Saturday, December 19, 2009

Uchumi wa China kuonyesha mabadiliko.

Uchumi wa China kuonyesha mabadiliko. Beijing,China - 19/12/09. Serikali ya China, imetangaza ya kuwa uchumi wa umekuwa kwa kiasi cha asilimia 0.6 hadi kufikia mwisho wa mwezi wa Novembea. Kwa mujibu wa habari zilizo tolewa na serikali ya China, zinasema kukua huku kwa uchumi kwa kipindi cha miezi kumi iliyo pita , kuanatokana na kuongezeka na ununuzi na uzalishaji na kuwekwezwa kwa vitega uchumi kuliko ongezeka. Picha hapo juu ni bendera ya China nchi ambayo uchumi wake umeanza kuku kwa kulinganisha na nchi zinanzo endelea dunia.

Taliban yawa na mbinu mpya za mashambulizi.
Kabul Afghanistan - 19/12/09. Kiongozi mmoja wa kundi la Taliban,amesema ya kuwa kundi la Taliban litabigana na jeshi la Amerika na NATO hadi mtu wa mwisho, hata kama wakileta zaidi ya wanajeshi 200,000.
Kwa mujibu wa maelezo ya wataalamu wa mambo ya kivita wamesema ya kuwa Taliban, wamebadilisha mbinu ya kupigana hasa kwa kipindi cha baridi, wameongeza mashambulizi tofauti na miaka ya nyuma.
Picha hapo juu wanaonekana wapiganaji wa Taliban, wakiwa mafichoni tayari kwa kuanza mashambulizi.
Jibu la kutunza na kulinda mazingira bado kitendawili kwa jumuia za kimataifa.

Copenhagen,Denmark-19/12/09.Umoja wa mataifa umekubaliana kimsingi uamuzi uliochukuliwa nchini Denmark na viongozi na marais walioudhulia mkutano wa kujadili jinsi ya kukabiliana kuaribika kwa maziangira na hali ya hewa.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon, alisema" Nchi zote zimekubaliana kimsingi kukubaliana ni kwa jinsi gani zitashiriki kupunguza uharibufu wa masingira na hali ya hewa, muda muafaka utakapo fika miswaada iliyo kubalika itakuwa sheria."

Hata hivyo Amerika, Brazil, China na Afrika ya Kusini, zimekubaliana kwa kiwango kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa kutokana na nchi hizo kuwa na viwanda vingi.

Picha hapo juu, wanaonekana baadhi ya wanachama wa chama cha Kijana na wananchi wengine wakiwa wanapinga na kusema ni aibu kwa uamuzi uliofanywa wa kutokuwa kubaliana kwa pamoja kupambana na uharibifu wa mazingira.

Picha ya pili wanaonekana waandamaji wakiwa wamebeba maelezo yenye ujumbe kwa wajumbe walioudhulia mkutano wa kukabiliana na uharibifu wa mazingiza jijini Copenhagen Denmark.

No comments: