Leo ni siku ya Waingereza wasimama njia panda.
Kura hizo ambazo zimeaanza kupigwa leo hasubuhi, huku wanasiasa wa pande zote, wanao unga mkono kujitenga na wale wanao pinga kujitenga, watakuwa wanasubiria kuona kama kampeni walizo fanya zimeleta matokeo waliyo tarajia.
Matokeo ya kura hizo yatangazwa siku ya Ijumaa 19/09/2014.
Ikiwa wananchi wa Scotland watapiga kura kujitenga, kutavunja muunganao ulidumu miaka 307, jambo ambalo litaleta mabadiriko makubwa ya kisiasa, kiuchumi,kijamii na pia kiutawala wa kifalme.
Rais wa Ukraine aililia Marekani kimsaada.
Washington, Marekani - 18/09/2014. Rais wa Ukraine, ameitaka Marekani kuipatia nchi yake siraha na vifaa vya kivita ili serikali yake iweze kuzitumia kuleta amani Mashariki mwa Ukraine.
Akihutubia bunge la Kongresi la Marekani, rais Petro Poroshenko alisema "Blangeti na vifaa vya kuangazia usiku wa giza ni muhimu, lakini hata hivyo blanketi haziwezi kusaidia kushinda vita na kuleta amani, hivyo tunaomba mtupe vifaa vya kivita ambavyo vitasaidia kuleta amani."
Akipigiwa makofi na wabunge wa Kongresi, rais Poroshenko aliongezea "Naiomba Marekani kutupatia msaada ya kiulinzi ambao utaambatana na ushirikiano wa jumuhia ya NATO, kwa Ukraine haitaweza kusimama peke yake katika mapambano haya."
Vile vile katika hotuba yake, rais Porocshenko, aliitupia lawama Urusi kwa kuhusika katika kuvuruga amani nchini Ukraine kwa kuwaunga mkono wapinzani wa serikali yake.
Na pia rais Poroshenko alifananisha hali iliyopo nchini Ukraine ni sawa na ile iliyotokea Georgia, na hivyo Marekani ni muhimu kutoruhusu hali kama hiyo kutokea tena.
No comments:
Post a Comment