Waumini wa dini ya Kislaam kuelekea Mecca Kuhijji.
Mecca, Saudi Arabia - 14/11/09. Mamilion ya waumini wa dini ya Kislaam wameanza kuelekea nchini Saudi Arabi, kwa ajili ya Kuhiji na kujiswafi nia zao na kufuata maagizo ambayo Mungu aliyaagiza kupitia Mtume Muhammad SW.
Kwa mujibu wa serikali ya Saudi Arabia, hali ya usalama ipo katika hali nzuri na hakuna haja ya Waumini wa kuwa na wasiwasi.
Picha hapo juu, wanaonekana waumini wa dini ya Kislaam wakiwa katika Hijja, kwa kujiswafi.
Syria na Izrael huenda wakaanza mazungumzo ya amani.
Paris,Ufaransa - 14/11/09. Rais wa Syria, Bashar Al Assad,amesema amekutana na rais wa Ufaransa,Nikolas Sarkozy, wakati alipo tembelea Ufaransa kwa ziara ya kiserikali.
Katika ziara hiyo, marais hao walizungumzia, ni kwa jinsi gani wataanzisha mazungumzo ya kuleta amani kati ya Izrael na Syria.
Hata hivyo, rais wa Siyria, aliseama yakuwa "hatafanya mazungumzo na waziri mkuu wa Izrael moja kwa moja, itabidi Izrael kutuma ujmbe wake na Syria itatuma wajumbe wake na hapo mazungumzo yanaweza kufanyika."
Picha hapo juu anaonekana rais wa Syria, Bashar al Assad, akisalimiana na rais wa Ufaransa, Nikalas Sarkozy,wakati walipo kutana nchini Ufaransa.

No comments:
Post a Comment