Wednesday, June 23, 2010

Rasi Obama amteua mkuu wa majeshi mpya kuongoza NATO

Rais Obama amteua mkuu wa majeshi mpya kuongoza NATO.

Washington,USA - 23/06/2010. Rais wa Amerika Baraka Obama, ametangaza kujiudhulu kwa General Stanley McChrystal kuwa kiongozi mkuu wa majeshi ya NATO na kumteua General David Petraeus kuchukua nafasi yake.
Kutangazwa huko kunakuja baada ya General McChrystal kushutumu uongozi wa serikali ya USA kwa kuwa na myumbo katika kuendeleza vita nchini Afghanistan.
General Mc Chrystal aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na mahojiano na gazeti la Rolling Stone.
Rais Baraka Obama, alisema kujiudhuru huko kwa General McChrystal, hakuta badilisha msimamo wa USA nchini Afghanistan kupambana na kundi la Taliban. Picha hapo juu anaonekana General Stanley McChrystal akielekea ofisi za Ikulu ya Amerika kunana na rais Baraka Obama.
Picha ya pili anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama akielekea kutangaza kujiudhulu kwa General Stanley McChrystal, na nyuma anaonekana General David Petraeus akimfata rais kumtangaza rasmi kuwa kiongozi wa majeshi ya NATO.

No comments: