Wednesday, March 14, 2012

Mahakama ya Hague yamtia hatiani Thomas Lubanga.

Mahakama ya Hague yamtia hatiani Thomas Lubanga.

Hague, Netherlands - 14/03/2012. Mahakama inayo shughurikia  makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu iliyopo jijini Hague imemkuta na hataia aliyekuwa kiongozi wa Union of Congolese Patriots UPC Thomas Lubanga kwa kuwatumia vijana wadogo chini ya miaka 15 kama wanajeshi katika kundi lake.
Lubanga anatarajiwa kuhukumiwa siku za karibuni, kwa mujibu wa wanasheria waliofatilia kesi hii wanasema " huenda akahukumiwa kifungo cha maisha"
Thomas Lubanga, amekuwa kiongozi wa kwanza kukutwa na hatia tangu koti hiyo iliyopo Netherlands Hague kuanzishwa miaka 10 iliyo pita.

Ikulu ya rais wa Somalia yashambuliwa.

Mogadishu, Somalia - 14/03/2012. Watu watatu watano wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya ya bomu kulipuka kwenye Ikuru ya rais yaliyopo  mjini Mogadishu.
Kundi la Al-Shabab limekili kuhusika na "mlipuko huo na kuonya yakuwa milipuko  na mashambulizi mengine yatafuata."
Al Shabab walifukuzwa katika maeneo ya jiji la Mogadishu baadaya ya majeshi ya umoja wa Afrika kwa kusaidiana na majeshi ya Somalia kuzidi nguvu kundi la hilo.

No comments: