Tuesday, June 1, 2010

Uturuki ya laani vikali kitendo cha Izrael.

Umefikia afrika kuwa na kiti ndani ya UN. Nice,Ufaransa- 01/06/2010. Rais wa Ufaransa Nicalas Sarkozy amesema "umefika wakati wa bara la Afrika kuwa na kiti maalumu katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa." Rais, Sarkozy aliyasema hayo wakati alipo kutana na viongozi wa bara la Afrika kwa kusisitiza ya kuwa "hatuwezi kuongea habari za ulimwengu na dunia bila kuhusisha bara la Afriaka"

Mkutano huo ambao uliitishwa na Ufaransa, na kwa mara ya kwanza ulizishirikisha nchi zilizo kuwa makoloni ya Mwingereza ili kuzidisha uhusiano wa karibu na nchi za bara la Afrika.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi kutoka bara la Afrika pamoja na rais wa Ufaransa, wakati walipomaliza mkutano na serikali ya Ufaransa ili kudumisha uhusiano.
Uturuki ya laani vikali kitendo cha Izrael.
Ankara, Uturuki-01.06/2010. Waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amelaani kitendo cha jeshi la Izrael ni la kinyama na yamefanywa kinyume cha sheria za kimataifa.
Akiongea na viongozi wa serikali na kutangazwa karibu dunia nzima na mashirika tofauti ya habari waziri mkuu huyo alisema, "Asitokee mtu kuijaribu uvumilivu wa Waturuki, kwani tuna heshimu marafiki, na kukosanana na Waturuki ni gharama kwa mtu huyo na hatuacha kuisaidia watu wa Gaza na tutazidi kukemea vitendo vya Izreal."
Waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan, alikatisha ziara yake nchini Chile, mara baada ya tukio hilo kutokea.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, akihutubia kuhusu kitendo cha Waizrael kuvamia msafara wa misaada ya kibinadamu iliyo kuwa ikielekea Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo na majeruhi katika msafara huo.
Picha ya pili anaonekana kijana mdogo akiwa amebebwa kwenye mabega wakati wa harakati ya kupinga kitendo cha Izrael kuvamia meli iliyo kuwa ilielekea Ukanda wa Gaza.
Al-Qaeda namba tatu asadikiwa kuuwawa.
Pakistan, Lahore - 01/06/2010. Jeshi la Amerika na washiriki wake wamesema, "wamefanikiwa kumua anayesadikiwa kuwa namba tatu wa kundi la Al-Qaeda Mustafa Abu al-Yazid au kwa majina mengine Sheikh Sa'íd al Masri."
Kuuwawa huku kwa Mustafa Abu al-Yazid kulitokea kaskazini mashariki mwa Pakistan, kwa shirikiana na majeshi shiriki.
Picha hapo juu anaonekana Mustafa Abu al Yazid, ambaye inasadikiwa aliuwawa wakati wamashambulizi yaliyo fanywa na jeshi la Amerika na washiriki wake hivi karibuni.

No comments: