Hatimaye ndoto ya kocha Alex Ferguson ya timia,"Man - United Bingwa wa Ulaya 2008-9".





Ushindi huu,ulipatikana baaday ya dakika 90 kumalizika kwa goli 1 kwa 1, na hata dakika za nyongeza kutokuzalizasha goli, na hivyo kuamuliwa kwa kupiga gozi la ng'ombe mbele ya matuta kumi na mbili, na kamptaini wa timu ya Chelsea FC , John Terry, kupeperusha gozi la mwisho la tano,na hatimayake kwenda kwenye matuta ya ziada na ndipo,Nikolaus Arnelka mchezaji huyo, gozi lake kushindwa kuvuka tuta la manchester na kuishia mikononi mwa golikipa namba moja wa Holland na Manchester, Edwin van der Sar.Na ndoto ya Chelsea FC kuondoka mikono mitupu ndini ya uwanja wa Luzhniki.
Timu ya Man United ilibebe kombe la ubingwa wa Ulaya chini ya kocha Alex Ferguson mwaka, 1998-1999, na sasa 2008 - 2009.
Picha hapo juu anaonekan kocha mkuu wa Man United, bwana Alex Ferguson,akiwapungia wapenzi wa timu yake baada ya kunyakua kombe la ligi ya Uingereza hivi karibuni.
Picha ya pili anaonekana kocha Alex Ferguson, akinyanyua kombe la ubingwa wa Ulaya kwa mara ya pili.
Picha ya tatu wanaonekana wachezaji wa Man United, wakishangilia ubingwa wa kombe la Ulaya 2008-9 ndani ya jiji la Moscow.
Picha ya nne, ni kombe ambalo huwa linagombaniwa kila mwaka, msimu wa 2008-9 limebebwa na Man United.
Picha ya tano,anaonekana bila matumaini golikipa wa wa Man United, Edwin van der Sar, akiangalia mpira bila matumaini uliopigwa na na John Terry, lakini uligonga mlingiti wa goli na kuikosesha Chelsea FC ubingwa wa Ulaya msimi wa 2008-9.
Picha ya sita anaonekana, mchezaji na kaptain John Terry, akiwa amekaa chini,kwa uchungu uku amewshikilia mguu wake wa kushoto ambao uliteleza na kunfanya apeperushe penati ya ushindi dhidi ya timu ya Man United.
Picha ya mwisho, anaonekana mchezaji wa siku nyingi wa timu ya Man United Poul School, akiwa ameinama mkao wa kondoo anaye taka kupigana na kondoo mwenzake, lakini siyo hivyo bali inaonyesha ni jinsi gani mechi ya fainali kati ya timu yake Man United na Chelsea ilivyoi kuwa ngumu, kwana kukaa kwa kwa mtindo huu, siyo kupenda bali inaonyesha yakuwa ubingwa huu wa Ulaya wameufanyia kazi kubwa na hata damu zilimwagika.
Poul School aliumia baada ya kugongana na mcheza wa Chelsea na wa timu ya taifa ya Ufaransa, Claude Makelele wakati walipo ruka juu kuwania mpira.
Wapiganaji Tuereg na wanajeshi wa serilika wapigana nchini Mali " Tuereg kudai madaraka".


Mapambano hayo amboyo yapo kaskazini mashariki mwa nchi ya Mali, yalipoteza maisha ya wanajeshi 15 na wapiganaji 17.
Wapiganaji hawa wa kundi la Tuareg, alivamia moja ya kitua cha jeshi kilichopo kaskazinimashariki mwa nchi ya Mali na ndipo mapigano yalipo anza kati ya kundi la Taureg na jeshi la serikali.
Kundi hili ambalo linadai kutaka kujitawala kimadaraka katika eneo lao, limekuwa likipigana na jeshi kwa kipindi kilefu sasa
Picha hapo juu, nanaonekana rais wa Mali bwana Amadou Toure, ambaye anaonekana akikagua shamba moja nchini mali kuangali hali ya ukame ilivyo asili kilimo nchini humo.
Chini ni picha za wapiganaji wa Tuereg, ambao wanapingana na serikali ya Mali inayo ongozwa na rais Amadour Toure.
Jeshi kupungunzwa hivi karibuni kutoka mstari wa mbele nchini Irak" Jemedari Mkuu"


Jemedar huyo,bwana David Petraeus, alisema haya mbele ya kamati ya huduma za jeshi, ingawaje hakutaja yakuwa ni idadi ya wanajeshi wangapi watapunguzwa kutoka mstari wa mbele nchini Irak.
Picha hapo juu, anaonekana Jemedari, David Petraeus, akiwa na wanajeshi wapiganaji nchini Irak hivi karibuni.
Chini ni picha ya Jemedari, David Petraeus, akinyanyuka baada ya kumaliza kuongea na kamati jeshi la Ulinzi la Amerika.
Je mazungumzo kati ya Israel na Siria, ni chanzo cha amani mashariki ya kati?



Mazungumzo haya ambayo yamechukua karibu siku tatu, yamekuwa yakifanyika, chini ya mpatanishi kutoka Uturuki bwana Ali Babacan , ambaye ni waziri wa mambo ya nchi za nje ya Uturuki.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa hali ya kiusalama na kisiasa kwenye maeneo ya mashariki ya kati, wamesema ya kuwa huu ni mwanzo, ijapo kuwa mazungumzo hay yalifanyika kupitia ngazi za chini za serikali hizi.
Hata hivyo, msimamizi wa mapatano haya bwana , Ali Babacan, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki, alisema ya kuwa mazungumzo haya ni chanzo cha kuleta matumaini ya amani kwenye maeneo haya ya mashariki ya kati.
Picha ya hapo juu ni picha ya rais wa Siria, bwana Bashar Assad.
Picha ya kati ni picha ya msimamizi wa mazungumzo ya bwana Ali Babacan, ambaye ni msimamizi wa mapatano kati ya Siria na Israel.
No comments:
Post a Comment