Friday, September 19, 2014

Wascotland waamua kuendelea na Muungano hauheni kwa waziri mkuu David Cameron.



Wascotland waamua kuendelea na Muungano kuwa hauheni kwa waziri mkuu David Cameron.
 
Glasgow, Uingereza - 19/09/2014. Wascotland wame amua kuendelea kuwa sehemu ya muungano wa Uingereza, baada ya matokeo ya kura kutoa jibu lililo kuwa likisubiliwa..
 
Majibu hayo yalitolewa baada ya kura kupigwa kujua nini wananchi wanataka kuhusu muungano, na kura nyingi zilitoa majibu ya kuwa kuendelea kuwa kwenye muungano na tofauti na wale waliopiga kura kujitoa.
 
Akiongea mara baada ya matokeo ya kura, waziri mkuu wa Scotland Alex Salmond na ambaye alikuwa kinara katika kuongoza kampeni ya kujitenga na muungano alisema " Wascotland wameamua kwa wingi  kwa sasa kuendelea kuwa katika muungano, hivyo naomba tushirikiane  na kuwa pamoja katika kuendelea kuijenga Scotland."
 
"Kilicho baki tungoje nini kitafanyika, kama kambi ya kuunga mkono muungano itatekeleza iliyo ahaidi wakati wa kampeni zao."Aliongezea waziri mkuu Solmond.
 
Naye waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron akihutubia taifa baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa alisema
 " Ni jambo la kujivunia kuwa Wascotland wamekubali kuendelea kuwa sehemu ya muungano wa Uingereza, na napenda kuwahakikishia kuwa yote tuliyo haidi yatatekelezwa na hii siyo tu kwa Scotland, bali pia kwa Wales, England na Irelandi ya Kaskazini."
 
Kufuatiwa matokeo ya kura za Scotland za kuunga mkono kuendelea kuwa sehemu ya muungano wa Uingereza, mabadiriko makubwa ya kiutawala na kisiasa yana tarajiwa kutokea, kwani nchi zilizomo kwenye muungano wa Uingereza ambazo ni Wales, England na Ireland ya Kaskazini nazo zimetaka zipewe haki sawa kama Scotland.
 
Jambo ambalo serikali ya waziri David Cameron itakuwa na wakati mgumu katika kukamilisha matakwa hao.
 
Hata hivyo wataalamu wa siasa wameeleza kuwa mmatokeo ya kura, yamemsaidia waziri mkuu David Cameron, kwani kama yangekwenda kinyume na matarajio ya serikali yake, basi angekuwa na wakati mgumu kioungozi na historia ya Uingereza inge mnata kuwa David Cameron kama waziri mkuu alishindwa kuulinda muungano.
 
Afrika kuwa na kizazi zaidi kuliko mabara mengine.
 
Washington, Marekani - 19/09/2014. Dunia itakuwa na ongezeko la wingi wa atu ifikapo mwaka 2100, na asilimia kubwa la ongezeko hilo litakuwa katika bara la Afrika.
 
Adria Aftery, ambaye ni mtaalamu wa mahesabu ya ongezeko la watu kutoka chuo kikuu cha Washington alisema " kunauwezekano mkubwa wa ongezeko la watu ifikapo 2100, hasa katika bara la Afrika kwa asilimia 80% kutoka watu billion 3.5 na kuwa na ongezeko la 5.1."
 
"Na hivyo kufikia mwaka 2100 ongezeko la watu litakuwa mara nne zaidi kutoka billioni 1 na kufikia billion 4." Alisisitiza  Profesa Adrian Raftery.
 
"Hadi kufikia sasa idadi ya watu duniani imekuwa ikiongezeka kwa asilimia 1.14 kwa mwaka na hili niongezeko mara mbili katika kipindi cha miaka 40 iliyopita toka mwaka 1959 hadi 1999 kutoka billion 3 hadi kufikia billioni 6." aliongezea Profesa Raftery.
 
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa watafiti wa ongezeko la watu duniani, ongezeko kubwa la watu limekuwa kubwa katika bara la Asia, ambapo nchini kama India na China zimekuwa na ongezeko la watu kitaifa.
 
Na katika bara la Afrika, Nigeria imekuwa naongezeko kubwa kitaifa na kukadiriwa huenda nchi hiyo ikawa ya tatu dunia,  itakapo fika katikati ya karne ya 21 na kupita  nchi zilizopo katika mabara ya Amerika kwa ujumla.
 
Julian Assange aichimba na kuiweka wazi Google.
 
London, Uingereza - 19/09/2014. Mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange, ameendelea kufumbua siri, kwa kusemakuwa kampuni mama ya kimmtandao ya Google ni mshiriki mkubwa katika kutoa siri na habari za watu kwa serikali.

Akiongea Julian Assange alisema "Google inafanya kazi pamoja na kitengo cha masuala ya usalama cha GCHQ cha Uingereza  na NSA cha Marekani, na inapata kipato chake kwa asilimia 80%  kwa kufanya kazi ya ushushu kwa kukusanya na kuzigawa habari za watu na shughuli zao za kibinafsi kwa mashirika hayo."

"Na Google ilipata mkataba wa kufanya kazi hiyo mwaka 2002." aliongezea Assange.

Julian Assange, ambaye kwa sasa anishi ukimbizini katika ofisi za kibalozi za nchi ya Ekwado zilizopo nchini Uingereza, amekuwa akisubiriwa nje ya jengo hilo na polisi wa Uingereza,  ili wamkamate na kumpeleka nchini Swiden,  ambapo anatakiwa kujibu mashitaka ya kuhusika na maingiliano bila hiyari na wana dada wawili wakati alipo kuwa nchini Swiden.

No comments: