Thursday, August 5, 2010

Wakenya wakubali mabadiko ya katiba ya nchi.

Wakenya wakubali mabadiliko ya Katiba ya nchi.

Nairobi, Kenya - 05/08/2010. Matokeo ya uchaguzi wa kura ya maono yaliyolenga kubadirisha katiba ya nchi yamekubaliwa kwa asilimia kubwa.
Matokeo hayo ambayo yataleta mabadiliko makubwa katika katiba ya Kenya hasa kiuongozi na kisiasa.
Akiongea kwa furaha, kiongozi wa kampeni ya ndiyo, Kiraitu Murungi amabaye ni waziri wa nishati alisema "Wakenya wamekubali kwa pamoja na Kenya mpya imezaliwa"Wapigakura ya kukubali walipata asilimia 67.
Akiongea mara baada kiongozi aliye kuwa akiongoza kampeni za kupinga mabadiliko hayo Williamu Ruto ambaye ni waziri wa Elimu ya juu, aliseama "tumekubali matokeo ya kura."
Picha hpo juu ni bendera ya Kenya,nchi ambayo inatarajia kufanya mabadiriko ya kikatiba mara ya kura za wananchi walio wengi kukubali mabadiliko yafanyike.
Picha ya pili anaonekana mmoja wa raia wa Kenya akiwa ameshikilia karatasi iliyo andikwa 'ndiyo' kukubali mabadiliko ya katiba wakati wa kampeni.
Rais wa zamani wa Uganda aiga dunia.
Kampala, Uganda - 05/08/2010. Aliyekuwa rais wa Uganda Godfrey Binaisa, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa masemaji wa familia alisema " Mzee Godfrey Binaisa alifariki usiku wa manane nyumbani kwake."
Binaisa ambaye alitawala Uganda mara baada ya kuangushwa utawala wa Idi Amini Dada, aliwai pia kuwa mwanasheria wakatiwa uhamishoni nchini Amerika.
Picha hapo juu anaonekana Godfrey Binaisa enzi za uhai wake akihutubia moja ya mkutono kama mgeni rasmi.
Naomi Campbell akili mbele ya mahakama.
Hague,Uhollanzi-05/08/2010. Mahakama inayoshughulikia kesi za ukiukwaji wa haki za kibinadmu duniani leo imemuhoji mwanamitindo maharufu duniani Naomi Campbell.
Naonmi Campbell, aliongea katika mahakama hiyo, ili kutoa ushahidi kama alipokea alhmasi iliyo katwa kutoka kwa aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor mwaka 1997, wakati walipo kutana kweney chakula kilicho anadaliwa na aliyekuwa rais Afrika ya Kusini, Nelson Mandela.
Mwana mitindo huyo alikili yakuwa alipokea zawadi ya mawe kutoka kwa wanaume wawili waliokuja kumgongea wakati akiwa chumbani amalala na zawadi hizo alizichangia katika mfuku wa maradi wa Mandela ambao husaidia jamii.
Picha hapo juu anaonekana Naomi Campbell akitoa ushahidi mbele ya mahakama jijini Hague.
Picha ya pili anaonekana Naomi watatu kutoka kushoto wakati walipo pigwa picha ya pamoja na aliye kuwa rais wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela.

No comments: