Monday, May 19, 2008

Wageni wakiona cha mtema kuni Afrika ya Kusini"Wamekuja kuchukua kazi zetu" Wadai wazawa.

Jela ya mkabili Willy Snipes," Sitarudia tena kosa kama hili" Snipes.

Florida, USA - Msanii maarufu na nyota ya kucheza sinema duniani, Willy Snipes, amehukumiwa kwenda jela hivi karibuni kwa muda wa miaka mitatu na mahakama ya Ocala, mjini Florida, kutokana na kosa la kukosa kulipa kodi ya mapato katika kipindi cha miaka ya 1999 hadi 2001.
Akitoa hukumu hii, jaji William Terrel Hodges, nimuhimu kutoa hukumu kama hii , kuonyesha ya kuwa siyo vizuri kutolipa kodi ya mapatato kwa serikali, na akaagiza ya kuwa maasifa wa jela atakayo tumikia kifungu wampe taarifa ni lini ataanza kutumikia kifungo chake.
Hata hivyo Willy Snipe, yupo nje kwa dhamana hadi hapo rufani yake itakapo sikilizwa tena. Willy Snipes, alisema alikuwa anasikitika sana kwa kosa hili na ya kuwa hatarudi tena kosa kama hili.
Hata hivyo, mwana sheria mtetezi wa Willy Snipes , alisema ya kuwa , mteja wake anadaiwa kiasi kisicho pungua US dollal 400,000, na kwa kesi hiyo hastahili kutumika kifungo cha jela.
Navilevile wanasheria huyo aliendelea kwa kuongeza ya kuwa kuna baadhi ya wasanii na wacheza sinema,mfano , Marc Anthony na Meya wa jiji la Washington Mario Barry waliachiwa kwa kosa la kukwepa kulipa kodi ya mapato , na vilevile mwana musiki, Willie Nelson, aliachiwa huru kwa kosa kama hilo lakutokulipa kodi ya mapato ya thamani ya US dollal 17 million.
Picha hapo juu anaonekana, Willy Snipes akiwa na mcheza sinema mwingine Ving Rhames, wakati wa kicheza sinema ijulikanayo kama Mirax's Undisputeed.
Picha ya kati anaonekana Willy Snipes, akiwapungia wapenzi wake walio kuja kusikiliza kesi yake, na kupewa hukumo ya kukaa jela miaka mitatu.
Picha ya mwisho, anaonekana, Willy Snipes, akiwa ameinama na kufikilia nini la kufanya hapo baadaye.
Hali hii ni kawaida nchini Somalia," Maisha halisi mjini Mogadishu".
Nairobi, Kenya - Mazungumzo kati ya wawakilishi wa serikali ya Somalia, kikundi kikubwa kinacho pingana na serikali ya Mogadishu na kinacho julikana kama Alliance for the Re liberation of Somali (ARS) yanaendela nchini Kenya, huku baadhi ya viongozi wa ARS, wakisema ya kuwa mazungumzo haya hayataleta ufumbuzi wowote.
Mmoja wa viongozi hawa, alisema, itakuwa ni vigumu kufika muafaka,hadi hapo wanajeshi wa Ethiopia watakapo angamizwa ama kujitoa wenyewe nchini Somali. Machafuko na mapigano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini , Somali yamechukua miaka mingi sasa zaidimya miongo miwili.
Pichani hapo juu ni picha ya mmoja ya wapiganaji wa jeshi la Serikali, akiburutwa mitaani na anaonekana mwana dada akipiga picha ya mpiganaji huyu, kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Picha chini pi picha ya moja ya magari ya jeshi la serikali na mshirika wake Ethiopia, likipiga doria mjini Mogadishu hivi karibuni.
Tbilisi na Moscow, hali ya uhusiano wa kijirani wao ni tete.
Moscow, Urusi - Serikali ya Urusi , imesema hivi karibuni imemkamata mmoja wa wapelelezi kutoka nchini Georgia, ambaye inasemekana anahusika na kuleta mtafaruku katika eneo hilo.
Kutokana na habari zilizo patikana kutoka kwa shirika la habari na wakala wake FSB , zimesema ya kuwa usalama wa taifa wa Urussi, wamemkamata raia mmoja wa Georgia, ambaye alikuwa akiishi kusini mwa Urusi kwenye jimbo la Checheyna, inadaiwa raia huyu alikuwa mmoja wa wapiganaji walio pata mavunzo ya kijeshi.
Hata hivvyo, serikali ya Georgia ilikanusha madai haya, na kudai madai haya ya Urusi ni ya kuleta huasama na Tbilisi
Tsvangirai asitisha safari ya kurudi nyumbani, "MDC ya dai kuna njama ya mauaji".
Harare, Zimbabwe - Chama (MDC) Movemet Democratic Change, kinacho ongozwa na Morgan Tsvagirai, kimedai yakuwa kimepata habari nyeti ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho, bwana, Tsvangarai maisha yake yapo hatarini pindipo atakapo rudi nchini Zimbabwe kuanza kampeni ya kugombania kinyang'anyiro cha urais dhidi ya rais wa sasa wa Zimbabwe , bwana Robert Mugabe.
Bwana Morgan Tsvangirai, alitakiwa kurudi siku ya jumamosi nchini Zimbabwe, lakini ilibidi asimamishe safari hiyo, baada ya chama chake MDC, kusema ya kuwa kuna njama za kutaka kumuua, kwa kutumia mashushu.
Bwana, Morgan Tsvangirai ambaye yupo nchin Afrika ya kusini kwa sasa,hakuweza kuhudhulia moja ya vikao vya kampeni ya uchaguzi unao fuata hivi karibuni.
Marudiano hayo ya duru la uchaguzi, yanatarajiwa kufanyaika mezi wa sita - juni 27
Pichani hapo ni picha ya rais wa sasa wa Zimbabwe, bwana Robert Mugabe, ambaye atagombea kwa mara nyingine kuiongoza Zimbabwe.
Picha ya chini, ni picha ya bwana Morgan Tsvangirai, ambaye alishinda duru ya kwanza ya uchaguzi, lakino hakufika kiwango kinachotakiwa kuwa raisi wa nchi hii Zimbabwe.
Viongozi wa wapiganaji wa JEM, wa Sudani wafukuzwa nchini Misri.
Kairo, Misri - Serikali ya Misri hivi karibuni, imewafukuza nchini humo viongozi wa chama cha upinzani wa chama JEM (Justice and Equality Movoment) cha Sudani Darfur.
Hata hivyo serikalai ya Misri haikutoa sababu gani zimewafanya wawa fukuze viongozi hawa na wapiganaji wa JEM
Viongozi hawa na wapiganaji bwana Ahmed Tugd , Ahmed Sharif na Mohmed Ali, walikamatwa hivi karibuni na kutakiwa kuondoka nchini humo.
Picha hapo juu, ni picha ya bendera ya Misri.
Wageni wakiona cha mtemakuni Afrika ya Kusini,"Wamekuja kuchukua kazi zetu" Wadai wazawa.
Johannesburg, Afrikia ya Kusini - Zaidi ya wahamiji wasio pungua 20, wamepoteza maisha yao hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini, kutokana vurugu na machafuko yanayo endelea kati ya wanchi wazawa wa Afrika ya Kusini na wageni walio amia.
Vurugu hizi zimeanza kutokana na mtazamo wa wazawa wa Afrika ya Kusini ya kuwa hawa wahamiaji wanakuja kuchukua kazi zao.
Watu ambao wamekubwa na mikasa hii, ni hasa wananchi wanaotokea nchi za
Zimbabwe,Mozambiki, Malawi, na Zambia.
Raia mmoja wa Malawi, alisema ya kuwa amepoteza mali zake zote, alizofanyia kazi kwa kipindi kirefu na sasa hana kitu tena, na hajui atafanya nini ili kuweza kumudu maisha yake ya baadaye, na akadai yakuwa wazawa hawa walikuwa wakisema hawa makwerekwere, lazima waondoke warudi kwao,alimalizia raia huyu wa Malawi.
Kutokana na mikasa hii, wahamiaji wengi, wamekuwa wa kikimbilia katika vituo vya polisi ili kuokoa maisha yao, na wengine kukimbia kwa wasamalia wema.
Pichani anaonekana mmoja wa wazawa wa Afrika ya Kusini, akiwa ameshikilia bakora, tayari kufanya vitu vyake kwa wageni, huku moto ukiwa unawaka kwenye taveni au ( kioski), na inasadikiwa ya kuwa taveni hii na mali zilizopo ni mali ya mmoja wa wageni hawa.
Mume wa marehemu Bhuto, afutiwa kesi na mahakama," Kesi haikuwa na ushaidi kamili"Hakimu.
Islmabad, Pakistan - Mahakama ya nchini Pakistan, imetupilia mbali kesi iliyokuwa inamkabili ya mwenyekiti wa chama PPP ( Pakistan People's Part) bwana Asif Ali Zardari.
Mwenyekiti huyu bwana, Asif Ali Zardari, alikuwa akikabiliwa na kesi ya kuhusika na uingizaji wa madawa ya kulevya au (Mihadarati).
Kesi hii ambayo imechukua zaidi ya miaka mingi, akisema haya, jaji Ejaz Hussain Awan, alisema yakuwa kesi hii akuwa na ushaidi kamili.
Pichani hapo juu, ni picha ya bwana Asif Ali Zardari, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni.

1 comment:

Sindbad said...

Kajumulo kazi nzuri sana lakini jitahidi kutumia kiswahili fasaha na pia tupe khabari zaidi za nyumbani na Afrika.
Kifupi nakupa shavu na kuifagilia kazi yako.