Friday, May 16, 2014

Kenya yashambuliwa tena na mabomu.

Kenya yashambuliwa tena na mabomu.

Nairobi, Kenya - 16/05/2014.Wakazi wa jiji la Nairobi walishikwa na mstuko mkubwa baada ya milipuko ya mabomu kutokea kwenye soko la Gikomba ambalo ni la pili kwa ukubwa na maarufu kwa uuzaji wa nguo na bidhaa ndogo ndogo.


Akiongea baada ya tukio hilo, rais wa Kenya. Uhuru Kenyatta amesema "tutawatafuta pale walipo wale 
wote wanao husika au kuandaa kuvurga amani nchi Kenya, kwani wanafanya vitendo vya kishetani "

" Naamini kwa ushirikiano wa pamoja tutashida vita hivi zidi ya ugaidi." Asisitiza rais Kenyatta.

Milipuko hiyo ya mabomu ambayo imesababisha mauaji ya wati 12 na kujeruhi watu 90, imetokea wakati wananchi wa Kenya hasa wakazi wa jiji la Nairobi wakiwa bado na jeraha la kulipuliwa kwa eneo la maduka ya kisasa la Westgate ambapo watu 67 waliuwawa mwishoni kwa mwaka jana baada ya wapiganaji wa Al Shabab kuvamia eneo la maduka hayo.

Kenya imekuwa inakumbwa na milipuko ya mabomu ambayo kundi la Al Shabab limekuwa likidai kuhusika na  na mashambulizi yanayo tokea nchini humo ikiwa ni kupinga kitendo cha serikali ya Kenya kupeleka jeshi lake nchi Somalia ili kupambana na kundi la Al Qaeda

Hata hivyo serikali ya Kenya imekasirishwa na kitendo cha Uingereza kuwakataza raia wake kutokwenda Kenya na kuwataka wale walipo Kenya kuondoka kwa madai kuwa hakuna uhakika wa usalama wa raia hao wakati watakapo kuwa  Kenya.

Nchi mwenyeji wa kombe la dunia 2014 yavutana na wananchi.

Sao Paulo, Brazil - 16/05/2014.Waandamanaji wamepambana na polisi nchi Brazil kwa kupinga kitendo cha serikali kuaandaa michuano ya kombe la dunia, huku wanachi   walio wengi wakiwa na maisha ya kimasikini.

Maandamano hayo ambayo yamefanyika katika miji tofauti nchi humo, kuliwafanya polisi kutumia mabomu ya machozi ili kupambana na waandamanaji waliokuwa na asira huku waki imba kudai maisha bora na huku wakipindua magari yaliyokuwa barabarani pia kuvunja baadhi ya maduka.

Mmoja wa waandaji wa maandamano hayo Luana Gurther alisema " serikali inatakiwa kutumia pesa katika kujenga hospitali, shule, nyumba na kusaidia kuinua maisha ya watu, badala ya kutumia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kombe la dunia."

Maandamano hayo yamekuja baada ya hali ya maisha kuwa juu, na huku bei ya vitu kupanda bei kwa asilimia 50% .

Brazili itakuwa mwenyeji wa kombe la dunia  la mwaka huu wa 2014 na pia michuano ya michezo ya  Olimpiki ya 2016.

Umoja wa mataifa wadai ukiukwaji wa haki za binanadamu ni mkubwa nchini Ukraini.

Geneva, Uswisi - 16/05/2014. Umoja wa mataifa mestushwa na hali ya  uvunjwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchi Ukraini,  baada ya kupokea  ripoti yenye kurasa 37 ambayo imetolewa na shirika la kutete haki za binadamu la Umoja wa mataifa.

Akiongea kuhusu hali hiyo, mkuu wa kitengo cha kutete haki za binadamu Navi Pillay amesema " uvujwaji wa haki za binadamu nchi Ukraine umekuwa ukifanywa kwa wale watu ambao wamekuwa wakiandamana bila kufanya vurugu na pia na wale wasiohusika katika vurugu na huku polisi wa serikali wakiwa wanaangalia au wakati mwingine kushiriki katika kufanya matendo ya unyanyasaji."

" Hii pia imekuwa ikitokea kwa waandishi wa habari kupigwa kutekwa nyara na hata jeruhiwa kwa makusudi." Aliongezea Pillay.

Naye aliyekuwa Kansela wa Ujerumani kati ya 1074-1982 Helmut Schmidt, ameilaumu  muungano wa nchi za Ulaya kwa kusema " Nchi za muungano wa Ulaya zinavyofanya katika mgogoro wa Ukraini zinatishia kuzuka kwa vita na Urusi, kwani  kadri siku zinavyo kwenda na hali hii inazidi kuwa mbaya  na hali kama hii ilitokea mwaka 1914."

Mazungumzo hayo ya kuzilaumu nchi za muungano wa Ulaya yaliyo fanywa wakati  Kansella Helmut Schmidt alipo ongea  na gazeti la Bild hivi karibuni, ili kuona mwono wake wa hali halisi ya ushiriki wa muungano wa nchi za Ulaya katika mgogoro wa Ukraini.

Marekani yadai ikoma macho na Iran.

Al-Quads, Izrael - 16/05/2014. Marekani imeihakikishia Izrael kuwa haitaruhusu Iran kutengeneza bomu la nuklia.

Matamshi hayo yaliongewa na waziri wa Ulinzi wa Marekani  Chuck Hagel, ambaye yupo nchini Izrael kwa ziara ya kiserikali wakati  apokutana na waziri mkuu wa Izrael  Benjamin Netanyahu katika jiji la Jerusalem ambalo kwa kiarabu linajulikana kama Al-Quads.

"Napenda kuwahakikishia kuwa  Marekani ipo macho kwa kila hali ili kuhakikisha Iran haitengenezi bomu lolote la nyuklia, na kama Iran itaendelea kutosikia basi hatua kali zitachukuliwa kufuatia sheria za kimataita."

Akizungumzia kuhusu matamshi hayo ya waziri Chuck Hagel, mtaalamu wa maswala ya kidiplomasia na mwandishi wa habari wa Iran Hamid Golpira amesema"Izrael imekuwa ikikanusha kuwa haina mabomu ya nyuklia wakati ukweli unajulikana kuwa Izrael ina mabomu ya nyukila yapatayo 200, na mpaka sasa haitaki kuweka wazi japo jumuiya ya kimataifa inalikua hili, ikiwemo  Marekani."

Mvutano kati ya Marekani , washiriki wake na Iran kuhusu masuala ya kinyuklia umekuwa ukipigwa danadana katika kila vikao vinavyo fanywa vya  5+1  vya nchi za Iran, China, Ujerumani, Marekani, Ufaransa na Uingereza. kwa kutoa majibu ya sintokubaliana kila baada ya mikutano

No comments: