Friday, December 25, 2009

Ulinzi wa Papa waingia dosali.

Ulinzi wa Papa waingia dosali Vatican city, Vatican - 25/12/09. Waumini wa madhehebu ya Kikatoriki waliokuja kuhudhuria misa ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu katika kanisa kuu la Vatikani,walishikwa na mshituko baada ya mmoja ya waumini wa kike kuruka kizuizi na kumkaba Papa Benedikt wa XVI na kuanguka nae chini. Mwanamke huyo jina limehifadhiwa, anaulaia wa Itali na Swis,alikamatwa na walinzi wa Papa na baadaye kuwekwa chini ya ulinzi kwa mahojiano. Hata hivyo, Papa , 83 aliweza kuendelea na misa ya usiku wa Krismas, baada ya kuthibitisha hakupat madhara ya aina yoyote. Picha hapo juu anaonekana Papa Benedikt wa XVI akiwasalimia na kuwabaliki waumini waliokuja kuudhulia misa ya Krismas. Waathirika wa nguvu za kinyuklia kulipwa fidia. Paris, Ufaransa - 25/12/09. Serikali ya Ufaransa imekubali kulipa fidia kwa wanachi wa Algeria walio athirika kutokana na mazara ya kujaribiwa nguvu za kinyuklia mnamo kati ya miaka ya 1960-67. Kukubali kwa serikali kumekuja baada ya bunge la Ufaransa kupitisha mswada huo wa malipo kwa waathirika wa nguvu hizo za nyuklia. Hata hivto malipo yatalipwa kutokana na kesi ya kila mwathirika atakapo wakilisha kesi yake. Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Herve Morin alisema " Kupitishwa kwa seria hiyo kumeleta usawa." Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wafanyakazi wa moja ya mitambo inayoongoza nguvu za kinyuklia wakiwa wanaangalia kwa makini mitambo hiyo.

Mwanjeshi aliye kamatwa na Taliban bado yuhai.

Kabul, Afghanistan - 25/12/09. Viongozi wa jeshi la NATO lililopo Afghanistan limethibitisha ya kuwa picha ya video ya mmoja ya mwanajeshi wa Kiamerika aliyekamtwa miezi mitano iliyo pita na kundi la Taliban.

Mwanajeshi huyo, Bowe Bergdahl alitekwa nyara mara baada ya kuwasili Afghanistan katika moja kambi moja ya kijeshi iliyopo Paktika.

Video hiyo ilionyeshwa kwa dakika 36, huku mwanajeshi huyo, akiongea ya kuwa kuwepo kwa majeshi ya NATO nchini Afghanistan ni kimyume cha wananchi wa Afghanistan.

Katika video hiyo, kiongozi mmoja wa Taliban,Zabihullah Mujahid, alisema "Itabidi kuwepo na kubadilishana wafungwa ikiwa NATO inataka Bowe Bergdahl aachiwe na kundi hilo."

Picha hapo juu ni ya Bowe Bergdahl, akiongea katika picha ya video iliyo tolewa na kundi la Taliban hivi karibubi.

No comments: