Sunday, December 27, 2009

Ulinzi waongezwa kwenye viwanja vya ndege.

Maelfu wakumbuka waliopoteaza maisha wakati wa Tsunami. Aceh, Sri Lanka - 27/12/09. Maelfu ywa watu diniani wamekusanyika kwenye nchi ambazo zilipata maafa makubwa kutokana na Tsunami yaliyo tokea mnamo mwaka 2004. Maafa hayo ta Tsunami yalipoteza maisha ya watu wapato 226,000 na watu wengine kuachwa bila makazi na kuleta uaribifu mkubwa katika jamii. Kwa mujibu wa shirika linalo shughulikia utoaji wa misaada la umoja wa Matifa Red Cross, limesema maafa ya Tsunami bado yapo katika maeneo yote na hasa kwa familia zilizo athirika na na janga hili. Picha hapo juu ni picha ya boti, ambayo ilibakizwa baada ya janga la Tsunami,na anaonekana mama mmoja akiangalia kwa uchungu janga lililoletwa na Tsunami katika eneo lao.

Gaza waadhimisha mwaka mmoja tangu kuisha vita.
Gaza, Palestina-27/12/09. Wapalestina wakazi wa Gaza wameandamana kukumbuka siku ya kuanza kwa mashambulizi yaliyo fanywa na jeshi la Izrael kwa muda wa siku 22.
Mashambulizi hayo ambayo yalisababisha vifo vya watu 1600 na uaribifu mkubwa wa makazi ya Wapalestina.
Vita hivyo ambavyo vilileta maafa katika eneo la Gaza, vilikuwa kati ya Hamas na jeshi la Izrael.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya waandamanaji wakiwa wakiaandamana kuadhimisha siku ya kuanza kwa vita vya Gaza.
Ulinzi waongezwa kwenye viwanja vya ndege.
Michigan, Amerika- 27/12/09. Raia wa Nigeria ameshitakiwa kwa kosa la kutaka kulipua ndege ya abiria iliyo kuwa ikitokea Schiphol Asterdam.
Hakimu alimsomea kesi mshitakiwa akiwa hospital katika hospitali ya Ann Arbor iliyopo Michigan.
Mshitakiwa huyo kwa jina Umar Abdulmutallab 23, alianzia safari yake nchini Nigeria siku moja kabla ya siku ya tukio.
"Kufuatia tukio hilo , ulinzi umeongezwa katika viwanja vya ndege vyote nchin Amerika" alisema msemaji wa mwaswala ya ualama wa anga wa taifa nchin Amerika.
Picha hapo juu wanaonekana maafisa wa usalama wa moja ya kiwanja cha ndege wakiangali kwa makini wasafiri wanavyo jiandaa kukaguliwa.
Siku ya Ashura yaingia dosari nchini Iran.
Tehran, Iran - 27/12/09. Wapinzani wa serikali nchini Iran, wamepambana na polisi wa serikali wakati wa kusherekea kumbulumbu ya siku ya Ashura na watu kupoteza maisha na wengi kujeruhiwa.
Siku hii ilikuwa ni kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha mjuukuu wa Mtume Muhammad, Ashura, kilichotokea karne ya 7th
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Iran, watu wanne walipoteza maisha katika maandamano hayo.
Msaidizi wa jeshi la polisi la Iran,Ahmad Reza Radan, alisema " watu wapatao 300,walikamatwa kwa kusababisha vurugu wakati wa sherhe ya kumbukumbu ya Ashura.
Hata hivyo, viongozi wa vyam vya upinzani walisema kun zaid ya watu wanne waliopoteza maisha yao.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja ya mwanadamaji akisaidiwa na wenzake mara maada ya kujeruhiwa vibaya na moto.

No comments: