Tuesday, May 6, 2008

China na Watibet wakubaliana kimsingi, wasema wasemaji wa Dali Lama.

Pete ya ndoa ya harusi yaghalimu madola, penzi limefika palipo.

Nassaua City, Bahama - Mwana mziki maarufu duniani wa mtindo wa R&B, bi Miarah Kerry, amefunga pingu za maisha na mwanamziki, mcheza sinema na T show,bwana Nick Cannon.
Harusi hii imefanyika hivi karibuni Bahama, baada ya hwa wapendanao kuchumbiana kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Pete ya harusi ya bi Mariah Kerry, aliyo vaa wakati wa sherehe hizo bi Mariah ilighalimu kiasi cha dola 2,5 million .
Sherehe hiyo iliudhuliwa na watu wakaribi saana wa bi Mariah na bwana Cannon, ni pamoja na mwanamuziki Da Brat
Picha hapo juu,anaonekana bi,Mariah Kerry akiwa kazini kimuziki kutumbwiza wapenzi wa muziki wake.
Picha ya chini anaonekana bwana, Nick Cannon akiwa anaonyesha misuli ambayo imemchanganya bi, Mariah.
Hapo juu ni picha ya bi Maria, akiwa ame pozi huku uzuri wake ukuionekana.
Chini picha ya mwisho wanaonekana Mariah na Nick wakiashilia ya kuwa huo ulikuwa mwanzo wao tu sasa wamethibitisha ya kuwa roho zimeridhiana.
China na Watibet wakubaliana kimsingi,wasema wasemaji wa Dalai Lama.
Beijing, China - Mazungumzo kati ya serikali ya China na Wawakilishi wa Jimbo la Tibet, linalo ongozwa na Kiongozi wa Kidini Dalai Lama, yameisha katika hawamu ya kwanza.
Akisema hayo walipo wasili kwenye kiwanja cha ndege cha Hong Kong, msemaji wana mwakilishi wa Dalai Lama, kuwa mazumngumzo hayo yalikuwa ndio mwanzo wakutafuta ufumbuzi wa mgoggr wa Tibet, na hivyo kutakuwa namazungumzo mingine hapo baadaye, ijapo kuwa akueleza yatafanyika lini.
Mazungumzo haya yamekuja baada ya purukushani, maandamano na hata baadhi ya watu kupoteza maisha yao wakati wakupinga sera zote za China katika jimbo la Tibet.
China mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki ya 2008, hivyo mazungumzo haya yatasaidia kupunguza baadhi ya maoni yaliyo tolewa kuhusu serikali ya China dhidi ya jimbo la Tibet.
Juu ni bendera ya China, na serikali ya China inasema Tibet ni sehemu ya China.
Picha mbili tofauti hapo juu, anaonekana kiongozi wa Kidini, Dalai Lama, akiwa anaongoza maombi ya swala.
Rais wa Misri, atimiza miaka 80, makubaliono ya siasa bado mvutano.
Cairo, Misri - Rais wa Misri, Hussein Mubarak, ametimiza miaka 80, hivi karibuni huku hali ya kisiasa nchini humo ikiwa katika hali ya mvutano.
Rais Mubarak,ambaye aliingia madarakani baada ya kifo cha rais, Anwar Sadat, amekuwa madarakani tangu 1981, na kwa kipindi kisicho pungua miaka 27 amekuwa rais wanchi hiyo ya Misri hadi hivi sasa.
Na wakati huo hu polisi wa kulinda mpaka kati Misri na Israel, wamefyatua risasi na kuwauwa watu kadhaa, akiwepo kijana mmoja wa Kinageria, wakati walipo jaribu kuvuka mpaka na kuingia nchini Israel.
Picha hapo juu ni picha ya rais Hussein Mubaraka, ambaye ametawala kwa kipindi kisicho pungua miaka 27 nchini Misri.
Chini pi picha ya rais, Mubaraka akiongea na rais George Bush, mapema mwaka huu wakati rais Bush alipo tembelea Misri.
Chini wanaonekana polisi wa kuzuia fujo wakiwatimua waandamanaji kwa kutumi hewa ya kutoa machozi, na hapo anaonekana mwana mama anakimbia kwa nguvu zake zote kujiepusha na janga hili.
Hawakuweza kunishawishi kukiuka madaili yangu ya kazi, ili niwatumikie.
Khartumu, Sudani - Shirika la Utangazaji la Al Jazeera, ndugu pamoja na marafiki walishangilia baada ya kumwona mmoja ya wafanyakazi mwenzao bwana Sami Al Hajj, ambaye ameachiwa hivi karibuni kutoka jela ya Guantanamo Bay.
Akielezea , bwana Sami Al Hajj, alisema ya kuwa aliojiwa zaidi ya mara 130, kati ya haya 95 ni kuhusu kazi yangu, "Na walitaka mimi niwe shushu wao Amerika"Hivyo baadaye waliamua kumkamata mwandishi yoyote, ambaye atataka kuonye ukweli kuhusuhali halisi wakati vita Afganistani vilipoanza.
Hata hivyo msemaji, wa Jeshi la Amerika, alisema ya kuwa yote yaliyo ongelewa na bwana Sami al Hajj ni ya uongo na alijifanya mgojwa saana alipo wasili mjini Kartumu.
Picha hapo juu ni picha ya bwana Sami Al Hajj, alipo kutana na ndugu, jamaa na marafiki wakati alipo wasili mjini Kartumu nchni Sudani.
Bwana Sami al Hajj alieama"Na walizidi kunitaka niwatumikie nikiwa kama mwandishi wa habari, hata hivyo hawakuweza kunishwishi kukiuka maadili ya kazi yangu ya uandishi wa habari".
Kuwepo kwa mitambo yetu ni moja njia ya kukua kwa kundi letu "Hezbollah".
Beirut, Lebanoni - Serikali ya Lebanoni, imesema yakuwa itachukuwa hatua za kisheria dhidi ya kundi la Hezbollah,ambacho kinaongozwa na viongozi wa Kishia.
Akisema haya msemaji wa serikali ya Lebanoni, bwana Ghazi al Aridi, alisema haya karibuni ya kuwa kikundi cha Hezbollah, linakwenda kinyume, kwa kutumia kutumia mawasiliano amabyo yanamilikiwa na kundi hili la Hezbollah. Akiongezaa , alisema ya kuwa imefikia hadi kundi hili limeweka kamera katika kiwanja ndege, ambazo zimekuwa zikitumiwa na kundi hili kuangalia na kuchunguza nani anaingia na nani anatoka.
Hata hivyo msemaji wa Hezbollah, alisema ya kuwa wanavyombo ya mawasiliano na alikataa ya kuwa Hezbollah, hawatakubali kusikia serikili ya Lebanoni inasema nini. Hapo juu ni picha ya bwana Qassem(Kassim), ambaye alisema mitambo hii ni njia mija wapo ya kukua kwa kundi hili.
Picha chini ni ya bendera la kundi la Hezbollah ikipepea huku pembeni zinaonekana bendera za nchi ya Lebanoni zikipepea, wakati wanachama na wapenzi wa Hezbollah walipoandamana hivi karibuni.

Mpambano nchini Afghanistani bado, na rais anusurika na mashambuliza.
Washington, USA - Rais George Bush, amesema hivi karibuni ya kuwa hali ya Afghanistani bado haijafikia kiwango kizuri cha kimaendeleo.Lakini hata hivyo alisisitiza ya kuwa jumuia za kimataifa na majeshi yake yanafanya kila njia na hali itakua nzuri hapo baadaye.
Rais, George Bush, alisema haya baada ya wapiganaji wa Taliban, walipo shambulia gwaride ambalo liliudhuliwa na rais Hamid Karzai, na kusababisha vifo vya watu wasio pungua sita akiwemo mmoja wa wabunge wa serikali.
Picha hapo juu ni wanaonekana baadhi ya wakazi wa sehemu fulani nchini Afghanistani, wakiwa wamelizunguka gari la jeshi la kimataifa linalo ongozwa na Amerika.
Chini ni picha ya wanajeshi wa Afghanistani wakiwa wanakula kwata, tayari kuwa imara kulinda nchi.
Hapo juu anaonekana rais, Hamid Karzai, akiongea baada ya chambuli lililo fanywa wapiganaji wa Talibani
Moscow yazidi kuimarisha ngome zake mipakani.
Moscow,Urusi - Serikali ya mjini Moscow, imeongeza majeshi yake hivi karibuni karibu na mpaka wa nchi ya Georgia.
Kutokana na msemaji wa serikali ya Moscow,alisema ya kuwa kuwepo kwa jeshi hili ni kukamilisha na kuendeleza ile kazi ya kudumisha amani kufuatia mkataba ulipitishwa mwaka 1994.
Hata hivyo, msemaji wa serikali ya Georgia alisema ya kuwa, kitendo hiki cha serikali ya Moscow, ni kinyume cha sheria za kimataifa, na inahataisha usalama wa eneo zima.
Picha hapo juu wanaonekana wanajeshi wa Urusi wakiwa mbioni, kujiandaa na safari ya kuelekea mpakani na nchi ya Georgia.
Picha ya chini, inaonekana na ramani ya ianayo onyesha mpaka kati ya Georgia na Abkhazia .

No comments: