Thursday, November 5, 2009

Rais wa Wapalestina atangaza kutogombea urais mwakani.

Rais wa Wapalestina, atangaza kutogombea urais mwakani. Ramal, Palestina 05/11/09 - Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, ametangaza rasmi yakuwa hatagombea uchaguzi wa rais ambao unatarajiwa kufanyika mapema mwaka ujao 2010. Akitangaza mbele ya waandishi wa habari, alisema ameamua hivi kufuatia vikwazo ambavyo vinakwamisha kuwepo kwa amani kati ya Waizrael na Wapalestina. Picha hapo juu, anaonekana rais wa Wapalestina, Mahmoud Abbas, akijianda kuongea mbele tya waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake wa kutogombea kiti cha urais . Wafanyakazi umoja wa mataifa nchini Afghanistan matatani. Afghanistan, Kabul - 05/11/09. Umoja wa Matifa,umetangaza ya kuwa wafanyakazi wake wote waliopo nchini Afghanistan waondoke nchini humo kutokana na hali ya usalama kuwa tata. Uamuzi huo unakuja baada ya wafanyakazi watano wa umoja wa mataifa kuuwawa hivi karibuni. Hata hivyo mwakilishi wa umoj wa matifa Kai Eide,alisema yakuwa haina maana umoja wa matifa utasimamisha misaada yake kwa Afghanistan. Picha hapo ju ni moja ya gari la umoja wa matifa, ambalo lilishabuliwa hivi karibuni.

No comments: