Iran yakubalia kuendelea mazungumzo juu ya haja na mipangoo ya kinyulia.
Marekani, Fransi, Britain, China, Urussi na Ujerumani zimekubali kuanza mazungumzo ambayo yalikuwa yamesimamishwa kutokana na kutokuelewana kati ya nchini hizo na Iran.
Rais wa Marekani Baraka Obama alisema " hii ni faida kwa kila mtu, kwani kutatua swali hili kiamani ni jambo la maana."
Wakati huo huo, serikali ya Iran imetoa ruhusa kwa wakaguzi wa maswala ya kinyuklia wa kimataifa kutembelea eno la kambi ya jeshi ambao linazaniwa kuwa na mitambo ya kinyuklia.
Marekani na waashiriki wake wamekuwa wakishuku ya kuwa Iran inampango wa kutengeneza sirha za kunyukia, jambo ambalo Iran imekataa ya kuwa inampango huo.
Machifu watanagaza serikali yao nchini Libya.
Benghazi, Libya - 07/03/2012. Serikali ya mpito ya Libya imetangaza kupinga kitendo cha viongozi wa Mashiriki ya Benghazi kutangaza kujitawala na kuunda serikali yao.
Kiongozi wa serikali ya mpito Mustafa Abdel Jalil alisema " tutalinda muungano na Libya ni moja, hatupo tayari kuigawa nchi.
"Ningependa kuwatahadharisha ya kuwa wawe waangalifu na wafuasi wa Muamar Gaddafi na serikali itatumia kila nguvu zilizopo kulinda Libya na inashangaza ya kuwa baadhi ya nchi za Kiarabu zimeounga mkono uamuzi huo na nisingependa kuzitaja."
Libya ilizaliwa mwaka 1959 -63 baada ya kuungana kwa majimbo ya kichifu ya Cyrenaica, Tripolitania na Fezzan.
Aliyefanya mauaji nchini Norway afunguliwa kesi ya uhaini namauaji.
Olso, Norway - 07/03/2012. Serikali ya Norway imemfungulia mashitaka ya kesi ya uhaini na mauaji kwa raia wanchi hiyo ambaye aliyafanya na kuisitua dunia nzima.
Anders Behring Breivik 33 amefunguliwa kesi hiyo, baada ya mauaji aliyo yafanya kwa kuua watu 77 kwa kuwapiga risasi katika kituo Utoeya na kuhuusika na kutega mabumu katika jiji la Olso.
Mwanasheria wa serikali Svein Holden alisema " Anders amefanya makosa ya kihaini ambayo ni ya kihistoria katika nchi yetu."
Kwa mujibu wa habari zilizopo zinasema huenda Anders Behring Breivik akahukumiwa kwenda jela miaka 30 ingawa hapo awali alionekana na ubovu wa akili.
Mwakilishi wa umoja wa Maataifa awasili nchini Syria.
Bab Amr, Syria - 07/03/2012. Mwakillishi wa Umoja wa Mataifa katika kushughulikia haki za binadamu amewasili nchini Syria na kutembelea maeneo yaliyo athirika na mapambano.
Valerie Amos alitembelea Bar Amr baada ya serikali ya Syria kuhakikisha yakuwa hali ya usalama wake ulikuwa umekamilika.
Waziri wa mambo ya nje wa Syia Walid Muallem alimweleza ya kuwa serikali ya Syria inatoa huduma za chakula n madawa kwa wale wote walio athirika na mashambulizi hayo.
Valerie Amos aliwasili nchini Syria baada ya kukubaliwa kutembelea maeneo yaliyoathirika na vita kati ya majeshi ya serikali na yale yanayo pinga serikali ya Syria.
No comments:
Post a Comment