Thursday, September 11, 2014

Marekani kufanya mashambuli nchini Syria zidi ya ISI.

Boko Haram yateka mji mzima.

Maiduguri, Nigeria - 11/09/2014. Kundi linalo pingana na sheria za serikali ya Nigeria la Boko Haram limewaweka wakazi wa mji Maiduri roho zao juu kwa kutangaza kuwa mji huo upo chini ya utawala wao.

Kwa mujibu wa habari kutoka kwa wakazi wa mji huo na kuthibitishwa na kundi la Boko zinasema "kundi la Boko Haram, lipo kati ya km 40 kwa 50 kila upande wa mji wa Maiduguri,  na hivyo wamefanikiwa kuuzingira mji wa Maiduguri nawanaweza fanya mashambulizi kutoka kila upande wa mji huo wakati wowote."

Hata hivyo kufuatia tangazo hilo la kundi la Boko Haram, serikali ya Nigeria imekataa kuongelea suala hilo.

Kundi la Boko Haram limekuwa likisumbua na kutibua amani nchini Nigeria kwa kutaka wanachi wa nchi hiyo kufuata sheria za dini ya Kiislaam  na wakikataa wamekuwa wakiuwawa au kuteswa.

Vile vile kundi hilo limekuwa likiwakamata watu kwa nguvu  na kuwaficha na pia kundi hilo katikati ya mwaka huu  lilishutumiwa na jamii ya kimataifa baada ya kuwateka wanafunzi wa kike wapatao 200  siku ya 29/Juni/2014, na ambapo mpaka leo wanafunzi hao hawajulikani walipo, japo kuliwepo haadi za kimataifa ya kuwa wataokolewa muda siyo mrefu tangu wa wanafunzi hao wa kike watekwe.

Ni miaka 13 tangu mashambulizi ya Septemba 11/2001.

New York,  Marekani - 11/09/2014. Wanachi wa Marekani leo wamefanya maombi na sara kwa kuwakumbuka mamia ya wata walio umia na kufariki dunia baada ya mashambulizi ya kigaidi kufanywa  nchini humo miaka 13 iliyo pita.


Mashambulizi hayo ambayo yalifanyika mwaka 11/09/2001 na kundi la kigaidi la Al Qaeda na kusababisha upotevu wa maisha, ajali na uharibifu wa mali, yamefanyiwa kumbukumbu nchini kote.
Huku rais Baraka Obama akiwa mongozi mwa Wamarekani walio omboleza na kusari katika kukumbuka siku hiyo  ya Septemba 11 ambapo   majina ya wale wote walipoteza maisha kutokana na mashambulizi hayo yalisomwa kwa kuwakumbuka.
Hii ndiyo majengo ya Manhatani yanavyo onekaa kabla ya mashambulizi.

Kufuatia mashambulizi hayo yanayo julikana kama Septemba 11, serikali ya Marekani ilitangaza vita zidi ya ugaidi wa kila namna na kuanza kupambana na kundi la Al Qaeda  na washiriki wake na kufanikiwa kumuua kiongozi wa kundi la Al Qaeda,  Osama bin Laden, tarehe  2/05/2011, ambapo alikukuwa mafichoni nchini Pakistan, na mpaka sasa vita zidi ya ugaidi bado inaendelezwa duniani kote na Marekani ikiwa kinarani.


Marekani kufanya mashambuli nchini Syria zidi ya ISI.

Washington, Marekani - 11/09/2014. Rais wa Marekani ametangaza mkakati mpya wa kupambana na kundi la ISI na kuliangamiza bila kuacha kinvuli.

Akilihutubia taifa rais Baraka Obama alisema " nia kubwa hasa ni kuahakikisha kuwa kundi la ISI linapotea na kutokuwepo, na hivyo kila njia itatumika ili azimio hili lifikiwe na hatutasita kuwafanya mashambulizi mahali popote walipo ISI ."

Katika hotuba hiyo, rais Obama aliongea kuwa serikali yake itatoa  wanajeshi wasio pungua 500 ambao watahusikia katika masuala ya ufundishaji kwenye jeshi la Irak,  jeshi la Wakurdi na wapinzani wa serikali ya Syria  ili kuweza kupamana na na kundi la ISI lenye mizizi yake nchini Irak  na hivyo kuliomba bunge la Kongresi la Marekani kukubaliana naye kwa kuunga mkono serikali yake katika mpango wa kuwapa  kutaka kutoa mafunzo ya kijeshi.

Kufuatia hotuba hiyo, Marekani itakuwa na uwezo wa kufanya mashabulizi nchini Syria, ambapo pia kundi la ISI limekuwa likipiga kambi zake katika kutimiza azma yake ya kukuza kundi hilo la ISI.

Hata hivyo serikali ya Syria imeonya  kuwa "kitendo cha kufanya mashambulizi nchini Syria kwa kusingizio cha  kufanya mashambulizi zidi ya kundi la ISI,  halitakubalika na itakuwa ni kitendo cha kuvunja sheria za kimataifa." Alisema waziri wa mambo ya maridhiano na mapatano wa  Syria  Ali Haidar.

Akiongezea Haidari alisema " Syria imeshatangaza kuwa ipo tayari kushirikaiana na jumuiya ya kimataifa katika kupambana na kundi la ISI, na haitakuwa jambo la busara kufanya mashambulizi ndani ya Syria kwa kisingizio cha kuwashambulia wapiganaji wa ISI."

Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi, Alexander Lukashevich, akizungumzia kuhusu uamuzi wa Marekani kuamua kufanya mashambulizi kwenye makazi na vilinge vya wapinzani walioko chini Syria  alisema "ikiwa kitendo hicho kitafanyaka, basi kitakuwa ni kitendo cha utumiaji wa nguvu kinyume cha sheria na itakuwa vyema kushirikiana na serikali ya Syria kabla ya kufaya mashambulizi nchini humo."

Marekani imekuwa ikikuwa ikifanya kila njia ili kupambana na kundi la ISI, wakati huo huo imekuwa ikitaka utawala wa rais wa Syria Bashar al Bashir utolewe.

No comments: