Sunday, November 1, 2009

Uchaguzi wa Afghanistan waingia doa, mpinzani ajitoa kushiriki uchaguzi.

Waasi wa Nigeria watishia kuvunjika kwa makubaliano ya amani. Niger Delta, Nigeria - 01/11/09. Msemaji wa kundi MEND Henry Okah ambalo linapinga kuwepo kwa makampuni ya kigeni ambayo yanachimba mafuta katika eneo hilo limesema linataka makampuni yote yaliopo eneo hilo yaondoke. Akuiongea, Henry Okah, alisema yakuwa serikali ya Nigeria imekuwa haitimizi matakwa ya wanachi na wakazi wa Niger Delta, basi haitachukua muda hali itakuwa mbaya katika eneo hilo. Picha ya kwanza hapo juu wanaonekana wapiganaji wanaotete haki zao katika eneo la Niger Delta wakiwa wamshikilia siraha na wanatishia kuvunjika kwa makubaliano ya amani yaliyopo. Picha hapo juu, ni ya bendera ya Nigeria ya Nigeria, nchi ambayo eneo la Niger Delta linaleta kichwa kuuma kwa serikali ya Nigeria. Raia wa Afrika ya Kusini kuchunguzwa. Johannesburg, Afrika ya Kusini - 01/11/09. Serikali ya Afrika ya Kusini, inafanya uchunguzi ili kujua ni raia gani wa Afrika ya Kusini walishiriki katika vita vya Wapalestina na Waizrael mapema mwisho wa mwaka 2008. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema yakuwa ikiwa kuna raia wa Afrika ya Kusini alishiriki,hatachukuliwa hatua za kisheria, kwani serikali ya Afrika ya Kusini hairuhusu raia wake kushiriki vita bila ruhusa ya serikali. Picha hapo juu, wanaonekana, wapiganaji wakiwa wamepiga picha pamoja. Uchaguzi wa Afghanistan waingia doa, mpinzani ajitoa kushiriki uchaguzi. Kabul, Afghanistan - 01/11/09. Mgombe uchaguzi wa urais wa Afghanistan ,Dr Abdullah Abdullah, amesema hatashiriki katika marudio ya uchaguzi yanayo tarajiwa kufanyika tarehe 07/11/09. Uamuzi wa mgombea huyo, Abdullah Abdullah, alisema ameamua kutoshiriki, kwa uchaguzi huo hautakuwa wa haki. Hata hivyo, uamuzi huo, umekuja baada ya serikali kukataa kuwafukuza kazi baadhi ya viongozi ambao chama cha Dr, Abdullah Abdullah kiliwataka viongozi hao wafukuzwe kazi, kwa kukosa imani nao. Akiongea, mbele ya wadau na waandishi wa habari, alishangiliwa na baadaye kujibu maswali baadaye. Picha hapo juu, anaonekana, Dr, Abdullah Abdullah akiongea mbele ya waandishi wa habari kutoshiriki kwakwe katika uchaguzi mkuu wa rais utakaofanyika 07/11/09. Amerika bado kupata jibu la Wapalestina na Waizrael kuwa na amani.

Jerusalem,Izrael - 01/11/09.Waziri wa mambo ya nje wa Amerika Bi, Hillary Clinton, amemaliza ziara yake mashariki ya kati bila yakuwa na mafanikio makubwa ya kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael.
Hali hii inakuja baada ya viongozi wa Palestina na Izrael kuzidi kuvutana kufuatia madai tofauti ya kila upande, ambayo yamefanya hali ya amani katika eneo hilo kuwa na utata.
Picha hapo juu, anaonekana kushoto Bi, Hillary Clinton, na kulia ni rais wa Palestina, Mahmoud Abbas wakati walipo kuta mapema jana.
Picha ya pili anaonekana, waziri mkuu wa Izrael, Binyamin Netanyahu kushoto akiwa na Bi, Hillary Clinton wakati walipo kuwa wanaongea na waandishi wa habari.

No comments: