Thursday, May 1, 2008

Msanii apigwa marufuku kwa kupiga nyimbo za kupinga ushoga.

Nadal awa moto wa kuotea mbali, Roger Feder,hakuamini macho yake.

Monaco, Monte, Monaco - Mchezaji maarufu wa mchezo wa tenis na anaye shuikila numbea mbili duniani katika mchezo hu kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal, amejiongezea tena donge nono na kikombe kinginem baada ya kumshinda mchezaji namba moja wa machezo huo duniani Roger Feder kwa point 7-5, 7 -5, katika fainali iliyochezwqa hivi karibuni mjini Monte Carlo.
Kocha wa mchezaji Rafael Nadal, alisema ya kuwa ushindi huu ni changamoto kwa mchezaji wake, kwa kujiandaa na mashindano ya Wimbleydon yatakayo anza hivi karibuni.
Wakati huo huo, waandalizi wa mchezo wa tenis, nchini Uingereza, wa mashindano ya Wimbleydon wametangaza rasmi ya kuwa bingwa wa mashindano haya watapata donge nono zaidi, kwani wameongeza ongezeko la asilimia 4.7%.
Hivyo washindi wa mashindayo hayo, ambayo yapo katika maandalizi watapata kiasi cha paundi 750,00, sawa na Euro 1.49 mil.
Msanii apigwa marufuku kwa kupiga nyimbo za kupinga ushoga.
Guyana, Georgetown - Serikali ya Guyana imempiga marufuku mwanamuziki wa maadhi ya miziki wa regge kutoka Jamaika, Bounty Killer kupiga musiki wake nchini humo hivi karibuni.
Akitangaza uamuzi huo, waziri wa mambo ya ndani ya Guyana, bwana Clement Rohee, alisema yakuwa, serikali imemkatalia msani huyo, kwani itikadi yake ya kupinga ushoga ni kinyume na haki za binadamu na uamuzi wakuwatenga watu kijinsia kwa kutumia nyimbo zake ni kinyume na sheria na anahatarisha usalama wa badhazi ya watu.
Na hii siyo mara ya kwanza kwa serikali ya Guyana kupiga marufuku kuingia baadhi ya wasanii kutoka Jamaika, kwani hata sikun zanyuma ilimpiga marufuku masanii ajulikanaye kwa jina Mavado.
Pichani hapo juu anaonekan msanii,Bounty Killer akiwa anawaangali wapenzi wa muziki wake kwa macho, kama ujumbe wameu pata.
Picha nyingine anaonekana akilfanya vitu vyake jukwaani hivi karibuni katika moja ya maonyesho yake.
Karata nyingine, Tarika Aziz afikishwa kizimbani kujibu mashitaka.
Irak, Baghdad - Aliyekuwa mmoja wa viongozi na msemaji mkuu wa kutete serikali ya hayati rais Saddam Hussein, bwana Tarik Aziz, amefikishwa mahakamni hivi karibuni kujibu mashitaka ya kuwa alihusika kwa njia moja katika mauaji ya wafanyabiashara wapatao 42, waliopanadisha bei vyakula, wakati Irak ilipo wekewa vikwazao vya kiuchumi na serikali za Magharibi miaka 15
iliyo pita.
Kesi hiyi imeanza 29/04 mjini Baghdad.
Dunia itamkumbuka bwana Tarik Aziz, kuwa mtu wakaribu saana wa aliyekuwa rais wa Irak, marehemu, Saddama Hussein wakati wa utawalawake, bwana Tarik Aziz kwa jina jingine alijulikana kama Alikuwa Mikhail Yuhanna, ni mmoja ya mawaziri ambao walikuwa waumini wa dini ya Kikristu.
Pichani anaonekana bwana Tarik Aziz, akiwa amevalia nguo za munga'nda, sare ya jela, tangu alipowekwa kizuizini na jeshi la Amerika mjini Baghdad.
Picha ya chini anaonekana bwana Mikhail Yuhanna au kwa jina Tarik aziz, enzi hizo alipo kuwa ofisini akisikiliza nini anaelezwa na mmoja wa washauri wake.
Irak bado kitendawili miaka ya zidi kujiongeza, lawama kila kukicha.
USA, Washingtone - Leo ni siku amabyo rais wa Amerika bwana George Bush , alipo tangaza ya kuwa shughuli zote za kivita nchini Irak zimekwisha.
Rais George Bush, aliyaongea haya, mbele ya meli ya kivita ijulikanayo kama Abraham Linchon, huku nyuma kukiwa na tangazo kubwa la kuonyasha ya kuwa kazi imetimizwa/timilika. au kwa kingereza Mission Accompilish.
Lakini hata hivi, tangazo hilo limekuwa kama kitendawili, kwenye vichwa vya wanasiasa na wataalamu wa mambo ya kijamii na maendeleo, hivyo kumkosoa kwa kila hali rais George Bush kila kukicha.
Nimiaka mitano sasa tangu vita dhidi ya Irak vianze na mpaka sasa hakuna jibu kamili lini vita hivi vita kwisha rasmi, alisema mmoja wa wanawakitaaluma kuhusu maendeleo ya kijamii.
Pichani nhapo juu wanaonekana baadhi ya wananchi amabo wanapinga kuendelea kwa vita nchini Irak wakiwa wameshilia kitambala kikubwa chenye maandishi yasemayo kazi imetimizwa/imetimilika, kwadhiaka wakati wa maandamano na mmoja ya wnaandamanaji hawa akiandika idadi ya wanajeshi ambao wamepoteza maisha yao kwenye vita hivi.
Chini anaonekana rais wa Amerika bwana George Bush, akiashiria kwa kidole gumba wakati alaipo tangaza rasmi yakuwa vita vya Iraki vimekwisha.
Mgogoro wa Mashariki ya kati, bado joto ya jiwe kwa kila mwana siasa.
Mashariki ya kati, Gaza - Mgogoro unao endelea kati ya, Wapalestina na Waisrael unazidi kuleta utata, hivi karibuni jeshi la Israel limeshambulia maeneo ya wakazi wa Palestina na kusababisha vifo ya watu wasiopungua watano ambao ni jamaa wa famila moja.
Lakini hata hivyo, msemaji wa jeshi la Israel, alisema walishambulia eno hilo baada ya wapiganaji wa jeshi la Hamas kuanza mashambuli dhidi ya jeshi la Israel.
Kutokana na mgogoro huo imekuwa nivigumu hata wakazi wanao ishi karibu na mpaka unao tenganisha Israel na Palestina kuwa na wakati mgumu , hasa kwa ndugu kutembeleana. Picha hapo juu ni picha ya mmoja ya wakazi wanao ishi karibu na mpaka wa Israel akionyesha ishara ya kuomba aruhusiwe aingie nchi Israel
Picha nyingine ya chini wanaonekana baadhi ya wakazi wa Kipalesstina wa kiombea dua miili ya watu walio fariki dunia baada ya Israel kushambuali kufanya shambilizi hivi karibini.
Mmoja wa viongozi wa jeshi linalo pigana na jeshi la serikali auwawa.
Somali, Mogadishu - Jeshi la Amerika , limesema yakuwa limemua, aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Shabaab ambalo limekuwa likipingana na serikali ya Somalia inayo saidiwa serikali ya Ethiopia.
Kiongozi huyo anayejulikana kama Aden Hashi Eyrow,alikuwa ndiyo nguzo moja ya kikundi hiki cha UIC (Union of Islamic Courts) na kundi la Al Shabaab.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo, amesema ya kuwa kuuwawa kwa bwana Eden Hashi Eyrow, siyo mwisho wa mapambano bado yataendelea na wale wote walio husika na mauaji ya kiongozi huyu wajihadhali.
Pichani anaonekana mmoja wa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab , akiwa ameshikilia mtutu tayari kupigana na wanajeshi wa serikali.

No comments: