Hugo Chavez arudi nyumbani baada ya matibabu nchini Kuba
Karakas, Venezuela - 17/03/2012. Rais wa Venezuela amewasili nyumbani baada ya kumaliza matibabu ya kansa ambayo ilikuwa ina muathiri afya yake.
Rasi Hugo Chavez akiongea kutoa shukurani kwa wale wote walio mwombea na kuwa naye katika wakati mgumu wa ki afya alisema "nimerudi nyumbani na nguvu mpya na nipo tayari kuongoza jahazi"
Hugo Chavez alitolewa uvimbe wakati wamatibabu yake nchini Kuba.
Venezuela nchi ambayo inakalibia kufanya uchaguzi wa rais, Hugo Chavez anatarajiwa kugombea tena kiti cha urais wa Venezuela kwa mara nyingine tena.
Aliyehusika na mauaji ya Sobibor aaga dunia.
Berlin, Ujerumani - 17/03/2012. Askari wa mwisho aliyehusika katika mauji katika kambi ya Sobibor nchini Paland amefariki dunia.
John Demjanjuk 91 ambaye alikutwa na makosa ya kuhusika katika mauaji zaidi ya watu 167,000 wakati akiwa kama mlinzi kati ya mwaka 1942-43.
Habari za kuhusika kwa Demjanjuk kuhusika katika vifo hivyo zilipatikana katika kumbukumbu za mauaji ya Holokost ambayo yalifanya afunguliwe kesi na kukutwa na hatia baadaye alihukumiwa kwenda jela miaka mitano.
Hata hivyo Demjanjuk alikata rufaa na kuruhusiwa kuishi katika nyumba za wazee ambapo ndipo umauti ulimkuta.
Iran ya dai yakuwa Izrael haina uwezo wa kupigana vita zaidi ya wiki.
Tehran, Iran - 17/03/2012. Waziri wa mambo ya nje wa Iran ametahadharisha ya kuwa kitendo cha Izrael kushambulia maeneo yaliyo na mitambo ya kinyuklia ya Iran kitaleta matokeo ambayo hayatasemeka.
Ali Akbar Salehi alisema " kitendo cha Izrael kushabikia vita zidi ya haikisaidii kwani kama vita vikiianza basi Izrael haina uwezo wa kupigana zaid ya wiki moja, hivyo kila kitisho kinachotolewa tunakichukulia kwa makini na hatuzani kama Izrael ni kitisho kwa Iran."
Iran imekuwa ikisukumwa kusimamisha mradi wake wa kinyuklia na nchi za Magharibi, jambo ambalo Iran imekuwa ikidai ya kuwa ni haki kwa nchi hiyo kuendelea na mradi huo wa nguvu za kinyuklia kwani ni kwa ajili ya maendeleo ya kisayansi.
Serikali ya Syria yadai Saudi Arabia inawauzia siraha wapinzani.
Waziri wa habari wa Syria Adnan Mahmoud alisema " Saudi Arabis na Katar ni nchi ambazo zipo mbele katika kuwasaidia wapinzani wa serikali ambo wengi ni maharamia wanatumia siraha hizo kinyume na sheria na hata kuwadhuru raia."
Maelezo hayo yamekuja baada ya bomu kulipuka katika jiji la Damascus na kuuwauwa zaidi ya watu 20 na kuwajeruhi watu wapatao 27.
Serikali ya Syria imekuwa ikidai ya kuwa tangu mwezi wa Machi 2011, Saudi Arabia na washiriki wake wamekuwa wakishiriki katika kuwapa siraha wapinzani wa serikali na kusababisha machafuko nchini Syria.
No comments:
Post a Comment