Wednesday, June 9, 2010

Iran yaongezewa vikwazo.

Iran yaongezewa vikwazo.

New-York, Amerika- 09/06/2010. Kamati ya usalama ya umoja wa mataifa imepitisha makubaliano ya kuwekewa vikwazo kwa serikali ya Iran.
Mswaada huo ambao ulipitishwa kwa kura 12 na mbili kupinga mswaada huo na moja kutopiga kura. Nchi ambazo zilipinga mswaada huo ni Brazil na Uturuki nchi ambazo ziliongoza mazungumzo na kuifanya Iran kukubali kuruhusu baadhi ya madini yanayo timika kutumika kuzalisha nguvu za nyuklia.
Hata hivyo serikali ya Iran imekilaani kitendo hicho na kusema, "Hatuta hathirika na vikwazo hivyo kwa kuto kuendelea na mpango wetu wa kuendeleza nyuklia ya kisayansi."
Picha hapo juu wanaonekana wanasayansi wa Iran wakiwa wanajadili maendeleo ya mitambo ya kuzalisha nguvu za nyuklia.
Picha ya pili wanaonekana wajumbe wa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa wakiwa katika mkutano kujadili mswaada wa Iran.

No comments: