Sunday, August 8, 2010

Pentagon wataka Wikileaks kurudisha nyaraka za siri.

Pentagon wataka Wikileaks kurudisha nyaraka za siri.

Washington, Amerika- 08/08/2010. Amerika imetaka chombo cha habari kilicho toa maelezo ya siri kuhusu mpango mzima wa kivita zidi ya kundi la Al-qaeda na Taliban kurudisha nyaraka zote kwa serikali ya Amerika. Wikileaks chombo ch a habari ambacho ndicho kilicho andika habari hizo, kimedai ya kuwa bado kina nyaraka za siri zipatazo 15,000 na huenda wakazitoa habari hizo muda wowote kwenye mitandao. Msemaji wa Pentagon Geoff Morrell alisema "tungeomba wikileaks watukabidhi karatasi hizo kwa ni watakuwa wamefanya jambo la busara na ninamatumaini watakubaliana na sisi katika swala hilo." Hata hivyo Wikileaks kuna tetesi ya kuwa "Wikileaks watachapisha siri zote ikiwa wafanyazai wa chombo hicho watasumbuliwa au kukamatwa." Picha hapo juu ni ya alama ya Wikileaks chombo cha habari ambacho kilitchapisha hivi karibuni nyaraka za siri za pipango ya kivita vinavyo endelea zidi ya Al-qaeda na washiriki wake nchini Afghanistan na kote duniani. Tarik Aziz ataka Amerika isawazishe makoso kabla ya kuondoka.
Baghdad, Iraq- 08/08/2010. Aliyekuwa waziri kiongozi wa serikali, wakati wa utawala wa Saadam Hussein, amesema kuondoka mapema kwa jeshi la Amerika nchini Iraq ni kuicha nchi hiyo katika hali ya hatari kubwa. Tarek Azizi ambaye kwa sasa anatumikia kifungo, alisema "Iraki haitakuwa Irak tena, na Amerika inatakiwa kubaki na kuijenga Irak kama walivyo ikuta, kwani Amerika imefanya makosa na hivyo lazima isahiishe makosa kabla ya kuondoka." Tarek Azizi, pia aliisifu serikali ya Saadam Hussein kwa kusema " Saadam hakuwa mwongo na hakubadilisha ukweli, ni mtu ambaye nilimweshimu na kumpenda na nimtu ambaye historia itatoa jibi wakati utakapo fika, kwani alijenga nchi, alitumika nchi yake na watu wake, na nchi za Magharibi zilimwelewa vibaya kutokana na sababu fulani." Pichani hapo juu anaonekana Tarik Azizi enzi za uongozi wake akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali halisi ya uongozi wa serikali yake. Fidel Castro aonya kuzuka kwa vita vya matumizi ya nyuklia.
Havana, Kuba - 08/08/2010. Rais wa zamani wa Kuba Fidel Castro, amehutubia taifa kwa mara ya kwanza tangu alipo achia madaraka ya uongozi.
Fidel Castro 83 amabye mpaka sasa ni kiongozi wa chama Commnist alionya ya kuwa dunia inaelekea kwenye mashindano ya kivita ambapo matumizi ya nyuklia huenda ya katumika.
Na alisema "Uongozi wa serikali ya Amerika unampango wa kuzishambulia Iran na Korea ya Kaskazini, vilevile ikiwa rais wa Amerika Baraka Obama atatoa ruhusa ya kuanza vita,basi watu wengi watateketea wakiwemo Waamerika wanao fanya kazi katika maeneoya Mashariki ya Kati,na huo utakuwa ndiyo mwisho wa kuwa na amri moja ya kidunia na kuleta mgongano mkubwa kwenye maeneo ya Mashariki ya Kati na kwingine kote duniani."
Vilelevile Fidel Castro alisema " swala la mkubwa mmoja kutoa amri litafikia mwisho na baadhi ya miundo mbinu ya kibiashara na fedha zita hathirika na kuangamia."
Pichani anaonekana aliye kuwa rais wa Kuba Fidel Castro akihutubia mkutano hivi karibuni jijini Havana.

No comments: