Sunday, August 1, 2010

Desmond Tutu kujihudhuru kazi za kiofisi.

Desmond Tutu kujihudhuru kazi za kiofisi. Cape -Town, Afrika ya Kusini - 01/08/2010. Aliyekuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Agrikan nchini Afrika ya Kusini na mshindi wa zawadi ya Amani ya Laureate Desmond Tutu ametangaza ya kuwa atajihudhuru na kutumia muda mwingi na familia yake. Akiongea hayo Askofu mstahafu alisema, "Nita kuwa nasiku moja ya kiofisi hadi hapo mwaka 2011 Februari. Askofu Desmond Tutu alikuwa mmoja wa viongozi waliopinga ubaguzi wa rangi. Picha hapo juu anaonekana Askofu mstahafu, ambaye ifikapo 2011 Februari atakuwa na muda mwingi wa kukaa na familia yake na kusimulia hadithi kwa wajukuu. Washukiwa wa mauaji ya Kampala kizimbani.

Kampala,Uganda - 01/08/2010. Mahakama nchini Uganda imeanza kusikiliza kesi inayo wakabili raia watatu kutoka nchini Kenya kwa kuhusika na mauaji ya watu wapatao 76.
Mauaji hayo yalitokea wakati mamia ya watu walikuwa wamekusanyika kuangalia fainali ya kombe la dunia July 11/ 2010 jiji Kampala.
Watuhumiwa hao ni Hussein Hassan Agad, Mohamed Adan Abdow na Idris Mogandu.
Picha hapo juu wanaonekana washitakiwa wakiwa mbele ya hakimu kusikiliza mashitaka zidi yao.
Jeshi la Kiholanzi la rudi nyumbani.
Kabul, Afghanistan - 01/08/2010. Jeshi la Kiholanzi limeanza rasmi kuondoka nchini Afghanistan, na kuwa jeshi la kwanza kutoka shirikisho la NATO kuondoka.
Jeshi hilo ambalo lilikuwa nchini humo kwa kipndi cha miaka minne.
Katika kipindi hicho chote nchini Afghanistan, jeshi hilo lime wapoteza wanajeshi wapatao 24.
Akiongelea kuondoka kwa jeshi hilo, katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen, alisema "kuondoka kwa jeshi la Kiholanzi siyo mwisho kwani jeshi jingine litakuja kuendeleza kazi.
Jeshi hilo ambalo lili anza kazi yake mwaka 2006, lilikuwa na kazi ya kutoa misaada ya kibinadamu na kusaidia kujenga uhusiano kati ya jamii nchini Afghanistan.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wanajeshi wa jeshi la Kiholanzi wakiwa kazini wakati walipo kuwa nchini Afghanistan.

No comments: