Mswada wa Kofi Annan juu ya Syria wakubaliwa na Umoja wa Mataifa.
New York, Marekani - 21/03/2012. Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa imepitisha mswada ulio pendekezwa ili kuleta amani nchini Syria.
Mswaada huo ambao ulipendekezwa na aliye kuwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Kofi Annan
ambaye alipewa jukumu la kusuruhisha mgogoro wa kisiasa uliyopo nchini Syria, ambao umesababisha vurugu na vifo vingi nchini huko.
Mswaada huo ambao unazitaka pande zote mbili, serikali ya Syria na wapinzani kuweka siraha chini ili kutoa njia kwa misaada inayotakiwa kutolewa kwa watu walioathirika na vita na kila pande ikubali kumaliza mgogoro huu kwa kukaa chini ya meza na kuongea."
Mswaada huo pia ulikubaliwa na China na Urussi nchi ambazo hapo mwanzo zilipinga mswaaada uliopendekezwa kabla ya huu mpya uliotolewa na Kofi Annan.
Mwingereza aliyetekwa nyara nchini Somalia ahachiwa huru.
Judith Tebbut 57 alisema " nafurahi kuwa huru japo ninamajonzi kutokana na kifo cha mume wangu na nashukuru kupata fursa ya kuwa na familia yangu tena.
Nawakati wote nilipo kuwa chini ya maharamia hawakuni nyanyasa, na walikuwa wananiangalia kwa makini, na hasa nilipo umwa walitoa matibabu haraka."
Kundi lililo mteka nyara limedai yakuwa "kunamalipo ya pesa zilitolewa na ndipo wakaamua kumwachia huru Judith."
Judith Tebbutt ambaye alitekwa nyara katika mji wa Lamu ulipo kwenye pwani ya bahari Indi nchi Kenya mapema mwezi Semptemba 2011 wakati wakiwa katika mapumzikoni nchini Kenya na mume wake kuuwawa wakati wa tukio la kutaka kuwateka nyara wote.
Ofisi ya mabo ya nje ya nchi Uingereza imethibitisha kuachiwa huru kwa Judith Tebbutt na kuhusu swala la kutolewa kiasi cha pesa, msemaji wa serikali alikanusha madai hayo na kusema "cha umuhimu kwa sasa ni kuhakikisha Judith anaelekea nyumbani kwani amechoka na anahitaji kuwa na mapumziko na kujiunga na familia yake.
No comments:
Post a Comment