Tuesday, November 10, 2009

Serikali ya China kuisaidia Afrika.

Serikali ya China kuisaidia Afrika. Sharm El Sheikh, Misri - 10/11/09. Serikali ya china imesema itazipatia nchi za Afrika billions 10 za dollah ya Kiamerika kwa ajili ya kuinia na kujenga jamii zao nchi zao na kuziwezesha nchi hizo kufanya biashara na China. Akiongea hayo mbele ya viongozi wa Afrika waliohudhulia mkutano uliofanyaka nchi Misri, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao,alisema wale wanao ikosoa na kuilaumu serikali ya China, waangalie kwani China inawataaalamu zaidi ya 15,000 katika bara la Afrika, ambao wanasaidia katika nyanja mbalimbali na China haitajihusisha na maswala ya ndani ya nchi yoyote. Serikali ya nchini imeseini mikataba ya kibiashara na nchi nyingi za Kiafrika na kufikia kiwango cha asilimia 33% ya kibiashara kwa mwaka. Picha hapo juu, amnaonekana, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, akiongea mbele ya viongozi na marais wa Afrika walioudhulia katika mkutano uliofanyaka katika mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri. Charles Taylor, azilaumu nchi za Ulaya Mgharibi na Amerika. The Hague, Uhollanzi - 10/11/09. Aliyekuwa rais wa Liberial, Cherles Taylor, ameiambia mahakama ya kuwa kuondolewa kwake madarakani ulikuwa mpango wa serikali ya Amerika na nchi za Ulaya Magharibi ili ziweze kutawala upatikanaji wa mali ya asili iliyopo katiak eneo hilo. Akiongea kuelezea kukamatwa kwakwe, Charles Taylor, alisema hakuwa anaotoroka au kikimbia kutoka Nigeria,bali serikali ya Nigeria, ilishindwa kutimiza makubaliano yaliyo wekwa na rais wa wakati ule Olusegun Obasanjo yakuwa hakutakuwa na kesi zidi yake ikiwa atatoka madarakani lakini ikawa kinyume cha makubaliano yaliyowekwa. Uamuzi wa kesi hiyo huenda ikatolewa mwaka 2010 baada ya pande zote kutoa ushahidi wa kutosha mbele ya mahakama. Picha anaonekana rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor akiwa mahakamani tayari kusikiliza kesi ambazo zinamkabili. Korea ya kaskazini na Kora ya Kusini zatupiana risasi. Seoul,Korea - 10/11/09. Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini, zimelaumia baada ya wanajeshi wa nchi hizo mbili kutupiana risasi kwenye mpaka ulipo katika bahari Manjano. Mapambano hayo ambayo yalitokea 11:28 kwa saa za maeno hayo. Hata hivyo kwa mujibu wa masemaji wa serikali ya Korea ya Kusini , alisema, " Hakukua na majeruhi yoyote." Picha hapo juu, nimoj ya meli ya kivita ambayo inaaminika ilitumika kushambuliana katika ya nchi ya Korea ya Kusini na Korea ya kaskazini.

No comments: