Monday, November 2, 2009

Umoja wa Matifa waismamisha misaada ya kijeshi nchini Kongo DRC.

Umoja wa Mataifa kusimamisha misaada ya kijeshi nchi Kongo DRC.

Kinshasa, DRC - 02/11/09. Umoja wa Mataifa umesimamisha misada iliyokuwa inatoa kulisaidia jeshi la Kongo (DRC) kwa kudai yakuwa kuan baadhi ya wanajeshi wa jeshi hilo la serikali wanakwenda kinyume na sheria za kijeshi kwa kuhusika na kutesa , kunyanya na hata kuua raia.
Akiongea, msemaji wa UN, anayeshughulikia maswala ya amani, Alain Le Roy, amesema yakuwa raia wamekuwa hawapati kulindwa na jeshi hilo, na badala yake jeshi limekuwa likienda kinyume.
"ata hivyo serikali ya Kongo DRC, imesema imekuwa inafanya uchunguzi wa kesi hisi,na haitakuwa jambo la busara kwa UN kusimamisha kulisaidia keshi la Kongo kwani kutafanya hali ya usalama kuwa mbaya"alisema waziri wa habari wa wa Kongo DRC, Lambert Mende.
Picha hapo juu, ni bendera ya Umoja wa mataifa, ambapo UN, imetangaza kusimamisha kuisaidia Kongo DRC kijeshi.
Picha ya pili, anaonekana rais wa Kongo DRC, Joseph Kabila, ambye serikali yake imekuwa inawakati mgimu wa kuijenga upya Kongo DRC,na kupambana na makundi ya wapinzani wanao pigani malia ya asili ya Kongo DRC.
Korea ya Kaskazini na Amerika bado zavutana.
Pyong Yang, Korea ya Kaskazini - 02/11/09. Serikali Korea ya kaskazini,imeitaka serikali ya Amerika kufikiara kutoa uamuzi wa haraka kama itakubali mazungumzo ya nchi hizo mbili kufanyika.
Habari kutoka wizara ya mambo ya nje ya Korea ya kaskazini,zilisema ya kuwa Korea ya Kaskazini imeweka bayana ya kuwa inataka kuzungumza na serikali ya Amerika moja kwa moja, na kama haitafanyika haraka, basi korea ya Kaskazini itaamua ni nini la kufanya.
Hata hivyo serikali ya Amerika, imekuwa inasisitiza mazungumzo yafanyike kuwa kuhusisha nchi za China, Urussi, Japan,Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini.
Picha hapo juu, wanaonekana wanajeshi wa Korea ya kaskazini wakiwa wanakula kwata katika moja ya sherehe za kimataifa za nchi hiyo.
Hamid Karzai kuwa rais wa Afghanistan.
Kabul Afghanistan - 02/11/09. Kamati ya uchaguzi wa Afghanistan, imetangaza rasmi ya kuwa Hamid Karzai kuwa mshindi wakiti cha urais kutokana na uchaguzi wa uliofanyika mapema mwezi wanene tarehe 20, ambapo matokeo ya uchaguzi huo yalionekana yakuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.
Uamuzi wa kumtangaza Hamid Karzai kuwa rais wa Afghanistan, kumekuja , baada ya mpinzani wake Dr Abdullah Abdullah kujitoa katika uchaguzi wa marudio ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe 07/11/09 kwa kudai yakuwa hautakuwa wa haki, kutokana na baadhi ya mahsrti waliyo taka kutotimizwa.
Picha hapo juu, ni ya bendera nchi ya Afghanistan, nchi ambayo hali ya kisiasa imekua katika mutata kwa muda mrefu sasa.
Picha ya pili ni kushoto, Dr Abdullah Abdullah,ambaye amejitoa katika uchaguzi wa rais na kumpa nafasi ya kutangazwa Hamid Karzai kulia kuwa rais wa Afghanistan.
Iran yataka mkataba wa nyuklia utazamwe upya.
Tehran, Iran - 03/11/09. Serikali ya Iran imetaka shirika linalo shughulikia maswala ya nguvu za kinyuklia kutizamwa upya.
Akiongea na waandishi wa habari, waziri wa mabo ya nje wa Iran, Monouchehr Mottaki, alisema ya kuwa Iran,imelitizama kiundani swala la kuitaka Iran, kupeleka nje madini yanayo tumika kutengenezea nguvu za nyuklia nje ya Iran, ili kuihakishia dunia yakuwa aina mpango wa kutengeneza bomu la nyuklia.
hata hivyo Iran, imekuwa ikisisiti yakuwa haina mpango wa kutengeneza mabomu ya nyuklia.
Picha hapo ju ni moja ya kiwanda cha kutengenezea na kuchuja madini ambayo yanatumika kutengeneza nguvu za nyuklia.

No comments: