poteza maisha ikaongezeka kutokana na milipuko hiyo ya mabomu. Serikali ya Irak, imelaaani kitendo hicho na kudai yakuwa ni kitendo cha kulaani wa na jumuia ya kimataifa na lazima kupigana na hali hii kwa hali na mali. Picha hapo juu, unaonekana moshi ukielekea juu, baada ya bomu kulipuka karibu na ofisi za serikali.

No comments: