Monday, September 28, 2009

Miaka ya 1980s,dunia ingepatwa na mstuko mkubwa.

Miaka ya 1980s,dunia ingepatwa na mstuko mkubwa.

Havana, Kuba 28/09/09.Miaka ya 1980s, ambapo Amerika na Kuba, zilikuwa katika hali ya hatari karibu kupigana kivita,hakukuzaniwa ya kuwa hali hii,ilifikia hadi rais, wazamani wa Kuba ,Fidel Catro kuimba Urussi, kuisaidia Cuba ,kuishambulia Amerika kwa bomu la nyuklia, pindipo vita vitaanza.
Lakini kutokana na ushauri wa wataalamu wa Urussi, walimweleza ya kuwa ikiwa bomu hilo litatumika, basi hata wanachi wa Kuba wanaweza kiathirika pia.
Miaka ya 1980s, ilikuwa maka ya hatari hasa kati ya Amerika na Kuba pamoja na Urussi,na kupelekea aliyekuwa rais wa Amerika, Ronald Regan, kuizinisha mpango wa kujihami kisiraha,kwa kujihami na Urussi.
Hata hivyo,hali haikufikiwa ya kutokea vita, japo kuwa rais, Ronald Regan, alishambulia Urussi kwa maneno makali na kuiita Muungano wa nchi za Urussi ni wa kishetan.
Picha hapo juu, ni ya rais , mataafu wa Kuba ,Fidel Castro, ambaye alikuwa adui wa viongoziwa Amerika kwa muda mrefu kwa msimamo wake.
Picha ya pili, anaonekana, hayati, rais wa Amerika, Ronald Regan, ambaye wakati wa utawala wake Amerika na Kuba zilikuwa almanusla kupigana.
Tushirikiane kuepuka kutegemea nchi za Ulaya na Amerika,"marais wawakumbusha marais/viongozi wenzao".
Margarita, Venezuela - 28/09/09. Rais wa Venezuela, Hugo Chavez ,amewataka viongozi wa Afrika na Amerika ya Kusini, kushirikiana kikamilifu ili kuepuka kuzitegemea nchi za Ulaya na Amerika.
Akiongea katika mkutano huo, rais Cahvez, alisema kushirikiana kwa nchi za dunia ya tatu, kutasaidia nchi hizo kiuchumi na kuinua maisha ya watu wake.
Rais, Chavez,alisisitiza ya kuwa huu ndiyo mwazo wa kujikomboa kwa nchi za Afrika kwa kushirikiana na nchi za Amerika ya Kusini,kwani nchi hizi zina kila kitu, na kama zikishirikiana vizuri, basi karne ya 21, itakuwa ni ya kuinua uchumi wa nchi hizi.
Naye rais, wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, alisema hakuna matatizo yasiyo kuwa na majibu, hivyo basi ni muhimu kwa viongozi kukakana kutafakari na jibu litapatikana, ili kukabili hali halisi ya Afrika na Amerika ya Kusini
Kwa kuunga mkono, hoja hizo, rais wa Libya , Muammar Gaddafi, alisema inabidi kuundwa NATO ya Kusini, kwani nchi zenye nguvu, zimekuwa zikitumia nguvu zao vibaya,kwa kupoteza nafasi ya kutusaidia ,bali kututumia kama wanyama na kuaribu ardhi yetu.
Hivyo umefikia wakati wa kupigania kujikomboa kwa kila hali.
Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Venezuela, Hugo Chavez,akiongea mbele ya viongozi/marais wa Afrika na Amerika ya Kusini, wakati wakikao cha wakuu wanchi hizo.
Picha ya pili ni ya rais wa, Brazil, Lula Da Silva,ambaye alisisitiza utafakari wa kutatua matatizo.
Picha ya tatu, ni rais wa Libya, Muammar Gaddafi,ambaye alitaka nchi za Afrika na Amerika ya Kusini, kuanza kujikomboa kwa kila hali.
Hali ya usalama na amani wa Guinea mashakani
Konakry,Guinea - 28/09/09. Watu kadhaa wameuwawa na wengine kujeruhiwa baada ya polisi kupamabana na waandamanaji wanaopinga uamuzi wa mkuu wa jeshi, kugombea kiti cha urais
Mkuu huyo wa majeshi,Moussa Dadis Camara, ambaye amechukua madaraka kwa mapinduzi , baada ya kifo cha rais wa nchi hiyo Lansana Contee, ambaye alitawala tangu mwaka 1984.
Kwa mujibu wa mashaidi waliokuwepo kwenye maandamano hayo, ambayo yalianzia karibu na kiwanja cha mpira cha Konakry,walisema polisi walitumia gasi za kutoa machozi na kufyatua risasi kuelekea kwa waandamanaji.
nchi ya Guinea , imekuwa ikitawaliwa na kiongozi ambaoyealikuwa mwanajeshi na wanajeshi lilikuwa nyuma yake.
Picha hapo juu, anaonekana moja ya mwanadamanaji, akiwa chini ya ulinzi wa maafande tayari kumpeleka mung'anda.

No comments: