Thursday, December 24, 2009

Wakristu duniani wakumbuka kuzaliwa kwa Mkombozi.

Wakristu duniani wakumbuka kuzaliwa kwa Mkombozi. Usiku wa Krismas- 24/12/09. Mamilion ya waumini wa dini ya Kikristu duniani leo usiku wanasherekea siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu,akiongea kwa furaha, mmoja wa waumini wa dini ya kikristu alisema "Sisi wakristu tunaamini ya kuwa alikuja kuikomboa dunia na kupitia yeye kila mtu atakombolewa akimfuata Yesu Kristu. icha hapo juu, wanaonekana waumini wa dini ya Kikristu, wakiwa kanisani kuhudhulia misa ikiwa ni siku muhimu ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristu.

Iretrea yawekewa vikwazo na UN.
New York, Amerika - 24/12/09.Kamati ya usalama ya umoja wa Matifa, imeiwekea vikwazo serikali ya Iritrea kwa kushirikiana na kuwasaidia magaidi wa Kisomalia wa Al Shabaab na kukataa kutoa jeshi lake karibu na mpaka na Djibuti. Azimio hilo lilipitishwa kwa pamoja kwa kura 13,lakini China na Libya hazikupiga kura. Hata hivyo serikali ya Iritrea, imekuwa ikikanusha ya kuwa inashirikiana na kundi la Al Shabaab ambalo lina pigana na jeshi la serikali ya Somalia. Picha hapo juu anaonekana mmoja wa mwanajeshi wa Iritrea,akiwa kazini kulinda mpaka kati yake Iretrea na Djibuti. Mwana sayansi akubali kutolewa kwa viungo vya mwili.
Tel-Aviv, Izrael- 24/12/09.Mwanasayansi na mchiunguzi wa miili ya binadamu, Jehud Hiss amekubali yakuwa Izrael ilikuwa ikitoa baadhi ya viungo vya binadamu bila ruhusa ya watu walio aga dunia au ruhusa za ndugu zao.
Jehud Hiss, ambaye alikuwa akifanya kazi katika moja ya maabara ambazo zilikuwa zikitumika katika kupima na kuangalia nini nyanzo vya vifo vya watu hao.
Jehus Hiss alisema "viungo kama mioyo ngozi na baadhi ya mifupa ilikuwa ikitolewa kwa ajili ya matumizi binafsi na viungo hivyo vilikuwa vikitolewa katika miili ya wafanyakazi wageni na Wapalestina."
Kukubali kwa habari hizo kunakuja baada ya moja ya gazeti la nchini Sweden, kutoa habari yakuwa Izrael ilikuwa ikitoa baadhi ya viungo vya miili kwa watu walioag dunia bila makubaliano ya watu hao au ndugu zao, habari ambayo Izrael ilikanusha.
Picha hapo juu ni moyo kiungo muhimu katika mwili wa binadamu.
Urussi kuimarisha nguvu zake za kinyuklia.
Moscow, Urussi - 24/12/09. Rais wa Urussi, Dmitry Medveded, amesema Urussi itaendeleza nguvu zake za kinyuklia kufuatina na wakati.
Akiongea na waandishi wa habari, rais Medvedev alisema" Ili kulinda nchi yetu ni lazima kuendeleza na kufanyia marekebisho siraha zetu za kinyuklia na Amerika wanaelewa swala hilo."
Rais Medvedev, aliongezea kwa kusema ya kuwa kukua kwa uchumi wa Urussi, umeanza na utachukua muda kufikia hali nzuri.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja ya raia wa Urussi, akiangali runinga,wakati rais wa Russia , Dmitry Medvedev akiongea na waandishi wa habari.
Volkano yatishia maisha ya wakazi.
Mlima Mayon, Philipinsi- 24/12/09 . Hali ya hatari imetangazwa kwa wakazi wanao kaa karibu mlima Mayon kufuatia mlipuko wa volkano uliotokea katika mlima huo.
Akionga kwa msisitizo, mkurugenzi wa maswala ya sayansi ya volkano, Renato Solidu malisema"Mlipuko huo ulionza mwamzoni mwa wiki iliyo pita na hadi kufikia sasa unaelekea kuleta madhara makubwa kwa jamii na mzingira ya karibu na mlima huo." Majivu ya moto yaliotokana na mlipuko huo, yalionekana kuruka kuelekea hewani kiasi cha umbali wa zaidi ya mita miatano.
Picha hapo juu, majivu ya moto yanaonekana yakiruka juu, hali ambayo wakazi karibu na maeneo hayo wamekuwa na wasiwasi mkubwa.
Urussi yafungua mpaka na Georgia.
Moscow,Urussi- 24/12/09 . Serikali ya Georgia na Urussi, zimekubaliana kufungua mpaka nchi zao, tangu kusimama kwa vita vilivtotokea mwaka mmoja uliopita.
Kwa mujinu wa wasemaji wa serikali zote mbili, ufunguzi wa mipaka hiyo utawasaidia wanachi wa Georgia kusafirisha mizigo yao.
Urussi, ilifunga mpaka na Georgia tangu mwaka 2006,kutokana na mvutano wa kisiasa uliotokea kati ya nchi hizo.
Picha hapo juu, kinaonekana moja ya kifaru cha kijeshi kikiwa katika ulinzi wa mpaka kati ya Urussi na Georgia.

No comments: