Tuesday, June 3, 2014

Abdul Fattah al Sisi ashinda uchaguzi wa Urais nchini Misri.

Rais Obama atangaza msaada kwa NATO.

Warsaw, Poland - 03/06/2014. Serikali ya Marekani imetangaza kutoa pesa ili kusaidia   kuikuza NATO kiulinzi kwenye bara la Ulaya.

Hayo yalisemwa na rais Baraka Obama wakati alipo kuwa akihutubia jiji Warsaw, Poland wakati wa alipokutana na wanajeshi wa Kimarekani waliopo nchini humo.

Rais Obama alisema "tukiwa marafiki na washirika wakubwa ni jukumu letu kujilinda kwa pamoja, na naomba wabunge wa kongresi waunge mkono wito wakukubali kutoa dola billion moja ilikuweza kufanikisha lengo hili kwani usalama wa washiriki na marafiki zetu ni usalama kwetu pia."

 |April mwaka huu wanajeshi 150 wa Kimarekani waliwasili nchini Poland, baada ya hali ya machafuko kuongezeka nchini Ukraine.

Rais Baraka  Obama alipokelewa na mwenyeji wake rais Poland Bronislaw Komorowsiki kwenye uwanja wa Kijeshi ambapo ndipo waliongea na kutoa hotuba kwa pamoja.

Baada ya kumaliza ziara yake nchi Poland rais Obama atatembelea  nchi Ubeligiji na baadaye pia kuwasili Ufansa ili kuhudhuria sherehe ya miaka 70 tangu kuisha vita vya pili vya dunia.

 Waziri mkuu wa Uturuki akemea CNN.


Istambul, Uturuki - 03/06/2014. Waziri mkuu wa Uturuki ameyalaumu mashirika ya habari ya nchi za magharibi kwa kutangaza habari kwa kupendelea na pia kuwa kama makampuni ya makachero.

Waziri mkuu  Recep Tayyip Erdogan aliyasema hayo wakati alipo kuwa akihutubia katika mkutano wa wanachama wake wa chama cha AK  na kutoa mfano kuwa  CNN ni moja ya shirika la habari ambalo limekuwa likifanya kazi yake kama ofisi ya kikachero.

Akiongea waziri mkuu Erdogan alisema "CNN ilitumia masaa nane wakati wa siku ya kumbu kumbu ya Gezi, na mwaka huu wamekamatwa na kuonyesha kuwa hawafati maadili ya uandishi na kazi yake ni kuchangia kuvuruga nchini."

"Ni jukumu langu kuhakikisha Uturuki inakuwa salama kwa kila mtu, na polisi wanatakiwa kufanya kazi yao bila kuingiliwa ili kuleta usalama na nitawalinda kwa hali na mali."

"Mbona hawaonyeshi yanayo fanywa na polisi nchini Marekani au Uingereza?" 

Waziri mkuu Tayyip Erdogan, alilitaja shirika la habari la CNN kuwa katika ripoti yake ya vurugu zilizo tokea mwaka 2013 katika kiwanja cha Taskim, ilikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya nchi za kigeni na mpaka sasa bado mashirika hayo yanania ya kukuza mvugo wa amani nchini Uturuki. 

Kuongea huko kwa waziri Erdogan umekuja baada ya mmoja wa waandishi wa habari wa CNN kukamatwa wakati wa maandamano na baadaye kuachiwa  huru baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda wa zaidi ya dakika 45.

Abdul Fattah al Sisi ashinda uchaguzi wa Urais nchini Misri.



Kairo, Misri - 03/06/2014. Matokea ya uchaguzi nchini Misri yamempa ushindi mkubwa Abdul Fattah al Sisi ambaye alikuwa anagombania kiti cha urais.

Sisi ambaye alikuwa mkuu wa majeshi na kuachia magwanda Machi 26 2014, ameshinda kwa wingi wa kura za asilimia 96.91 katika uchaguzi mkuu uliyo fanyika Misri.

Ushindi huo wa Sisi, umekuja miezi tisa tu, baada ya kuhusika katika mapinduzi ya serikali ya rais Mohammed Morsi  na  ambaye alimchagua Sisi kuwa mkuu wa majaeshi. 

Tangu kuangushwa kwa serikali ya Hosni Mubara mwaka February 11/ 2011, Misri imekuwa na misukosuko ya kisiasa na kupelekea kuvuruga  nchini humo, jambo ambalo Sisi amehaidi kulipatia jibu na pia kusema "itachukua miaka 25 ili kuleta demokrasi kamili nchi Misri."

Abdul Fattah al Sisi anatarajiwa kuapishwa kuwa rais siku ya Jumapili wiki hii.

Mwizi wa kimtandao atafutwa kwauvumba na ubani.


Washington, Marekeni - 03/06/2014. Marekani inamsaka raia wa Urusi ambaye alifanikiwa kuingia katika mfumo mzima wa kimtandao na kuiba mamilioni ya pesa katika mabenki tofauti duniani.

Evgenivy Bagacgev 30 ambaye ametajwa kama mtuhumiwa wa wizi wa kimitandao, anatakiwa kujibu mashitaka ya kuhusika na kutengeneza mfumo wa kimtandao ambao uliweza kutengua mfumo mama wa kiulinzi wa kibenki na kuweza kupenyeza na kuiba pesa tangu 2006. 

Akiongea mara baada ya kutoa wajihi wa mtuhumiwa, mmoja  wa mkuu wa kitengo cha usalama wa mitanndao wa  Marekani Leslie Caldwell  alisema "mfumo aliyotengeneza Bagacgev ni wa hali ya juu na ilikuwa vigumu kuugundua, na hii tuliweza kugundua kwa kushirikiana na nchi 10 ambazo zilikumbwa na matatizo haya na hivyo lazima atafutwe kwa uvumba na ubani"

Evegenivy Bagacgev anasemekana kwa mara ya mwisho alionekana katika maeneo ya Black See kwenye kitongoji cha Anapa akijiliwaza .

 Wapalestina wapata serikali mpya.


Ramallah, Palestina - 03/06/2014. Wapelestina wamepata serikali ya muungano, ambayo itakuwa na kazi kubwa ya kuuanda matayarisho ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge.

Serikali hiyo ambayo imeunganisha vikundi vya Hamas na Fatah, itakuwa na viongozi 17 kutoka pande zote. 

Kuundwa huko kwa serikali ya muungano, kumekuja baada ya majadiliano yaliyo chukua wiki tano na kufanikiwa kufikia tamati kwa makubaliano ambayo yalifanyika April 23 mwaka huu.

Akiongea mara baada ya kuundwa na kula viapo kwa viongozi wapya wa Kipalestina, rais wa Wapelestina Mahamoud Abbas alisema "serikali hii itakuwa ya mpito, na maswala ya ukombozi wa Wapalestina katika majadiliano ya amani na Izrael yapo chini ya PLO - Palestina Liberation Organasation, na serikali hii kama serikali zilizo pita, itafuata na kutii sheria zilizo sainiwa hapo awali."

Hata hivyo kitendo cha Fatah na Hamas kuungana na kuunda serikali, kimepingwa vikali na Izrael, na kuitaka Marekani kutounga mkono serikali hoyo.

Uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi kwa Wapalestina unatarajiwa kufnyika mwaka 2015

Mfalme wa Uispania kuachia madaraka.

Madrid, Uispania - 03/07/2014.Mfalme wa Juan Carlos Uispania ametangaza kuachia kiti cha ufalme, baada ya kukikalia kwa miaka arobaini.

Akiongea kumwakilisha Mfalme Juan Carlos, waziri mkuu wa Uspania Mariano Rajoy alisema " Mfalme Juan Carlos ameamua kuachia uongozi wa kifalme, ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya na pia nakuwa na matumaini katika kurekebisha makosa ambayo yametokea katika harakati za  kuijenga na kuimarisha Uispania"

Mfalme Juan Carlos, amependekeza kuachia kiti hicho kwa mwanae 46 Prince Phillipe, ambaye anatazamiwa kuwa mfalme wa kizazi cha kisasa na kuwa na majukumu  magumu ya kuimarisha ufalme, kutokaa na baadhi ya kashfa kuzuka katika ufalme huo.
 Na vile vile kutokea upinzani wa hapa na pale  wakupinga uongozi wa Kimfalme nchi Uispania

No comments: