Monday, November 9, 2009

Hatimaye Lebanon kupata serikali.

Wanaharakati na Wapalestina wavunja ukuta. Qalandiya, Palestina - 09/11/09. Wapalestina hukun wakishirikiana na wanaharakati wa kigeni wamebomoa ukuta uliojengwa kutenganisha Wapalestina na Waizrael katika eneo la mji wa Qalandiya. Wanaharakati hao na wapalestina walitumia roli na kuvuta ukuta kwa umbali wa mita mbili, kabla ya polisi wa Izrael, kuja kuwazuia. Mmoja wa wanana harakati hao, Abdullah Abu Rahma, alisema wanaona ukuta huo ni sawa ule wa Berlin, "na ikiwa leo wanaadhimisha miaka 20 tangu kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin, basi waliona ni bora kuvunja ukuta huo kwa kuadhimisha sherehe hiyo." Picha hapo juu wanaonekana, baadhi ya wanaharakatina Wapalestina wakiwa juu ya ukuta unaotenganisha Izrael na Palestina. Hatimaye Lebanon kupata serikali. Beiruti, Lebanon - 09/11/09. Waziri mkuu wa Lebanon , Saad Hariri, amkabidhi majina ya mawaziri amabo wataunda serikali ya Lebanon kwa rais wa nchi hiyo Michel Sleiman. Kuteuliwa kwa mawaziri hawa kumekuja baada ya mazungumzo marefu yaliochukuwa miezi kadhaa, kujadiliana na vyama vya upinzani ambavyo vilikataa uteuzi uliofanyaka mara ya kwanza. Serikali hiyo itakuwa na mawaziri 30,ambapo chama cha Hezbollah kimepata wizara 10. Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa vyama tofauti wakiwa katika mazungumzo ya kuunda serikali ya Lebanon itakayo apishwa kuongoza serikali. Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ,azitaka nchi za Kislaam kuisaidia nchi yake. Istambul,Turkey- 09/11/09. Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, amezitaka nchi wanachama shirikisho la nchi za Kiislaam kuisaidi Afghanistan kiuchumi na kijamii. Akiongea hayo , rais wa Hamid Karzai, alisema wananchi wa Afghanistan, wanaitaji msaada mkubwa kwa sasa, kutokana na hali halisi ya nchi hiyo, ambapo imekuwa na matatizo ya kivita kwa muda mrefu. Picha hapo juuanaonekana, rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, alipo wasili katika jiji Istambul. Maaelfu washangilia miaka 20 tangu kuvujwa kwa ukuta wa Berlin. Berlin, Ujerumani - 09/11/09. Wanachi wa Ujerumani pamoja na viongozi mbali mbali duniani wameungana kwa pamoja kushangilia miaka 20 ya kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin. Wakiongozwa na , Kanselar, Angela Markel na rais wa Ujerumani,Horst Koehler,na huku mvua kubwa ikinyesha viongozi hao na wananchi wali tembelea eneo ambalo ukuta wa ulikuwa umejengwa. Baadhi ya watu waliokuwepo kipindi hicho cha kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin, wamekuwa wakisikika wakisema "hawaamiani kama sasa ni miaka 20 imepita tangu kuvunjwa kwa ukuta huo na kuifanya nchi ya Ujerumani kuwa moja." Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu wakiwa juu ya ukuta wa Berlini, huku wakishangilia kuvunjwa kwa ukuta huo mwaka 1989.

No comments: