Thursday, June 5, 2014

Wakuu wa G7 vichwa kuuma juu ya Urusi.

Rais Bashar al Assad ashinda tena uchaguzi mkuu nchini Syria.

Damascus, Syria - 05/06/2014. Matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais  uliyofanyika 03/06/2014 nchi  Syria umempa ushindi mkuu rais wa sasa wa Syria kwa asilimia kubwa.

Bashar al Assad ambaye ndiye rais wa sasa wa Syria na ambaye alikuwa akigombea kiti hicho kwa mara nyingine ameshida uchaguzi huo kwa mara ya tatu kwa asilimia zaidi ya 90 kutoka kwa wapiga kura milioni 10.

 Hata hivyo matokeo ya ushindi  wa kura wa rais Bashar al Assad, umepingwa vikali na serikali za Marekani na washiriki wake kwa kudai ya kuwa " Uchaguzi huo haukuwa wa maana na hakuwa wa halali na ni uchaguzi sifuri."

Hata hivyo Iran ambayo ni mshiriki mkuu wa serikali ya Syria imesema
"kitendo cha kuchaguliwa tena rais  Bashar Hafez al Assad ni pigo kwa wapinzani wa watu wa  Syria, na hasa ni kitendo cha aibu kwa Marekani na washiriki wake kwani hawapo kwa aajili faida ya watu wa Syria bali wanacho angalia ni maslahi yao"

Syria imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wale wanao unga mkono serikali ya rais Bashar al Assad na wapinzania wake jambo ambalo limesababisha maelfu ya Wasyria kukimbia nje ya  nchi na mamia kupoteza maisha yao.

Rais Bashar al Assad, ameshinda uchaguzi huo ambao ulikuwa wa vyama vingi na anatarajiwa kushika utawala wa kiti hicho cha urais kwa muda wa miaka saba ijayo.

Rais  Vladmir Putini ataka ushahidi uonyeshwe hazarani.

Paris, Ufaransa - 05/06/2014. Rais wa Urusi amezitaka Marekani na washiriki wake kuonyesha ushaidi kwa jumuiya ya kimataifa kuwa majeshi ya Urusi yapo nchi Ukraine.

Rais Vladmir Putin aliyasema hayo wakati alipo kuwa akiongea na waandishi wahabari jijini Paris, ambapo amewasili nchini Ufaransa kwa ajili ya sherehe za kumbukumbu ya miaka 70 ya vita vya pili vya dunia.

Akiongea rais Putini alisema " ni jambo la kushangaza, ikiwa kuna wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine mbona mpaka sasa hawajaonyesha ushahidi"

" Dunia nzima inakumbuka wakati Marekani ilipo toa ushaidi kuwa Irak ina siraha za sumu, kuwa kuonyesha, malori na chupa zilizo kuwa na unga aina ya poda ambazo walidai sumu na ni za Saddam Hussein, na kwa kigezo hicho wakavamia Irak na baadaye Saddam Hussein alinyongwa, muda haukupita ikajulikana kuwa Irak haikuwa na siraha za sumu."

" Na ushahidi kuhusu Irak, ulitolewa mbele ya kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa, hivyo napenda kukumbusha kuwa, kuongea ni vyepesi na kutoa ushaidi wa huhakika ni hali nyingine."
 
Akisisitiza rais Putini alisema "baada ya mapinduzi ya serikali nchini Ukraine Februari mwaka huu,  Urusi iliunga mkono na kusimamia kura ya maoni ya jimbo Cremia kutaka kujiunga na Urusi, kwani hii niuamuzi wa watu wa Cremia na hii ipo katika kifungu cha 1 cha katiba ya Umoja wa mataifa."

Maelezo hayo ya rais  Putin yamekuja baada ya Marekani na washirika wake kudai kuwa Urusi ndiyo chanzo cha vurugu zinazo endelea nchi Ukraine.

Hata hivyo, rais Putin alisema kuwa yupo tiyari kukutana na kiongozi yoyote kuongea naye kuhusu  masuala ya kimataifa ikiwemo ya Ukraine wakati atakapo kuwa nchini Ufaransa, na kama rais wa Marekani yupo tiyari, basi yeye hanakipingamizi.

Wakuu wa G7 vichwa kuuma juu ya Urusi.

Brussels, Ubeligiji - 05/06/2014. Viongozi wa nchi za G7 au nchi zenye maendeleo ya kiuchumi wameionya Urusi kuwa huenda ikakumbwa na vikwazo zaidi ikiwa haita badili mwenendo wake kwa nchi ya Ukraine.

Onyo hilo lilitolewa na rais wa Marekani Baraka Obama , mara baada ya mkutano wa pamoja na viongozi wenzake wa G7 na uongozi wa jumuiya ya nchi za umoja wa Ulaya.

Rais Obama alisema " dunia inategemea uchumi shirikishi unaokuwa kwa pamoja, leo Urusi inajikuta haipo katika kuinuua uchumi wake, kwa ajili ya uchaguzi potofu unaofanywa na uongozi wa Urusi."

" Hivyo ipo haja ya Putin kuitambua serikali ya rais Petro Poroshenko na pia kusimamisha upelekeji wa siraha kwa wapinzani wa serikali ya Ukraine."

"Putin ananafasi ya kufuata sheria za kimataifa" Aliongezea rais Obama.

Mkutano wa wakuu wa G7, imefanyika baada ya ule mkutano  uliyokuwa ufanyike wa nchi za G8  kwenye mji wa Sochi Urusi kugomewa na Marekani na washiriki wake, kwa madai kuwa Urusi imejiingiza katika masuala ya Ukraine.


No comments: