Monday, December 14, 2009

Evo Morales aongoza kwa kura nchini Bolivia.

Evo Morales, aongoza kwa kura nchini Bolivia.. La Paz, Bolivia - 14/12/09. Matokeo ya uchaguzi uliofanyika nchini Bolivia, yanaonyesha rais wa sasa wa nchi hiyo Evo Morales, ameshinda kwa asilimia 60%. Kwa mujibu wa ripoti za kamati inayo simamia uchaguzi, mpinzani wa Evo, Manfred Reyes Villa, inasemekana amepata kura kwa asilimia 23%. Hata hivyo matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa wiki hii rasmi. Picha hapo juu anaonekana, rais wa Bolivia, Evo Morales,akihutubia kwa makini wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Bolivia. Rais wa Kuba Raul Castro, ailaumu Amerika. Havana, KUba 14/12/09. Rais wa Kuba ,Raul Castro, ameilaumu serikali ya Amerika kwa kuunga mkono uchaguzi wa Honduras, ambao hakuwa wa haki na inastahili rais wa zamani Manuel Zelaya arudishwe madarakani. Rais, Raul Castro, aliyasema haya wakati wa mkutano unao zikutanisha nchi za Latini Amerika Hata hivyo msemaji wa serikali ya Amerika, alisema " Raul Castro inabidi aanze demokrasi nchini mwake, kwani wakati wakuchaguliwa kwakwe kura zilikuwa za mtu mmoja." Picha hapo juu anaonekana rais wa Kuba,Raul Castro akiongea wakati wa mkutano wa viongozi wa Latini Amerika uliofanyika jijini Havana nchini Kuba kujadili maendeleo ya nchi zao kiuchumi na kijamii na kutafuta njia ya kukuza uchumi. Waandamanaji wakumbana na nguvu za dola. Copenhagen,Denmark - 14/012/09.Watu zaid ya 200, wamekamtwa na polisi wakati wa maandamano ya kupinga kuongezeka kwa machafuzi ya hali ya hwe na mazingira. Waaanamanaji hao, wanaanandamana kuwataka viongozi wa dunia ambao wapo kwenye mkutano nchini Denmark kujadili kila njia ya kupunguza machafuzi na kuharibu hali ya hewa duniani. Kufuatia maandamano hayo, polisi wamekuwa wanasimamisha watu na kuwakagua kama wana zana za hatari. Picha hapo juu anaonekana mmoja ya waaandamaji akikabiriana na polisi wanao linda mkutanao huo unaoendelea. Waziri mkuu wa Itali ashambuliwa. Roma. Itali - 14/12/09.Waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi,amejeruhiwa kwenye paji la uso baada ya mtu mmoja kumrushia kigae usoni. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, alisema "Mtu mmoja 42 ambaye anamatatizo ya akili ndiye aliyemrushia kigae hicho", mtu huyo alikamatwa na polisi mara moja. Waziri mkuu, Berlusconi, alijeruhiwa pua na baadhi ya meno kukuvunjika. Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Itali, Silvio Berlusconi, akiwa njiani kuelekea hospitali, baaada ya kushambuliwa na kigae.

No comments: