Monday, December 29, 2008

Rais wa Somalia aacha madaraka"Asema ameshindwa baadaya jitihada zake kugonga ukuta"

Nchi za Kiarabu zatakiwa kuongeza juhudi kutatua mgogoro wa Palestina na Israel "Katibu waUmoja wa mataifa ". Umoja wa Mataifa,Amerika-29/12/08. Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon,amezitaka Palestina na Israel kusimamisha mapigano mara moja , na kurudi katika meza ya majadiliano. Katibu huyo, Ban Ki-moon, akisitiza hayo,alizitaka nchi za Kiaarabu kufanya kila juhudi ili kuleta amani katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza kwani juhudi wanazo zifanya hazisaidi, hivyo inabidi waongeze juhudi zaidi. Katibu Ban Ki-moon, alisema vita vilivyopo kwenye Ukanda wa Gaza, haukubaliki na jumuia ya kimataifa, hivyo lazima visimamishwe mara moja kwani vita hivyo vinaleta mazara makubwa kwa jamii na watu wa pande zotembili, Israel na Palastina kupoteza maisha yao. Picha hapo juu anaonekana, Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kikao na kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali alisi na nini kifanyike ili kuwepo na amani katika eneo la Ukanda wa Gaza. Umoja wa nchi za Afrika waonyesha makali yake"Guinea yasimamishwa uanachama".

Conakry,Guinea-29/12/08.Umoja wa nchi za Afrika (AU- African Union), umesimamisha uanachama wa nchi ya Guinea, baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi.
Mapinduzi hayo, yamekuja baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo ,Lansana Conte ambaye alitawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 24.
Picha hapo juu, ni ya bendera ya nchi za Umoja wa Afrika, ambapo jumuia hiyo, imesimamisha uanachama uanachama wa nchi ya Guinea.
Picha ya pili, anaonekana rais wa zamani wa Guinea, hayati, Lansana Conte wakati wa uhai wake akiwasalimia wanachi wakati akiwasili kwenye moja ya mikutano nchini humo.
Picha ya tatu, anaonekana, kiongozi wa sasa ambaye ni mwanajeshi, Kaptain, Moussa Dadis Kamara, akiwasalimia wanachi baadaya ya kutangaza ya kuwa rais wa nchi,(Guinea).
Picha ya nne, wanaonekna wanajeshi wakiwa wameka chini ya kifaru, baada ya jeshi kutwa madaraka, baada ya kifo cha rais, Lansana Konte.
Picha ya nne, linaonekana jeneza la rais, Konte,wakati mazishi ya kumwaga kwa mara ya mwisho, rais Lansana Konte yalifanyika jiji Konakri
Rais wa Somalia aachia madaraka"Asema ameshindwa baada ya jitihada zake kugonga ukuta".
Baidoa, Somalia-29/12/08.Rais wa Somalia, Abdullahi Yusufu Ahmed amejiuzuru nafasi yake ya urais wa kuingoza nchi hiyo ambayo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi.
Akiongea hayo, rais mstaafu, Abdallah Yusuf Ahmed,ali wakumbusha wabunge yakuwa, ikiwa ni tashindwa kazi, basi nita jiuzuru, na leo nimeamua kuikabidhi kazi mliyo nipa mikononi mwenu,na Spika wa bunge atachukua majukumu.
Picha ya hapo juu anaonekana, rais, Abdullah Yusuf Ahmed, akijifuta jasho, kwani kazi aliyo kuwa nayo hapo hawali ya kuwa rais wa Somali haikuwa nyepesi.
Picha ya pili, wanaonekana baadhi ya wapiganaji wa Kisomalia, wakiwa wameshikilia siraha, hali kama hii ilikuwa ngumu kwa raia kutimiza majukumu yake.
Amani yatoweka Ukanda wa Gaza, "Wapalestina na Waisrael, hakuna wa kutegua kitendawili"
Gaza,Ukanda wa Gaza-29/12/08.Mgogora wa Mashariki ya Kati yameingia hatua nyingine, baada ya serikali ya Israel kushambulia katika maeneo ya Gaza, kwa kutumia ndege zake, ili kuvunja kabisa nguvu la kundi la Hamas, ambalo linaongoza katika mapambano na serikali ya Israel.
Kwa mujibu wa masemaji wa serikali ya Israel,alisema imebidi kuchukua hatua hii,baada ya kundi la Hamas, kuvunja makubaliano ya kuendeleza mkataba wa amani, kwa kuanza kurusha roketi katika maeneo ya Israel.
Kufuatia vita hivyo, kiongozi wa kundi la Hamas,Khaled Meshaal, amesema atafanya mazungimzo na kundi la Fatah, kinacho ongozwa na rais rais, Mahamoud Abbas.
Picha hapo juu anaonekana, kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas, Khaled Meshaal, ametanga kwa kuwataka wafuasi wake kupigana kwa kujitoa muhanga.
Picha ya pili,anaonekana mmoja wa mkazi wa Gaza, akinyanyua juu, mwili wa mmoja wa mtoto aliye poteza maisha baada ya kupigwa na mabomu zilizo dondoshwa toka kwenye ndege za kijeshi za Israel.
Picha ya tatu, anaonekana mmoja wa mkazi wa Gaza, akiangali ni jinsi gani majengo ya maeneo hayo yalivyo haribiwa na na mabomu.
Picha ya nne, moshi unaonekana ukiwa umetanda juu,baada ya mashambulizi ya liyo fanyika Gaza.

2 comments:

Anonymous said...

Yes undoubtedly, in some moments I can say that I agree with you, but you may be inasmuch as other options.
to the article there is stationary a question as you did in the downgrade issue of this request www.google.com/ie?as_q=winsql pro 6.0.71.582 ?
I noticed the catch-phrase you procure not used. Or you profit by the pitch-dark methods of promotion of the resource. I have a week and do necheg

Anonymous said...

Τhankѕ in support of sharing such a
nice oρіnion, paragraph iѕ nice, thаts whу
і have rеad it entirely

My ωebpage ... tantric massage London
Feel free to surf my weblog ... erotic massage in London