Wednesday, September 3, 2014

Mgonjwa wa Ebola raia wa Uingereza apona.

Tutawasaka wauaji na kuwaangamiza asema rais Baraka Obama.

 Estonia, Tallinn - 03/09/2014. Rais wa Marekani, amelaani kitenndo cha kuuwawa kinyama kwa raia wa Marekani ambaye alikuwa akishikiliwa na kundi la ISI linalo pambana na serikali ya Irak na sekali ya Syria.

Rais Barak Obama alilaani kitenndo hicho, baada ya  kundi la ISI kusambaza video kwenye mitandao inayo onyesha kuuwawa kinyama kwa raia wa Kimarekani Steven Sotloff ambaye alikuwa akifanya kazi ya uandishi wa habari.

 Akiongea wakati wa ziara yake nchini Estonia,  rais Baraka Obama alisema '' vyovyote kundi la ISI litakavyo fanya, halitafanikiwa, na watambue tutawasaka na kuwaweka kwenye vyombo vya sheria.''

'' Na wakae wakijua hatuwaachia wala kusahahu kwa vitendo wanavyo vyao vya kinyama wanavyo fanyaa''Alisisitiza rais Obama.

Kuuwawa kwa Steven Sotloff kumekuja baada ya raia mwingine wa Marekani James Foley kuwawa kinyama  na kundi ISI mwezi uliyo pita.

Hadi sasa kundi la ISI limefanya mauaji ya kinyama kwa raia  wawili wa Marekani, ambao wote walitekwa nyara wakati walipokuwa wakufanya kazi za uandishi wa habari, napia kudai kuwa siku za mbeleni lita muua raia wa Uingereza walie naye ikiwa mashambulizi ya ndege za kivita yanayo fanyiwa na Marekani, Uingereza na washiriki hayatasimamishwa.

 Rais, Obama alifanya ziara nchini Estonia, ili kuzihakikishia nchini za Baltik kuwa Marekani na washiriki wake chini ya muungano wa kiulinzi wa NATO upo tiyari kuwasaidia muda wowote kwa hali na mali, na hasa kwa sasa ambapo nchi za Baltik zimekuwa na wasiwasi na jirani ya Urusi.

Kundi la Aqaeda kufungua matawi barani India.

 Al Qaeda - 03/09/2014. Kiongozi wa kundi la Al Qaeda ametangaza kuwa kundi lake litafungua matawi katika nchi  zilizopo katika bara la India ili kukuuza uhusiano na wale wanao unga mkono kundi la Al Qaeda.

Akiongea Ayman al Zawahri alisema, ''Burma, Bangladesh, Assam, Gujarat, Ahmedabad, na Kashimir kwani maeneo haya ni muhimu sana na nia yetu ni kuhakikisha ndugu zetu katika Uislaam wanatendewa haki.''

'' Navile vile napenda kuwaeleza ndugu zetu wa waliipo Afghanistan chini ya uongozi wa Mullah Omar ya kuwa tupo  pamoja.'' Zawahri aliongezea.

Akiongea kuhusu kundi la ISI, kiongozi huyo wa Al Qaeda  Ayman Zawahri alisema '' nikitu ambacho hakitakiwi kufanyika kwa Muislaam kumuonea Muislaam mwingine kwa hali na mali, hivyo ISI wafanyavyo wanakwenda kinyume na Maadili ya Uislaam.

Ugomvi kati ya  ISI na Al Qaeda ulitokea mwaka 2013, baada ya kundi ISI kuanza kushambulia nchini Syria na vitendo vingine vya kuufanya mauaji ya kinyama nchini Irak.

Ayman Zawahri, alichukua kiti cha uongozi mwaka 2011, baada ya jeshi la Marekani kufanikiwa kumwua Osama bin Laden nchini Pakistani.

Mgonjwa wa Ebola raia wa Uingereza apona. 

London, Uingereza - 03/09/2012. Muuguzi raia wa Uingereza ambaye alikuwa amekumbwa na ugonjwa wa hatari wa Ebola, ameruhusiwa kutoka hospitali .

William Pooley 29, ambaye alipata ugonjwa wa Ebola wakati alipo kuwa akifanya kazi nchini ya uuguzi nchini Sierra Leone, alikimbiziwa nyumba Uingereza ili kupata matibabu na alipofika alizwa katika hospitali ya Uhuru wa Kifalme iliyopo London hadi alipo ruhusiwa baada ya waganga kuridhika ya kuwa amepona baada ya kutumia dawa aina ya ZMapp..

 Akiongea mara baada ya kutoka hopspitali, William Pooley alisema ''Nina bahati kupona, kwa nimeshuhudia ugonjwa wa Ebola ulivyo waua watu wengi na ukweli nilikuwa na wasiwasi kuwa nitakufa, jambo ambalo hata familia yangu ilikuwa na wasiwasi pia.''

Mganga Michael Jacobs aliyeongoza katika matibabu ya muuguziWilliam Pooley  alisema '' Pooley yupo mzima na ugonjwa aliyokuwa nao, sasa anweza kwenda nyumbani kuendelea na maisha yake kama kawaida.

Ugonjwa wa Ebola umekuwa tishio kubwa hasa katika bara la Afrika kwenye maeneo ya Afrika Magharibi na sehemu kadhaa nchini Jamuhuri ya Kongo, umepoteza maisha ya watu zaidi 3,500 na wengi wao kutoka Liberia, Sierra Leone, Guinea, Nigeria na Senegal na hivyo dawa ya ZMapp huenda ikawa ndo jibu la kutibu na kuangamiza ugonjwa hatari wa Ebola.

1 comment:

Channel Berita Misteri, Konspirasi dan Sejarah said...

Unique products please log on to http://selbuypay.blogspot.com