Barc'a wasema sasa basi kwa Frank Rijkaard, wataka bahati mpya, "Rais wa timu".


Rijkaard, ambaye alikuwa kucha wa timu hii ya FC Barcelona tangu mwaka 2003, nakuweza kurudisha jina la timu ya Barcelona duniani, kwa kuchuku ubingwa wa mashindano ya ligi ya Uispania (La Liga) na timu ya FC barcelona Kuwa bingwa wa mashindano ya vilabu vya Ulaya mwaka 2006.
Akisema haya, rais wa timu ya Barcelona , bwana Joan Laporta, alisema ya kuwa Rijkaard, ameiletea sifa timu yetu, lakini matokeo ya mwaka huu haya kuridhisha, hivyo uongozi wa FC Barcelona, unamshukuru sana na niwakati wake wakwenda kupumzika, tumpe nafasi kocha mwingine.
Kocha aliye teuliwa kuiongoza FC Barcelona ni aliye kua timu kaptain wa zamani wa timu hiyo,Pep Guardiola.
Frank Rijkaard alikuwa na mkataba wa kuwa kocha wa timu ya FC Barcelona hadi 2009.
Picha hapo juu anaonekan Frank akiwa anafanya mavitus enzi zake alipo kuwa akichezea timu ya AC Milan ya Itali.
Picha nyingine anaonekana Rijkaard, akiwa ana mpoza mchezaji nyota wa dunia Ronadinho, baada ya hali kuwa mbaya wakati walipo cheza moja ya mechi zao na kushindwa kushinda.
Frnk Rijkaard, anaonekana akitoka uwanjani kwa hasira baada ya timu ya kuendelea kutofanya vizuri katika moja ya mashindano ya la liga.
Hapo chini ni picha ya mwisho anaonekana, Rijkaard akiwa anajaribu kumyang'anya mpira Denis Bergkamp, wakati wa mchezo walipo cheza pamoja kwa ajili ya kuchangisha fedha.
Taifa teule latimiza miaka 60 tangu kuundwa, na wakati huo huo waziri mkuu kiti moto.



Kuanzishwa kwataifa la Kiizrael 1948, kulitokea baada ya Umoja wa Mataifa, kupiga kura mnamo mwaka 1947/29/11, li kuundwa taifa la hili, na matokeo ya kura ni kwamba kura zili pita kwa 33 kwa 13 na 10 hazikupigwa. Nakutokana na kura hii . ndipo kulipitishwa hazimio la kuanzishwa taifa la Waisrael,ambao kwa miaka mingi walikutwa na matatizo mbali mbali, na hasa lile la mauaji ya kutisha yaliyo tolea nchini, Ujerumani, Austria na Polandi,ambapo zaidi ya Waizrael millioni 6, waliuwawa, wakati wa utawala wa Aldoph Hitler, ambaye alikuwa kiongozi wa Ujerumani wakati huo.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Izrael, bwana Ehud Olmet, akisalimiana na watu walio kuja kusherekea siku ya kuanzishwa kwa taifa la Izrael mjini Jerusalem.
Picha ya pili wanaonekana, rais wa Israel bwana, Shimon Perez na waziri mkuu wa Izrael, bwana Ehud Olmet wakiingi kwenye ukumbi tayari kusherekea miaka 60 ya taifa la Izrael.
Picha ya mwisho anaonekana waziri mkuu wa Izrael, bwana Ehud Olmet. akiongea na waamdi shi wa habari, kujibu kashfa inayo mkabili yakupokea pesa kinyume cha sheria kutoka kwa mfanya biashara mmoja, ili aweze kushinda na kuwa waziri mkuu. Hataa hivyo waziri mkuu bwana Ehud Olmet, alikanusha madai haya na kudai hakufanya makosa, ijapo kuwa, kuwan wito unatolewa wa kudai ajiudhulu toka madarakani.
Pesa na mali zilizo potea kwa ubadhilifu zapatikana" Serikali ya Zambia".


Akisema hayo, waziri wa habari wa Zambia, bwana Mike Mulongoti, baadhi ya vitu vilivyo taifishwa ni nyumba ya bwana Chiluba iliyopo nchini Ubeligiji, ambayo itauzwa na fedha zake zitatumiwa kuwasaidia wanachi kukarabati hospitali,na zahanati.
Bwana Chiluba, anakabiliwa na kesi ya kutumia vibaya fedha za umma na ubadhilifu (rushwa), wakati alipo kuwa madarakani kama rais wa Zambi.
Picha hapo juu anaonekana bwana Fredrick Chiluba,akiwa mahakamani kwa mara ya kwanza kusikiliza kesi yake ya ubadhilifu wa mali ya umma.
Picha ya chini anaonekana bwana, Chiluba akitoka nje ya mahakama kusikiliza kesi inayomkabili.
Chini anaonekana bwana Fredrick Chiluba enzi hizo akiwa kama rais wa Zambia, akitembea kuelekea nyumbani baada ya kazi ngumu.
Amani bado kitendawili, jeshi ladai kuua waasi wanaopinga serikali"Kanali".



Msemaji wa jeshi,Kanali Aldophe Manilakiza, alisema ya kuwa mapigano na waaasi hawa yalitokea wakati wanajeshi walipo kuwa wakiwasaka waasi, ambao wamekuwa wanapingana na serikali ya Burundi inayo ongozwa na rais Pierre Nkurunzinza.
Pichani ni picha ya rais Pierre Nkurunzinza, siku ya kwanza alipo apishwa kuwa rais, kuhaidi kuleta amani na maelewano nchini Burundi.
Picha ya kati wanaonekana wanajeshi wakimpa kisago jamaa mmoja, ambaye anashukiwa ni mwasi anaye saidia kuleta vurugu.
Picha ya chini wanaonekana baadhi ya watu walio kimbia mapigano wakiwa wanaongea matatizo yao mbele ya viongozi wa swerikali na pembeni ni mmoja ya maasisa wa kijeshi, wakiwasikiliza kwa makini.
Urusi yapata rais mpya , nguvu mpya za kijeshi zaonekana mbele ya dunia.



Zaidi ya wanajeshi wapatao 8000 wakiongozwa na zana za kivita zenye nguvu za nyuklia na zakawaida, walipita mbele ya rais mpya wa wa Rusia, bwana Medvedev na waziri mkuu mpya wa Urusi bwana Vladamil Putin.
Maonyesho haya ni ya kwanza tangu kuvunjika kwa muungano wa jumuia ya Urusi.
Hata vivyo, rais Medvedev alionya ya kuwa watu ndio wanaosababisha vita , hivyo alisema nilazima watu wajitahidi kuepuka hali ya vita kutokea. Na alimalizia kwa kusema ya kuwa kuwa na nguvu za kijeshi ni kwa ajili ya kulinda nchi.
Juu kabisa katika picha, anaonekana amiri jeshi mkuu wa Urusi rais, Medvedev akisalimiana na wanajeshi wakati wa kukagua graride hilo.
Chini ni picha ya rais Medvedev, akiwa kwenye ofisi yake ya urais kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kuwa rais wa Urusi.
Picha ya mwisho, anaonekana waziri mkuu mpya wa Urusi, bwana Vladamil Putin , akiongea baada ya kupitishwa kuwa waziri mkuu hivi karibuni.
Lebanon yawa kidonda kingine kisicho pona, hali ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe yazuka na kuleta wasiwasi.


Mmoja wa wachunguzi wa kisisa za mashariki ya kati alisema haya.
"Kutokana na kutokuwa na amani na serikali kamili, imesemekana ni chanzo cha vurugu hizo na kusababisha kuvipa nguvu vikundi kama Hezbollah vinavyao pinga serikali, kuweza kujiamulia nini la kufanya na hatimayake kwa kutumia nguvu zake za kijeshi kukamata sehemu ya magharibi ya ya jiji la Beiruti".
Hadi kufikia sasa serikali iliyopo ambayo inasaidiwa na nchi za magharibi, imekuwa haina la kufanya na kuiacha nchi kuwa katika hali mbaya,na hali hii itasababisha kuzuka vita vya wenyewe kw wenyewe, alimalizia kwa kusema.
Hadi habari hizi zipo hewani, kundi la Hezbollah ndilo linalo shikilia sehemu kubwa ya jiji la Beiruti baada ya mapigano yaliyo chukuwa siku tatu hadi sasa.
Pichani hapo juu, linaonekana moja ya jengo linaungua kwa moto , baaada ya mapigano kati ya kundi la Sunni na Washia yaliyo tokea hivi karibuni.
Hapo chini ni picha ya baadhi ya wapiganaji wanao pigania vikundi vyao, wakiwa na ana angalia moja ya siraha ambazo ndizo zinazo tumika katika mapigano yanayo endelea.
No comments:
Post a Comment