Monday, May 12, 2014

Wanajeshi wa kukodiwa watumika nchi Ukraine


Serikali ya Nigeria yapinga matakwa ya kundi la Boko Haram.

Maiduguri, Nigeria - 12/05/2014. Kundi la kigaidi la Boko Haram, limesambaza na kuzimeonyesha video za wasichana wa shule iliyowateka karibuni wiki nne zilizo pita.
Video ya kwanza ilikabidhiwa kwa shirika la habari la Ufaransa AFP na baadaye kuanza kuonekana katika mitandao tofauti ambapo wasichana hao walionekana wa kiswali.

Akiongea baada ya kuonyeshwa kwa video hiyo ya wasichana hao, mkuu wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau alisema " wasichana hawa watashikiliwa hadi hapo wanachama na wapiganaji wa Boko Haram watakapo achiwa huru"

 Naye mwakilishi wa BBC aliyepo Nigeria John Simpson amesema "kubadili nia huko kwa kundi hilo la Boko Haram kumeo nyesha kuwa kundi hilo lipo tiyari kuongea kuhusu kuachiwa kwa wasichana hao."

Kundi la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2002 na toka hapo limekuwa likifanya mashambulizi zidi ya raia na ikiwa ni njia ya kuonyesha kupingana na mwenendo wa serikali ya Nigeria.

Jina Boko Haram linamaana ya kuwa  elimu na utamaduni wa kutoka nchi za Magharibi ( Ulaya na Marekani) ni marufuku kufuatwa na  wanchi wa Nigeria hasa wale walipo katika jimbo la Maiduguri

Wanajeshi wa kukodiwa watumika nchi Ukraine.


Donetsk, Ukraini - 12/05.2014. Maafisa usalama wa jimbo la Donetsk wamethibitisha madai yaliyotolewa na gazeti la Bild am Sonntag la Ujerumani   kuwa wanajeshi mamluki wa kukodiwa kutoka shirika la ulinzi  linaloitwa Xe Services lenye makao yake nchini Marekani  wameletwa nchi Ukraine ili kusaidiana na jeshi katika harakati za kupambana na wanapingana wanaopingana na serikali ya sasa ya nchi hiyo.

Mapema April 29/2014 gazeti la Bild  am Sonntag lililipoti kuwa kitengo cha usalama cha Ujerumani (BND) kilimpa maelezo Kansela Angela Merkel kwa kumweleza kuwa wanajeshi wa kigeni wa kutoka shirika la Xe zamani lililo julikana kama Blackwater na washiriki wake wapo nchi Ukraine tayari kusaidiana na serikali ya Kiev.

Maafisa hao wa usalama wamesema kuwa kuna idadi ya wanajeshi 400 mamluki ambao wapo nchi ni Ukraine na baadhi yao wameonekana kushiriki katika operesheni nzima ya kupambana na  wapinzani wa serikali ambao serikali ya Kiev inadai kuwa wanaungwa mkono Urusi, japo Urusi imekuwa ina kana kuhusika na hali ya machafuko yaliyopo nchini Ukraine na kwa kudai serikali iliyopo ndiyo ya kulaumiwa kutokana na machafuko yaliyopo nchini humo.

Nguvu za kisayansi katika jeshi la Iran za zidi kuonekana.


Tehra, Iran -12/05/2014. Iran imefanikiwa kutengeneza ndegeaina ya drone, ndege ambazo huwa zinaendeshwa bila rubani  ikiwa ni njia moja ya nchi hiyo ya kuweza kwenda sambamba na nchi nyingine ambazo zina ndege za aina hiyo.

Ndege hiyo ilionyeshwa kwa wataalamu wa kijeshi kutoka Urusi ambao walikuwa nchi Iran kikazi na kuelezwa kuwa "drone hiyo ambayo imetengenezwa kwa kufanana  na za Kimarekani, itakuwa na uwezo wa kurekodi maelezo ya picha na mienendo yoyote itakayo agiziwa kufanya na wataalamu wa  drone hizo"

Iran imekuwa na mikakati mikubwa ya kujiendeleza kisayansi na kiteknologia na vile vile kuhakikisha inaongeza nguvu zake za kijeshi tangu nchi hiyo ilipo kuwa na vita na Irak katika miaka ya 1980-89, na baadaye kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi.

 Na kutokana na vikwazo hivyo, Iran ilianza kuonyesha umairi wake wa kisayansi katika kijeshi mnamo mwaka wa 1992 baada ya kufanikiwa kutengeneza vivaru cha kivita, mizinga na ndege za kivita ikiwa kama njia ya kujihami.