Sunday, July 6, 2008

Venus atetea ubingwa wake,Williams wawanyota ya Wimbledon 2008.

Venus ateta ubingwa wake, Williams wawanyota ya Wimbledon 2008.

London, Uingereza - Bingwa mtetezi wa mchezo wa tenis kwa upande wa wanawake, Venus Williams ameweza kutetea ubingwa wake kwa kuweza kushinda tena kombe la mashindano ya Wembledon kwa mara ya nne, baada ya kumshinda mdogo wake Serena Williams, katika mchezo wa kutafuta bingwa wa tenis kwenye mashindayo hayo yaliyo fanyika nchini Uingereza.
Fainali hiyo iliyo udhuliwa na watu wasio pungua elfu kumi, wakiwemo aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza bi Barones Thatcher, pamoja na wageni wengine waalikwa.
Picha hapo juu anaonekana, Venus Williams akiwa ameshikilia dishi/kombe la ubingwa wa tenis la Wimbledon kwa upande wa wanawake mara baada ya kumshinda mdogo wake Serena kwa seti 7-5,6-4.
Picha ya pili wanaonekana Venus na Serena Williams, wakiwa wameshikia vikombe mara baada ya kushinda tena mchezo wa tenis kwa upande wa wanawake , ambapo hushindanisha wapinzani wawili kwa wawili.
Picha ya tatu wanaonekana Venus na Serena, wakiwa wameshikilia madishi yao mara baada ya kumaliza kupambana, mshindi alikuwa Venus.
Picha ya nne , ni ya baba ya Serena na Venus, mzee Williams, akiangalia kwa makini nini la kufanya ili watoto wake waweze kushinda, hata hivyo wakati Venus na Serena walipo kutana, mzee Williams akuangalia mechi hii na aliamua kueleka nyumbani USA, kwani alisema ya kuwa kazi yake alisha maliza nani kazi ya watoto wake kujijua nani ni mshidi kati yao.
Picha ya tano wanaonekana Venus na Serena wakimenyana kutafuta nani bingwa wa Wimbledon 2008.
Picha ya mwisho wanaonekana Serena na Venus wakiiongi uwanjani tayari kwa mpmbano wakutafuta bingwa kwa upande wa wanawake 2008 kwenye mashindano ya Wimbledon.
Maombi ya wengi yasikika, Bi, Ingrid Betancourt,yupo huru baada ya miaaka sita.
Paris, Ufaransa - Bi, Ingrid Betancourt aliwasili hivi karibuni nchi Ufaransa, baaada ya kuachiliwa huru na kundi la FARC lilipo nchini Kolombia tarehe 2/07/2008.
Bi, Ingrid Betancourt, alikuwa ameshikiliwa na kundi la moja linalo pinga ns kupigana na serikali ya Kolombia kwa kipindi kisicho pungua miaka sita.
Hata hivyo bi, Ingrid Betancourt, aliachiwa huru pamoja na mateka wengine watatu, ambao ni raia wa Amerika na wengine kumi na moja raia wa Kolombia.
Picha hapo juu wanaoneka bi, Ingrid Betancourt, akimkumbatia kwa hamu toto wake wakike wakati walipo walipo kwenda kumpokea.
Picha ya pili anaonekana, bi, Ingrid Betancourt, akiwa analia kwa furaha,baada ya kutangaziwa yakuwa hawapo tena chini ya mikono ya kundi la FARC, na wapo huru kuelekea nyimbani.
Picha ya tatu, bi, Ingrid Betancourt anaonekana akimshika mtoto wake wa kike, Merania kwa upendo, wakati walipo kuwa wakijiaandaa kutoa shukurani za dhati kwa watu wote walio shirikaana katika sara hadi alipo achiwa huru. Picha ya nne anaonekana ,bi Ingrid Betancourt, akiwa anaangalia juu na kumshukuru Mungu kwa maajabu na uwezo wake alioufanya hadi sasa yupo huru.
Picha ya mwisho chini anaonekana bi. Ingri Betancourt, akiwa pamoja na rais wa Ufaransa, bwana Nicolas Sarkozy wakati walipo kutana mara baada ya kuwasiri nchini Ufarannsa.
Hatutachanganya siasa na misaada au biashara katika bara la Afrika.
Beijing,China - Serikali ya China imesema yakuwa kuziwekea vikwazo nchi ni kinyume na haki za binadamu.
Msemaji huyo wa wa serikali, bwana Liu Guijin, ambaye ni kiongozi anayeshughulika maswala ya Afrika, alisema yakuwa China, aitachanganya siasa na uchumi katika kufanya biashara au utoaji wa misaada kwa bara la Afrika.
Hapo juu ni picha ya ramani ya bara la Afrika, ambalo limekuwa katika hali ya utata kila kunapo kucha.
Nchi tajiri duniani kukutana tena kujadili hali ya duniani.
Tokoyo, Japan - Viongozi wa nchi tajiri na zenye viwanda duniani wanakutana nchini Japan, ilikujadili hali halisi ya dunia, hasa kupanda kwa bei ya mafuta na upandaji wa bei ya vyakula na nyezo zakufanyia kazi.
Mkutano huu ambao utachukua siku tatu, vilevile utajadili hali ya ilivyo bara la Afrika na mabadiliko ya hali hewa duniani.
Nchi hizo,tajiri duniani ni, Canada, France,Germany, Itali, Russia,na Japan, Amerika na Uingereza.
Hapo juu wanaonekana polisi walikijiandaa tayari kulinda usalama wa mkutano wa nchi tajiri duniani
Irak yafutiwa madeni na nchi za jumuia ya nchi za Kiarabu.
Bagdad,Irak - Muungano wa jumuia ya nchi za Kiarabu, (UAE) , zimetangaza rasmi kufuta madeni yote ambayo yalikuwa yanaidai nchi ya Irak, ambayo yanathamani ya dola - $7billion.
Haya yametamkwa na ujumbe wa shirilikisho hilo la nchi za kiarabu, zilizo ongozwa na Sheikh Khalif bin Zayed al Nahayan.
Nawakati huu, muungano huu wa nchi za Kiarabu zimemteua bwana, Abdalah Ibrahim al Sheihhi, kuwa balozi wa jumuhia hio nchini Irak.
Shirikisho hili lilifunga ofisi zake za kibalozi nchini Iraq, baada ya aliyekuwa balozi wa nchi ya Misri kutekwa nyara na kuuwawa.
Picha hapo juu ni wanaonekana waziri mkuu wa Irak bwana Nouri Al Malik aliyea kaa kushoto, akiongea na Sheikh Khalifa aliyekaa kulia wakati walipo kutana hivi karibuni.

1 comment:

Anonymous said...

I like your story on the william sisters !!!I however do not see anything about the epic match between Nadal and Federer which is by all standards the best match of all times and one that changed the history of tennis.