Thursday, May 22, 2014

Iran yadai ipo tiyari kwa majibu ya kivita.

Uchaguzi wa urais nchi Malawi wawa tumbo joto kwa rais Joyce Banda.

Lilongwe, Malawi - 22/05/2014. Rais wa Malawi Joyce Banda na ambaye anagombania tena kiti cha urais, amekutwa na wakati mgumu  baada ya kashfa kuibuka  kuwa wa Malawi imepoteza mamilioni ya pesa kutoka hazina kuu wakati wa uongozi wake.

Huku akiwa anasubiri mataokeo ya uchaguzi mkuu ambapo  zaidi ya watu wapatao millioni 7 wamepiga kura, rais Joyce Banda alilalamikia mfumo mzima wa uchaguzi kwa kudai kuwa ''kumekuwa na ukiukwaji wa kimsingi wa mwenendo mzima wa uchaguzi na mitandazo ya kuhesabia kura kuvurugwa kimakusudi.''

''Na mimi sihusiki na wizi wa millioni ya dola za Kimarekani zinazo tajwa.''

Malawi inakadiliwa kupoteza zaidi ya dola  million 30, na pia serikali ya rais Joyce Banda iliwekewa vikwazo vya misaada na na pesa kutoka nchi wafadhili tangu kutokea sintofahamu katika uongozi wake.

Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi mkuu wa Malawi Maxon Mbendera amepinga kauli hiyo ya rais banda kwa kusema '' hakuna ukiukwaji wa sheria uliovunjwa na mitandao ipo safi, na kama ingetokea tatizo basi tunayo plan B ya kluhesabu kura kwa mkono.''

Rais Joyce Banda, amekuwa na wakati mgumu kutoka kwa wapinzani wake ambao wanaongozwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Malawi  Peter Mutharika Uchaguzi mkuu wa rais na wabunge kwa pamoja nchini Malawi ulinafanyika siku moja kwa mara ya kwanza tangu Malawi kupata uhuru 1962.

Iran yadai ipo tiyari kwa majibu ya kivita.

Tehran, Iran - 22/05/2014. Serikali ya Iran imesema kuwa  itakuwa ni makosa makubwa kwa Izrael kufanya mashambulizi nchini Iran kwani  majibu ya Iran baada ya kushambuliwa yatakuwa hayana mfano.

Onyo hilo limetolewa na mkuu wa maswala ya kijeshi na ushirikiano wa kiulinzi Brigedia Ramezan Sharif kwa kusema ''Natumaini Izrael haitafanya makosa kama hayo, na wakuu wa wanchi hiyo wenye busara wanajaribu kuzuia hatua hiyo kwa kujua kuwa Iran itajibu mashambulizi ambayo dunia nzima itastuka.''

Kuongea kwa mkuu huyo wa jeshi la Iran, kumekuja baada ya kudai kuwa vitisho vinavyo fanywa na baadhi ya viongozi wa Izrael vinaangaliwa kwa makini.

Mvutano na vitisho kati ya Iran na Izrael vimekuwa vimekuwa vikiendelea huku Izrael ikidai Iran izuiwe kuendelea na mradi wake wa kinyukilia kwa madai unania ya kutengeneza mabomu yatakayo tioshia amani kwa Irzael na mashariki ya kati nzima.

Na wakati huo huo Iran kudai kuwa mradi wake wa kimnyuklia ni wa kimaendeleo ya kisayansi, na pia kudai Izrael kuweka wazi kuwa ina siraha za kinyuklia jambo ambalo mpaka sasa Izrael haija liweka wazi.

China na Urusi zawaweka ngumu Umoja wa mataifa.

Washington, Marekani - 22/05/2014. China na Uruusi zimepiga kura ya veto kwa kupinga muswada wa kutaka serikali ya Syria kupelekwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

Kura hiyo ya veto immepigwa  baada ya Ufaransa  kuwakilisha muswada huo ambao unaishutumu serikali ya Syria kuhusika na ukiukwaji wa haki za minadamu na makosa ya jinai.
Muswada huu ambao uliungwa mkono na nchi 58, uligonga mwamba uliowekwa na China na Urusi kwa madai kuwa ulikosa baadhi ya ukweli.

Akiongea baada ya kura hiyo ya veto, balozi wa umoja wa mataifa wa Urusi Vitaly Churkin alisema '' uamuzi wa kupiga kura ya veto ni mzuri kwani unania ya kupunguza mlolongo wa kuendelea vita nchini Syria ambao umekuwa ukichochewa kila kukicha.''

Syria imekuwa katika vita vya wenyewe kwa kwa kipindi cha miaka mitatu na zaidi na inakadiriwa watu zaidi ya 175,000 wamecha poteza maisha na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa.


No comments: