Thursday, December 3, 2009

NATO kuongeza wapiganaji Afgahinstan.

NATO kuongeza wanajeshi Afghanistan.

Washington, Amerika - 03/12/09. Rais wa Amerika Baraka Obama, ametanganza ya kuwa wanajeshi wapatao 30,000 watakwanda nchini Afghanistan.
Akiongea mbele ya wanajeshi waliomaliza mafunzo ya kijeshi, rais Obama alisema "Vita hivi ni kwajili ya usalama na ulinzi wa Amerika na nchi wanachama wa NATO".
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana zinamsema kabla ya kutangaza hatua hiyo, rais Obama, aliwasiliana na viongozi wa bara la Ulaya wanachama wa NATO,ili kuzihimiza nchi hizo kushirikiana kikamilifu kushinda vita dhidi ya Taliban na kundi la Alqaeda.
Picha hapo juu anaonekana rai wa Amerika, Baraka Obama, akihutubia mbele ya viongozi wa serikali na wanajeshi,kuhusu kuongeza idadi ya wanajeshi watakaokwnda nchini Afghanistan.
Picha ya pili, wanaonekana wanajeshi wakiwa katika doria nchini Afghanistan, katika harakati za kupambana na Taliban na Alqaeda.
Rwanda mwamachama mpya wa Commonwealth.
Kigali, Rwanda - 03/12/09 . Jumuiya ya nchi wanachama wa ambazo zilitawaliwa na Mwingereza - Commonwealth group- zimeikaribisha rasmi nchi ya Rwanda kuwa manachama wa 54. Kwa mujibu wa waziri wa habari wa Rwanda, Louise Mushikiwabo, aliseama nchi yake imepiga hatua kubwa kimaendeleo tangu kutokea vita vya kikabila vya mwaka 1994.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye tangu kuwa kiongozi wa Rwanda, nchi yake imeendelea kiuchumi na kijamii kwa kiasi kikubwa.
Picha ya pili, ni ya rais wa Ufaransa, Nikolas Sarkozy, ambye nchi yake imekuwa mtawala wa Rwanda wakati wa kipindi cha ukoloni, na sasa Rwanda imejiunga na jumuia ya nchi zinazo sema kiingereza.

No comments: