Tuesday, March 13, 2012

Muamar Gaddafi alikuwa mtu wa karibu wa Nicolas Sarkoozy.

Ndizi zilizo iva ni muhimu kwa nguvu za kiume.

Kampala - Uganda - 13/03/2012.  Ndizi zilizo iva au kwa jina jingine "banana" zimetambulika kwa kuongeza nguvu zaa kiume mwilini.
Kama inavyo julikana ndizi zilizo iva zinakusaanya vitamini na vilishe  vya potassium, chuma zinc, cabohydrates,B6,A,C,B1,B2 na E ambavyo uhongeza nguvu.
Mataalaamu wa mambo ya  lishe Geoffrey Babaghirana alisema " ndizi zinasaidia kukuza nguvu za mwili hasa kwa wanaume na kuongeza uwezo wa kimapenzi kutokana na vilishe vinavyo patikana katika zao hilo na vile vile zinajenga ngozi ya mwili kutokana na kuwa na Vitamini C."
Zao la ndizi ni chakula kikuu katika jamii kubwa ya Waganda na sehemu za Tanzania zilizo pakana na Uganda.

Muamar Gaddafi alikuwa mtu wa karibu wa Nicolas Sarkoozy.

Paris, Ufaransa - 13/03/2012. Shirika moja linaloshughurikia uchunguzi wa maswala ya siasa na siri zake limetoa habari kuwa rais wa Libya Muaamar Gaddafi alichangia pesa ili kumsaidia rais wa Ufaransa.
Kwa mijibu wa shirika hilo zinasema "kiasi cha Euro 50 million zilitolewa kwa rais wa sasa wa Ufaransa Nicolas Sarkozy  na rais wa Libya Muammar Gaddafi kabla ya kuangushwa kutoka madarakani."
Hata hivyo rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alikanusha madai hayo kwa kusema " nafikri mnajua ya kuwa Gaddafi alikuwa akiongea atakalo na hizi habari si za ukweli."
Uhusiano wa rais Sarkozy wa Ufaransa na rais Gaddafi wa Libya ulikuwa wa karibu saana na hasa pale iliposhuhudiwa rais Sarkozy kumwalika Muammar Gaddafi nchini Ufaransa baada ya uchaguzi mkuu wa Ufaransa.

Mashambulizi ya mabomu yatokea Nairobi.

Nairobi, Kenya - 13/03/2012. Mabomu yamelipuka hivi karibuni katika jiji la Nairobi na kusababisha vifo na watu wengine kujeruhiwa.
Msemaji wa polisi Charles Owinom alisema " kulikuwepo na milipuko tofauti ambayo imesababisha vifo vya watu wanne na watu wapatao 40 wamejeruhiwa."
Jeshi la Polisi nchini Kenya limeilaumu kundi la Al-Shabab kwa kuhusika na mashambulizi na kuhaidi ya kuwa mashambulizi hayo hayata tikisa taifa la Kenya.
Mashambuulizi hayo yaliyofanyika hivi karibuni ni mrorongo wa mashambulizi ambayo yamefuatia yale yaliyo tokea mwishoni mwa mwaka  jana na kusababisha maafa kwa jamii.

No comments: