Wednesday, September 24, 2014

Viongozi wa dunia waambiawa amani huja kwa gharama.

Viongozi wa dunia waambiawa amani huja kwa gharama . 
  
New York, Marekani 24/09/2014. Rais wa Wamarekani, amehutubia mkutano wa viongozi na wakuu wa nchi walio hudhuria katika kikao cha 69 cha umoja wamataifa ambacho kimeanza rasmi wiki hii.
 
Akihutubia rais Baraka Obama alisema " dunia inatakiwa kushirikiana katika kuleta amani na kuilinda, kwani vita vya kupitia mlango wa nyuma vinavyo endelea havita leta suruhu kwa kila upande."
 
"Na inatakiwa kutumia nguvu za kila namna ili kuweza kushinda na kuleta amani, na wakati mwingine  amani inakuja baada ya gharama ya kivita kuwepo."
 
"Inabidi sheria za kimataifa zifuatwe ili amani iwepo, kwani vita vya imani za kidini ndiyo chanzo cha matatizo yote  vita."
 
 "Hivyo inatakiwa ushirikiano wa kweli ili kupata ufumbuzi kwanini imani za kidini zinaleta vita, na mfano halisi ni kati ya Shia na Suni nchini Irak."
 
Rais Obama, alizungumza kuwa Marekani itakuwa mshiriki mkubwa katika kutetea demokrasi na amani popote duniani, na haitaona haya kufanya hivyo, "kwani huo ndiyo msingi uliyo ijenga na ambao unaendelea kuijenga Marekani hadi sasa."
 
"Tunamatatizo yetu kama nchi nyingine, hii nikuonyesha kuwa, licha ya kuwa na matatizo kama nchi, lakini hatuachi kuwa mstari wa mbele katika kutetea demokrasi nza haki za binadamu ndani na nje ya nchi, kwa kupinga ukandamizaji na ubaguzi wa kila namna  na huu ndiyo msimamo wa Marekani"
 
Pia katika hotuba yake, rais Obama, aliilaumu Urusi kwa kuwa muhusika mkuu katika utibuaji wa amani nchini Ukraini, na vile vile akusita kuzishambulia nchi ambazo zinasaidia makundi ya ISI na washiriki wake kifedha na kuzitaka kuacha kufanya hivyo japo akuzitaja majina.
 
Akisitiza rais Obama, alinikuhuu maneno ya kitabu Kitakatifu kwa kuseme "mtendee mema mwenzio kama unavyo taka kutendewa" na kusema wale wanaofanya mabaya wanakwenda kinyume na maagizo ya Mungu.
 
Kwanye hotuba yake Obama alisisitiza pia ni muhimu kwa serikali za nchi zote kupambana na elimu ya itikadi kali, ambayo inaleta mvurugo wa amani, na hata kama ina tolewa na "Wakristo, Wayahudi, Waislaam au Waumini wa dini yoyote." kwani kwa kuachia hii itikadi basi jamii nzima itaaathirika na matokeo yake yanaonekana.
 
Mkutano  wa 69 wa umoja wa mataifa unawakutanisha viongozi wapatao 140 , ambao wanatarajiwa  kuzungumzia na kujadili masuala ya kuongezeka na kukua kwa makundi ya itikadi kali duniani, na jinsi ya kuyadhibiti na pia mbinu za kupambana na magonjwa hatari na hasa ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa tishio kwa jamii ya kimataifa.
 
Bwana matata aliyekuwa mwiba kwa Uingereza aachiwa huru. 
 



Amman, Jordan - 24/09/2014. Mahakama ya jijini Jordani, imemuachia huru mtuhumiwa aliye kuwa akishitakiwa kwa kupanga mauaji ya watalii wa raia wa Kiizrael,  Marekani  na pia  raia wa Jordani wakati wa sikuku ya kuanza karne mpya mwaka 2000 katika jiji la Amman.

Abu Qatada, ambaye alikuwa nchi Uingereza kama mkimbizi na baadaye kuwa mpinzani na mkosoaji wa serikali ya Uingereza na siasa zake za nje  kutokana na msimamo wake wa itikadi kali, jambo ambalo lilisababisha asafirishwe kurudi kwao Jordan na kukumbana na   mashitaka yaliyo kuwa ya kimkabili, na hatimaye  mahakama jijini Jordani imemwachia huru baada ya kukumkuta hana hatia.

Akiongea baada ya kuachiwa huru waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza  Thereza May amesema " Abu Qatada hataruhusiwa kurudi Uingereza, kwani alikuwa mtu hatari katika jamii ya Kiingereza na ni raia wa Jordan hapa alikuwa amepewa hifadhi ya kikimbizi tu."

Abu Qatada au kwa jina jingine Omar Othman alishutumiwa kwa kuhusika kwa njia moja au nyingine na kundi la Al Qaeda, na pia kuhusika katika kufundisha itikadi kali za kidini, na vile vile kuwashawishi vijana wa Kiingereza kujiunga na kundi la Al Qaeda na kusadikiwa kuwa ni kiongozi wa kundi hilo nchini Uingereza na kuwa mwiba kwa wanasiasa na serikali nzima.

Naye Abu Qatada akiongea baada ya kuachiwa alisema " Nilipewa nafasi ya kujitete na ukweli umeonoekana kuwa sikuwa na makosa, na yote yaliyozungumzwa zidi yangu yalikuwa ya kuzushwa kisiasa."

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Qatada kuachiwa huru, baada ya ya kesi aliyokuwa akishutumiwa yakuwa alikuwa na mpango wa kushambulia shule ya Kimarekani iliyopo nchini Jordani kutupiliwa mbali na Mahakam kwa kukosekana kwa ushahidi.

Mwaka 2000, mahakama ya jijini Jordani,ilimuhukumu Abu Qatada kwenda jela miaka 15, wakati huo alipo kuwa akiishi ukimbizini nchini Uingereza, baada ya kukubaliwa kuishi nchini huko kama mkimbizi mwaka 1994.







No comments: